Hii ndoto huwa si nzuri inatoa Ishara ya kuandamwa na Roho ya kurudishwa Nyuma kimaisha(Regression spirit).na mie ndoto za aina hiyo ziliwahi kunisumbua sana nikiota nipo darasani O.level (Wakati huo Shule ngazi hiyo nilikuwa nimeshamaliza kama miaka 20+ iliyopita) na wakati huo nilishamaliza Master Degree,lkn ndoto za Sekondari zinajirudia.Habari Wana Jamiforums natumani mko poa kabisa.
Kuna ndoto moja ina inanitesa Sana nimeona bora leo nilielezee hapa jukwaani angalau niweze kupata ufafanuzi kidogo kuhusiana na ndoto hii ninayo ota ikijirudia Mara kwa Mara kila Napo lala usiku.
Nimuda Sasa yapata Kama miaka Saba tangu nihitimu elimu ya sekondari lakini licha ya muda mrefu kidogo kupita tangu nimemaliza kidato Cha nne nimekua nikiota ndoto zikionesha kuwa nimerudi shule nasoma pia mazingira ya shule ni yale yale walimu wanafunzi wenzangu pia niliosoma nao ni wale wale.
Kiufupi naota ndoto hii imekua ikijirudia Sana na siku zinavyozidi kwenda nazidi Kuota hii ndoto na chaajabu ndoto hii uonesha kua nimerudi shule na wenzangu nimekuta wanaendelea na masomo Kama kawaida huku me nikionekana nilikua mtoro sihudhurii masomo yanayoendelea kwa Sasa katika kipindi icho ambacho Mimi nipo uraiani nimeshamaliza shule.
NB.
- Ndoto zote naota nipo tu sekondari wala sio shule ya msingi ama chuo
- Ndoto nyingi huwa naota nikiwa katika kipindi Cha kutaka kuadhibiwa wa mwalimu au kuhaibishwa mbele ya wanafunzi wenzangu
- Kwa mwezi naweza ota mara2 hadi tatu ndoto za aina hiyo ya kurudi shule.
kwa anaejua maana ya ndoto hii wakuu anisaidie tafsri yake Nini na kwanini ijirudie Mara kwa Mara ndoto Aina moja, inanitesa Sana kiukwel wakuu nakosa Raha naposhtuka usingzini baada ya Kuota ndoto hii na kichwa uwa kizito Sana. Nifanyeje ili niweze ondokana na ndoto hii?
Kila nilipokuwa nikiota ndoto hizo nilikuwa nakutana na Hali ya ku- struggle sana kazini na kupatwa changamoto mbalimbali kwenye upatikanaji wa Fursa ya Fedha au mahusiano na mabosi au wafanyakazi wenzangu mahala nilipokuwa nafanyia.kazi.
Cha kushangaza sikuwahi kuota nipo darasani 'A' Level au University,lkn za O-Level ndo zilikuwa zimenikomalia.
KIBAYA ZAIDI,Kuna kipindi nikaota nipo maeneo ya Shule ya Sekondari (O-Level) nikaona baadhi ya Majengo ya Classrooms za Shule yamebomoka kutokana na tetemeko la aridhi.haikupita hata wiki moja toka niote ndoto hiyo nikapata changamoto kazini.kwangu wakati huo(tena Kwa kubambikwa) mpaka NIKASIMAMISHWA KAZI(Suspension from duties).Hata hivyo ,baada ya hapo nilijikita sana kwenye kumuomba Mungu,na baada ya muda mfupi ikaundwa kamati ya uchunguzi na nikasafishwa na kurudishwa kazini.
Namshukuru Mungu,nina miaka kadhaa sijakutana na ndoto za kuwa Sekondari na mambo yapo shwari hivyo Nakushauri Kwa Imani yako muombe Mungu akuepushe na Roho hiyo ya kurudishwa Nyuma whether imekuja naturally au kutokana na vitendo vya kipepo vya wasiokutakia mema