Mkuu umeelezea vizuri sana na huo ndo ulikuwa msingi wa swali langu
Lakini nina maswali yafuatayo
1.Mfano mtu amedeposit kiasi cha Tsh 100000 na benki ikaweka 10% kama reserve then wakaacha 90000 kama loanable fund.Je mtu aliyedeposit mwanzo akirudi kutoa pesa yake Bank zitakuwa na Pesa ya kukopesha tena?
2.kuna mdau hapo juu ametuma articles ambayo inaelezea Creation of money.Humo wanasema kuwa Credit Creation inaweza kufanyika either Katika single bank or katika banking system Hapo nahisi umeelezea upande wa single bank only unaweza ukaelezea pia katika banking system inakuwaje??
3.katika huo mfano ulioelezea ni kwamba mtu atakayeenda kukopa pesa...huwa anapewa kwa style gani?...Ni cash au??
Karibu mkuu utupe maarifa
Hahaha asante sana mkuu 😂 😂 😂
Unajua kwanini nimecheka? muda si mrefu kuna wazo lilipita kichwani mwangu nikasema kuna mkuu kule
jamiiforums anaweza kuuliza swali hili lako kwamba
vp sasa yule mteja A akija kutaka ile TZS 100,0000 yake, je bank itawezaje kumpa iyo TZS 100,000 wakati tayari wamechukua TZS 90,000 katika pesa hiyo wamemkabidhi yule mteja B kama mkopo na maybe alivyokopeshwa huyo mteja B tayari sasa ameshaanza kudraw (kutoa pesa hapo bank), ile pesa aliyoikopa kutoka hapo bank? na si hapo tu bali zaidi ni kwamba na baada ya hapo vp bank itapata wapi pia hela za kukopesha tena wateja wengine? (swali lako)
Nimechangia kuongeza swali jingine kwenye swali lako nimelibold hapo juu.
Sasa mkuu jibu ni rahisi sana. Angalia mifumo ifuatayo hapa chini: -
1. Ratiba za madaladala, maboti, ndege, treni na mifumo mingine ya usafiri; na
3. Ratiba za wagonjwa kuumwa.
Kuna mifumo mingi tu ya maisha ya kila siku yametengenezwa na Mungu Mkuu wa Mbinguni (Kwa wasioamini Mungu basi chukulia tu kama mifumo iliyotokea hata ki bahati bahati tu ILA NAJUA UNAUHAKIKA kuwa mifumo hiyo ipo.
1. Sasa hiyo mifumo iko
almost balanced (kuna adjustments zinaweza kutokea zinazotokana na matukio/events nyengine) au basi jiulize vp kama kesho wakazi wote wa Dar es Salaam tuamke na wote tutoke labda TEGETA na wote tunataka kutoka hapo TEGETA twende POSTA hiyo siku itakuwaje? Ile ya kufungwa kwa JANGWANI tu watu walijionea kutoka POSTA au K/KOO kufika TEGETA ilivyokuwa . ni gari haziendi,. Naikumbuka vizuri ile kufungwa kwa JANGWANI iliyotokea mwaka I think around mwaka 2020 mwishoni au 2021 mwanzini ikla nakumbuka kama ilitokea mwaka 2020 mwiahoni, watu walifika majumbani mwao USIKU WA MANANE ila bahati nzuri keshoi yake ilikuwa ni sikukuu hivyo wafanya kazi na wanafunzi wemgi walikuwa hawalazimiki kwenda kazini /shuleni.
HIYO NI NADRA KAMA KUTOKEA KWA MAFURIKO MAKUBWA au mpaka TSUNAMI hivyo kuna errors hapa na pale:
Ila kimsingi misingi ya dunia iko hivyo almost balanced kwamba kila mtu ana ratiba zake ila mwisho wa siku mifumo hiyo inajikuta ipo almost balanced. huyu anatoka Posta kwenda Tegeta na mwengine anatoka Tegeta kuelekea Kawe, hivyo hivyo mpaka mfumo mzima unakuwa wote balanced. Mfano wa pili jiulize kama waTanzania wote 60+ million tukiumwa siku moja na kwa wakati mmoja je hospitali zitaweza kutuhudumia? Hapana. Ila inatokea huyu kaumwa leo na yule kaumwa kesho yake ndo hivyo mpaka mzigo wa wagonjwa hospitali unakuwa almost balanced.
Basi ndo hivyo hivyo kwenye mabenki, huyu akija kutoa ile TZS 100,000 mwengine anakuja kuweka TZS 120,000 hivyo hivyo mpaka kiasi cha pesa kilichopo kwenye mabenki kinakuwa almost balanced, na kuna vipimo na sheria zipo kucontrol kiasi gani cha pesa au mali zinazoweza kubadilishwa kuwa posa kirahisi benki iwe nayo wakati wote ili isitokee tukio kama hilo uliloongelea.
2. Katika banking system ni hivyo hivyo.
3. Mara nyingi huwa inabidi ufungue au uwe na account katika bank unayoenda kukopa then wataweka hela humo kwenye account.