AGROPRODUCT
JF-Expert Member
- Apr 2, 2023
- 290
- 952
Ni pale ambapo bank inatoa mikopo Kwa wateja wake na kufanya deposit kwenye account zao, piya pale ambapo bank Ina nunua. Bonds or treasury bills (securtie) Pesa kuingia kwenye mzunguko, wao wanapata Riba na faida kupitia hiyo mikopo or hizo dhamanaAhsante mkuu nimekuelewa...unaweza ukaongelea pia process ya Credit Creation inavyokuwa?
Piya Commercial Bank zinaweza fanya Creation of money through. Current account, watu Wana deposit cash kwenye account zao wao wanaokuwa wanatumia Cheque kufanya malipo na Kwa Sasa mambo ya digitalization ni mwendo wa internet banking, debit card(viza)Ni pale ambapo bank inatoa mikopo Kwa wateja wake na kufanya deposit kwenye account zao, piya pale ambapo bank Ina nunua. Bonds or treasury bills (securtie) Pesa kuingia kwenye mzunguko, wao wanapata Riba na faida kupitia hiyo mikopo or hizo dhamana
Unaweza ukaongezea nondo kidogo hapaPiya Commercial Bank zinaweza fanya Creation of money through. Current account, watu Wana deposit cash kwenye account zao wao wanaokuwa wanatumia Cheque kufanya malipo na Kwa Sasa mambo ya digitalization ni mwendo wa internet banking, debit card(viza)
Baadala ya cash
Shukrani sana nitaleta mrejesho jinsi nilivyoielewa hii ConceptCredit Creation: Basics Concepts, Limitations and Questions
Credit creation separates a bank from other financial institutions. In simple terms, credit creation is the expansion of deposits. And, banks can expand their demand deposits as a multiple of their cash reserves because demand deposits serve as the principal medium of exchange.www.toppr.com
I canβt explain the concept better than that βοΈ
Kuanzia mwanzo umeenda chaka ila hiyyo sentensi ya mwisho ni sahihi sema hujamalizia bado kuonesha kwanini kufanya hivyo ni kucreate money.Jinsi ninavyo jua
Kuweka bure kutoa gharama
Mfano weka 10,000 toa 8000
2000 wamebak nayo
Charges and fees
Monthly fees
Statement fees
Balance fees
Card fees
LOAN INTEREST
KOPA
MILLION 10 LIPA 15
WAKAT HUO UMEKOPA ELA AMBAYO MWENZAKO AMEWEKA SAVING
Saw mkuu ila unge ni correct,Kuanzia mwanzo umeenda chaka ila hiyyo sentensi ya mwisho ni sahihi sema hujamalizia bado kuonesha kwanini kufanya hivyo ni kucreate money.
Sawa mkuu niwie radhi. Labda kwa kuanzia kuna mkanganyiko nauona kwenye msingi wa swali lako kama nitakavyoelezea.Saw mkuu ila unge ni correct,
Labda unatak kusema zle bank charges za bank haziwapatii pesa?
Habari wakuu, natumaini mnaendelea vizuri kabisa
Katika harakati za kuendelea kujifunza nimekutana na hii kitu ambayo inaitwa Credit Creation ambayo ndo inasemekana kuwa ndo njia ambayo hizi banks wanatumia kucreate money
Hii Concept imeniwia vigumu sana kuielewa kwani ina kamkanganyiko fulani. Ninaomba kwa anayeielewa vizuri hii Concept atueleweshe nina imani sio mimi tu pia itawasaidia wengine ambao hawakuwa wanaielewa.
Karibuni sana.
Saw mkuu ila unge ni correct,
Labda unatak kusema zle bank charges za bank haziwapatii pesa?
kwako TZ-1 soma tena (nime edit comment ili kuongeza ufafanuzi zaid)Sawa mkuu niwie radhi. Labda kwa kuanzia kuna mkanganyiko nauona kwenye msingi wa swali lako kama nitakavyoelezea.
1. Kwa upande wako naona umetumia term "creation of money" by banks kama "benki kupata pesa, yani banks zinafanyaje mpaka zinatengeneza pesa (mapato).
2.Lakini kiuchumi hiyo term "creation of money" by banks inamaanisha jinsi gani banks zinafanya the general amount of money in the economy (and its effects) kuwa kubwa kuliko pesa ambayo Central Bank ya nchi husika imeitoa kwenda kwenye mzunguko wa uchumi mostly through hizi banks za kawaida.
Sasa mimi nilijibu kwa kuzingatia muktadha wa pili huo hapo juu kuhusu the term "creation of money"
Kama ulimaanisha jinsi gani banks zinatengeneza mapato basi uko sahihi, lakini term "creation of money" by banks mimi nimeongelea huo muktadha wa pili ambao ndo nakutana naao zaidi kwnye mambo ya uchumi.
Asante.
Ila bank tunakopeshan pesa zetu wenyew ila riba ya mkopo ni kubwa kulko interest for savingskwako TZ-1
Kwa kuongezea ngoja niweke mfano mmoja kuhusu how banks create money kwa
Mteja A ameweka (deposit) TZS 100,000 kwenye bank, kwahiyo mteja A akilini mwake anajua ana TZS 100,000 yake iko bank. na kimsingi sio tu kujua akilini mwake ana TZS 100,000 bali ni kweli muda wowote anaweza kufanya muamala wowote ndani ya hiyo laki moja.
Sasa anakuja mteza B ambaye ana TZS 0 kwenye account na mfukoni mwake pia.. Sasa mteja B anaenda benki kupata mkopo. Katika ile TZS 100,000 ambayo iko mikononi mwa benki (ambayo mteja A aliweka) benki inaweza kukopesha mpaka maybe TZS 90,000 (90%) ya ile deposit iliyowekwa na mteja n.b asilimia ya kiwango jcha juu zaidi ambayo benki inaweza kukopesha kutokana na deposits iliyo nayo inategemea na regulatory requirements za regulatory authority/ Central Bank. ya nchi husika, kwa Tanzania ni BoT. Kwahiyo mteja B anakwenda bank na kukopa TZS 90,000 na akapewa.
Kwahiyo mpaka hapo myeja A anajua ana TZS 100,000 benki na kimsingi anaweza kuifanyia muamala wowotw. pia na mteja B anajua sasa ana TZS 90,000 benki na anaweza kuifanyia muamala wowote. Kwa hiyo mpaka hapo kwenye uchumi kwa kuzingatia hawa wateja wawili A na yule B kuna TZS 190,000 ambayo inaweza kutumika kwenye transaction yoyote na shughuli za kiuchumi. Kwaio Central Bank iliingiza TZS 100,000 kwenye mzunguko wa uchumi ila sasa kwenye uchumi sasa kuna TZS 190,000. Kwaio hapo benki imecreate money ambayo ndo ile TZS 90,000 iliyoikopesha kwa mteja B. So ilitoka TZS 100,000 ila sasa ipo TZS 190,000.
Kwa hiyo ndio kama hivyo.
Asante.
Kwa hii hoja yako riba ambayo anatakiwa kulipa mteja B aliyekopeshwa inakuwa kubwa zaidi ya interest watakayokupa kwenye savings zako (au tuseme ya mteja Ayule) ili benki ziweze kucreate money lakini zipate faida pia mkuu, na zenyewe haziwezi kusurvive bila kupata faida sasa mkuu. Kuna gharama kushughulikia iyo process ya creation of money kuna wafanya kazi, Information Technology (IT) systems, consultants etc. . Sasa inadibi yule mteja B awekeze kwenye shughuli ambayo italeta faida zaidi ya kiasi cha riba ambacho mteja B atailipa benki baada ya kupewa huo mkopo.Ila bank tunakopeshan pesa zetu wenyew ila riba ya mkopo ni kubwa kulko interest for savings
Saving return interest 1.5 up to 3% per year
Loans interest 9 had 17% per year
Mkuu umeelezea vizuri sana na huo ndo ulikuwa msingi wa swali langukwako TZ-1 soma tena (nime edit comment ili kuongeza ufafanuzi zaid)
Kwa kuongezea ngoja niweke mfano mmoja kuhusu how banks create money kwa
Mteja A ameweka (deposit) TZS 100,000 kwenye bank, kwahiyo mteja A akilini mwake anajua ana TZS 100,000 yake iko bank. na kimsingi sio tu kujua akilini mwake ana TZS 100,000 bali ni kweli muda wowote anaweza kufanya muamala wowote ndani ya hiyo laki moja.
Sasa anakuja mteza B ambaye ana TZS 0 kwenye account na mfukoni mwake pia.. Sasa mteja B anaenda benki kupata mkopo. Katika ile TZS 100,000 ambayo iko mikononi mwa benki (ambayo mteja A aliweka) benki inaweza kukopesha mpaka maybe TZS 90,000 (90%) ya ile deposit iliyowekwa na mteja n.b asilimia ya kiwango jcha juu zaidi ambayo benki inaweza kukopesha kutokana na deposits iliyo nayo inategemea na regulatory requirements za regulatory authority/ Central Bank. ya nchi husika, kwa Tanzania ni BoT. Kwahiyo mteja B anakwenda bank na kukopa TZS 90,000 na akapewa.
Kwahiyo mpaka hapo myeja A anajua ana TZS 100,000 benki na kimsingi anaweza kuifanyia muamala wowotw. pia na mteja B anajua sasa ana TZS 90,000 benki na anaweza kuifanyia muamala wowote. Kwa hiyo mpaka hapo kwenye uchumi kwa kuzingatia hawa wateja wawili A na yule B kuna TZS 190,000 ambayo inaweza kutumika kwenye transaction yoyote na shughuli za kiuchumi. Kwaio Central Bank iliingiza TZS 100,000 kwenye mzunguko wa uchumi ila sasa kwenye uchumi sasa kuna TZS 190,000. Kwaio hapo benki imecreate money ambayo ndo ile TZS 90,000 iliyoikopesha kwa mteja B. So ilitoka TZS 100,000 ila sasa ipo TZS 190,000.
Kwa hiyo ndio kama hivyo.
Na ndomana banks zina umuhimu sana kwenye uchumi kwani zinaweza kucreate money kama hapa ambapo TZS 90,000 imekuwa created na hiyo bank ya kawaida kwenda kwenye shughuli za kiuchumi, TZS 90,000 ya ziada imekuwa created na bank ya kawaida kutoka kwenye TZS 100,000 iliyotolewa na Central bank. Na ndomana banks zinasimamiwa ili ziwe efficient kwenye iyo process ya kucreate moneywani inaweza kucreate money zaidi ya amount of money iliyotolewa na Central Bank ya nchi (Benki Kuu ya Nchi) hivyo shughuli za kiuchumi zinawezeshwa kupanuka zaidi ya kiiasi cha pesa kilichoingizwa na Cantral bank kwenye mzunguko. Maana jamii ikipoteza trust/kuziamini banks basi jamii itapunguza au kuacha kabisa kutunza pesa zao kwenye hizi bankss hivyo creation of money itapungua na hivyo shughuli za kiuchumi kushindwa kupanuka zaidi ya ile hela iliyotolewa na Benki Kuu ya nchi husika kuingia kwenye mzunguko wa uchumi, hivyo ukuaji wa uchumi wa nchi utapungua.
Sijui imeeleweka wakuu!!
Asante.
Hahaha asante sana mkuu π π πMkuu umeelezea vizuri sana na huo ndo ulikuwa msingi wa swali langu
Lakini nina maswali yafuatayo
1.Mfano mtu amedeposit kiasi cha Tsh 100000 na benki ikaweka 10% kama reserve then wakaacha 90000 kama loanable fund.Je mtu aliyedeposit mwanzo akirudi kutoa pesa yake Bank zitakuwa na Pesa ya kukopesha tena?
2.kuna mdau hapo juu ametuma articles ambayo inaelezea Creation of money.Humo wanasema kuwa Credit Creation inaweza kufanyika either Katika single bank or katika banking system Hapo nahisi umeelezea upande wa single bank only unaweza ukaelezea pia katika banking system inakuwaje??
3.katika huo mfano ulioelezea ni kwamba mtu atakayeenda kukopa pesa...huwa anapewa kwa style gani?...Ni cash au??
Karibu mkuu utupe maarifa
Dash mkuu umemaliza kila kitu aisee kweli JF ni chimbo la magreat thinkerHahaha asante sana mkuu π π π
Unajua kwanini nimecheka? muda si mrefu kuna wazo lilipita kichwani mwangu nikasema kuna mkuu kule jamiiforums anaweza kuuliza swali hili lako kwamba vp sasa yule mteja A akija kutaka ile TZS 100,0000 yake, je bank itawezaje kumpa iyo TZS 100,000 wakati tayari wamechukua TZS 90,000 katika pesa hiyo wamemkabidhi yule mteja B kama mkopo na maybe alivyokopeshwa huyo mteja B tayari sasa ameshaanza kudraw (kutoa pesa hapo bank), ile pesa aliyoikopa kutoka hapo bank? na si hapo tu bali zaidi ni kwamba na baada ya hapo vp bank itapata wapi pia hela za kukopesha tena wateja wengine? (swali lako)
Nimechangia kuongeza swali jingine kwenye swali lako nimelibold hapo juu.
Sasa mkuu jibu ni rahisi sana. Angalia mifumo ifuatayo hapa chini: -
1. Ratiba za madaladala, maboti, ndege, treni na mifumo mingine ya usafiri; na
3. Ratiba za wagonjwa kuumwa.
Kuna mifumo mingi tu ya maisha ya kila siku yametengenezwa na Mungu Mkuu wa Mbinguni (Kwa wasioamini Mungu basi chukulia tu kama mifumo iliyotokea hata ki bahati bahati tu ILA NAJUA UNAUHAKIKA kuwa mifumo hiyo ipo.
1. Sasa hiyo mifumo iko almost balanced (kuna adjustments zinaweza kutokea zinazotokana na matukio/events nyengine) au basi jiulize vp kama kesho wakazi wote wa Dar es Salaam tuamke na wote tutoke labda TEGETA na wote tunataka kutoka hapo TEGETA twende POSTA hiyo siku itakuwaje? Ile ya kufungwa kwa JANGWANI tu watu walijionea kutoka POSTA au K/KOO kufika TEGETA ilivyokuwa . ni gari haziendi,. Naikumbuka vizuri ile kufungwa kwa JANGWANI iliyotokea mwaka I think around mwaka 2020 mwishoni au 2021 mwanzini ikla nakumbuka kama ilitokea mwaka 2020 mwiahoni, watu walifika majumbani mwao USIKU WA MANANE ila bahati nzuri keshoi yake ilikuwa ni sikukuu hivyo wafanya kazi na wanafunzi wemgi walikuwa hawalazimiki kwenda kazini /shuleni.
HIYO NI NADRA KAMA KUTOKEA KWA MAFURIKO MAKUBWA au mpaka TSUNAMI hivyo kuna errors hapa na pale:
Ila kimsingi misingi ya dunia iko hivyo almost balanced kwamba kila mtu ana ratiba zake ila mwisho wa siku mifumo hiyo inajikuta ipo almost balanced. huyu anatoka Posta kwenda Tegeta na mwengine anatoka Tegeta kuelekea Kawe, hivyo hivyo mpaka mfumo mzima unakuwa wote balanced. Mfano wa pili jiulize kama waTanzania wote 60+ million tukiumwa siku moja na kwa wakati mmoja je hospitali zitaweza kutuhudumia? Hapana. Ila inatokea huyu kaumwa leo na yule kaumwa kesho yake ndo hivyo mpaka mzigo wa wagonjwa hospitali unakuwa almost balanced.
Basi ndo hivyo hivyo kwenye mabenki, huyu akija kutoa ile TZS 100,000 mwengine anakuja kuweka TZS 120,000 hivyo hivyo mpaka kiasi cha pesa kilichopo kwenye mabenki kinakuwa almost balanced, na kuna vipimo na sheria zipo kucontrol kiasi gani cha pesa au mali zinazoweza kubadilishwa kuwa posa kirahisi benki iwe nayo wakati wote ili isitokee tukio kama hilo uliloongelea.
2. Katika banking system ni hivyo hivyo.
3. Mara nyingi huwa inabidi ufungue au uwe na account katika bank unayoenda kukopa then wataweka hela humo kwenye account.