Msaada wa ndoto hii inayonisumbua kila siku

Msaada wa ndoto hii inayonisumbua kila siku

Habari ndugu jamaa na Marafiki,

Mimi ni kijana wa miaka 29. Nimehitimu elimu ya chuo tangu mwaka 2019, lakini nimekuwa na hari ya kutokewa na ndoto ya aina moja mara kwa mara, wakati mwingine inatokea usiku mara mbili mpaka mara tatu.

Ndoto yenyewe ni kuota niko chuoni bado nasoma na mara nyingi naota nikiwa najiandaaa kwenda kwenye chumba cha mtihani , na kibaya zaidi ninakuwa sijasoma kabra ya mtihani , sasa hofu yake inakuwa ni kubwa sana.

Wakati mwingine ninakuwa katika chumba cha mtihan lakni kinachonishangaza ni kwamba huo mtihani huwa sianzi kuufanya huwa tu kwenye mazingira ya mtihan ila kuunza kufanya ndo hamna nastuka natetemeka sjasoma.

Kama kuna mtaalamu wa kiroho au mjuzi wa kutafsiri ndoto naomba anipe mwanga kidogo maana hii ndoto inanitesa sana.

Naomba kusasilisha[emoji120][emoji120]

dreams can act as overnight therapy, a night shift designed to help us process difficult emotions.

Wasome hawa watu anaitwa allan hobson, william domhoff, rosalind cartwright,
 
Ndoto ya kawaida tu mkuu usiogope endelea na maisha yako, wanaokwambia sijui umerogwa ni wana imani potofu tu...! Na we ukiiingia kwenye huo mtego itakula kwako, ndoto ya aina hiyo inaotwa na watu wengi sana duniani kote, kwa hiyo watu wote hao wanakua wamerogwa???
Dah sawa mkuu, tunapeana moyo maana wanasema tatizo ukiambia watu ni nusu ya kulitatua.
 
Ndoto ya kawaida tu mkuu usiogope endelea na maisha yako, wanaokwambia sijui umerogwa ni wana imani potofu tu...! Na we ukiiingia kwenye huo mtego itakula kwako, ndoto ya aina hiyo inaotwa na watu wengi sana duniani kote, kwa hiyo watu wote hao wanakua wamerogwa???

Mkuu Umenikumbusha nilikuwa na mchumba tunaangalia toy story hii ni cartoon kutoka disney ina unicorn ndani yake,
sasa tumekaa baada kama baada ya wiki hivi ananiambia nimeota wanyama wa ajabu wananikimbiza halafu nafika mwisho kama wa korongo ni kama pundamilia hivi halafu ana pembe MOJA,
Nikamwambia umesahau kama tuliangalia cartoon hivi vitu ni vya kawaida
Wabongo wanakwambia usharogwa
 
Hapo kiroho uko nyuma..yani kimwili unaishi miaka ya sasa..ila kiroho kuna vitu vinakurudisha nyuma ..ukipuuza ni utapigika life yako yote
 
Nitajaribu pia na hii boss.
Hii uhakika Sana mazee ..
Ukitaka kujaribu kalale hata lodge ya jirani na hapo uone kama utaota hizo ndoto...asijue mtu hata mmoja unaenda kulala wapi...hata mkeo...
Jaribu Kama mara 2 utaniambia
 
Hii uhakika Sana mazee ..
Ukitaka kujaribu kalale hata lodge ya jirani na hapo uone kama utaota hizo ndoto...asijue mtu hata mmoja unaenda kulala wapi...hata mkeo...
Jaribu Kama mara 2 utaniambia
Ahsnte sana aise, ngoja nijaribu leo leo tu maana ndoto ishakuwa kero hii.
 
Back
Top Bottom