Kuna mtu mmoja, Yeye alikuwa amemaliza Degree ya Ununuzi na Ugavi, alikuwa akipitia wakati ngumu sana kiuchumi.
Ndoto aliyokuwa akiota na ikijirudia ni alikuwa akiota kwenye ndoto amevaa kaptula na shati la shule, anajiona anaingia darasani na kukaa na watoto darasani, mwalimu anaingia na kuwafundisha, alikuwa akihuzunika sana kuwa iweje ajione katika Hali hiyo wakati ni mtu mzima anakaribia miaka 40, afundishweje akiwa na watoto!!!
Ndoto ilipozidi kujirudia sana, aliamua kumuona mtumishi wa Mungu wa Kweli, baada ya kuombewa, ilidhihirika kuwa, NAFSI ya mtu huyo ilikuwa imefungwa na asingeweza Kutoka alipo bila maombi na kufunga Kwa muda Fulani alioelekezwa na Mtumishi wa Mungu.
Baada ya kuendelea na Maombi Kwa muda Fulani, aliota ndoto nyingine, wakati huu alijiona akiwa shule alosomea ya secondari,
Baada ya muda kupita, aliota ndoto akiwa chuo kikuu na BAADAYE aloianza kuota NDOTO zilizoendana na umri na maisha yake.
Maisha yake yalibadilika na Ugumu wa maisha uliisha na alipanda ghafula kiuchumi na sasa anamiliki makampuni yake na ameajiri watu wengi chini yake,
Angalizo: Usipuuze ndoto unayoota, Hasa ndoto ambayo ukiamka unaikumbuka.
Mtu halisi yupo ndotoni, ndoto ni HALISI,
Wachawi wakikuroga ktk vikao vyao, hawawezi kuzuia usifahamu mipango Yao maana Roho ya mtu katika Ulimwengu wa Roho inajua Kila kitu, na itakufahamisha ukilala ktk ndoto, ingawa lugha ya ndoto Huwa kimafumbo.
Muhimu ni kuwa makini na watu unaowasimulia ndoto zako.
Mfano, Mke wa mtu Fulani aliota ndoto na katika ndoto alimwona mumewe Yuko UCHI wa mnyama na watu wakimtizama Kwa dharau,
Kwa Sababu hakujua tafsiri na mtu sahihi wa kumshirikisha ndoto, alimsimulia mumewe aliyejua maana ya ndoto.
Mume alikuwa ametoka kuzini na kahaba siku kadhaa zilizopita na akafanya Siri.
Mke alipomsimlia ndoto Ile, alimdamganya kuwa ndoto hiyo ni uongo alimwambia atakuwa alikula chakula Cha kumzidi na na ndo sababu ya kuota vile.
Maisha ya mtu always hayatofautiani na ndoto anazoota Kila mara Hasa zinazojirudia.
Amen.