Msaada wa tafsiri ya ndoto ya kurudi shule mara kwa mara

Hii ndoto huwa si nzuri inatoa Ishara ya kuandamwa na Roho ya kurudishwa Nyuma kimaisha(Regression spirit).na mie ndoto za aina hiyo ziliwahi kunisumbua sana nikiota nipo darasani O.level (Wakati huo Shule ngazi hiyo nilikuwa nimeshamaliza kama miaka 20+ iliyopita) na wakati huo nilishamaliza Master Degree,lkn ndoto za Sekondari zinajirudia.
Kila nilipokuwa nikiota ndoto hizo nilikuwa nakutana na Hali ya ku- struggle sana kazini na kupatwa changamoto mbalimbali kwenye upatikanaji wa Fursa ya Fedha au mahusiano na mabosi au wafanyakazi wenzangu mahala nilipokuwa nafanyia.kazi.
Cha kushangaza sikuwahi kuota nipo darasani 'A' Level au University,lkn za O-Level ndo zilikuwa zimenikomalia.
KIBAYA ZAIDI,Kuna kipindi nikaota nipo maeneo ya Shule ya Sekondari (O-Level) nikaona baadhi ya Majengo ya Classrooms za Shule yamebomoka kutokana na tetemeko la aridhi.haikupita hata wiki moja toka niote ndoto hiyo nikapata changamoto kazini.kwangu wakati huo(tena Kwa kubambikwa) mpaka NIKASIMAMISHWA KAZI(Suspension from duties).Hata hivyo ,baada ya hapo nilijikita sana kwenye kumuomba Mungu,na baada ya muda mfupi ikaundwa kamati ya uchunguzi na nikasafishwa na kurudishwa kazini.
Namshukuru Mungu,nina miaka kadhaa sijakutana na ndoto za kuwa Sekondari na mambo yapo shwari hivyo Nakushauri Kwa Imani yako muombe Mungu akuepushe na Roho hiyo ya kurudishwa Nyuma whether imekuja naturally au kutokana na vitendo vya kipepo vya wasiokutakia mema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…