Msaada wa tafsiri ya ndoto ya kurudi shule mara kwa mara

Hapo ukute unaota kesho mtihani wa taifa halafu hujajiandaa hukumbuki topic yoyote.

Ila ndoto hiyo ukiamka unapata afueni, inakukumbusha tu maisha yote ni shule na unatakiwa kujiandaa muda wote.
 
Mm pia nlikua naota sana hivo, nikafuatilia majibu yake ni kuwa ntapata shida ya fedha na kweli sasa hivi nimefulia sana na madeni juu, kwa hio na ww jiandae, usitumie ovyo pesa, kuwa makini na vitu unavyonunua na pia usikopeshe watu pesa zako watakutia unyonge
 
Upo mkoa gani? Ni ugenini au nyumbani?
 
Mimi pia kuna ndoto nimeota zaidi ya mara 20,nakutana na viongozi mbalimbali ndotoni tunaongea then tunaachana,mpk nashangaa wakati mazingira yangu siwezi ktk kukutana nao,naota sana tena viongozi tofauti tofauti,wakuu wa mhimili mkubwa zaidi 3 nimewahi waota pia na baadhi mawaziri.
 
Spirit of setback and delay.
 
Hapo ukute unaota kesho mtihani wa taifa halafu hujajiandaa hukumbuki topic yoyote.

Ila ndoto hiyo ukiamka unapata afueni, inakukumbusha tu maisha yote ni shule na unatakiwa kujiandaa muda wote.
Hii huwa inanitokea sana tu mara nafanya mtihani wa Taifa mpaka muda unakaribia kuisha sijajibu swali lolote, au najikuta naamka late nawaona wenzangu wanatoka kwenye SoMo ambalo na mm nilitakiwa nilifanye muda huo yaan nawewezeka mpaka nashtuka na ukiangalia O level, advance na chuo nimepita vizur tu bila vikwazo japo maisha yangu Bado hayako sawa
 
Mkuu, kwanza pole kwa ndoto za aina hii. Nadhani umeona ndoto unayoota, watu wengi hapa wameshuhudia kuwa nao wanaiota. Kwanini watu wengi waote ndoto hii (kama zinatofautiana basi ni kidogo sana) moja? Mimi pia nimeota ndoto hizi mara kadhaa. Nadhani hili sio la kupuuzia, kama ambavyo baadhi ya watu wamesema. Kwanini watu wengi waote ndoto moja?

Naungana na wadau wengine waliochangia hapo mwanzo kuwa, ndoto za shule zinamaanisha unatakiwa ukimaliza (ukihitimu), ukaitumie elimu hiyo kwa manufaa yako na watu wengine; iwe ajira (kazi), biashara, nk. Hata maandiko matakatifu yanasema: Daniel kabla hajapelekwa kutumikia katika jumba la mfalme, alipatiwa mafunzo (shule) kwa muda maalumu. Kumbe tunaona baada ya shule, basi tufanye kilichokusudiwa.

Kwako wewe, kwenye ndoto yako umewaona watu uliiosoma nao huko nyuma, hao wenzako (uliowana kwenye ndoto), kwa sasa wapo mbali kimafanikio, japokuwa mlianza wote katika harakati za maisha, ikiwa ni pamoja na kusoma, lakini kuna mahala wewe ulikwama wakati wenzako wanapiga hatua. Hivyo ndoto hii inatukumbusha tusijisahau, bado tuna safari ndefu.
 
Umeandika urithi? Kama bado fanya hivyo haraka sana. Na ukifika huko uendapo mwambie anko magu mambo yamekua mazuri sana tz
 
unaenda kushuka kiuchumi,watu wagiza wameamua kurudisha maisha yako nyuma ili usikumbane na ghasia hii fanya maombi ya kujikomboa wewe na familia yako kiuchumi
 
Napojaribu simulia watu baadhi Yao huniambia Wenda nachezewa mkuu na Mimi siamini Sana katika Mambo hayo
Si kweli mwaya,kwasababu si wewe pekee unaeota hivyo,ni wengi nikiwemo na mim mwenyewe,sema tunatofautiana tu matendo tunayokua tunafanya hapo shule.Mim iliku naota primary school ticha wa hesabu anatufundisha std 4 kwa wiki naota mara 5,sku zngne naota nafanya pepa ya 4m4 na mda unakarbia kuisha me bado maswal meng sijajaza, mara ya mwisho niliota nafanya pepa la chuo(tokea hapa sijaota tena nipo shule).

Nimesahau group moja fb ningekuwekea link,kunamdau aliuliza kama wewe ulivouliza,hii ndoto watu weng comment karbu 500 na zaid watu walisema nao hua wanaota. Sasa hao wote WANACHEZEWA?? Kama ni hvo basi tanzaland tunawachawi wengi na wenye wivu sana. Na mpaka uchezewe wewe unakipi cha ziada??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…