Msaada wadau! Mjukuu anagoma kwenda kozi ya unesi na ukunga Dodoma. Anataka kuendelea na kidato cha tano. Nifanyeje?

Huwa wanatoa fursa ya kubadili combination/course kila mwaka asijali kama ana ufaulu unaomruhusu

Njia nyingine ni kwenda kwa Afisa Elimu Mkoa (REO) pia huwa wanahamisha ilimradi uwe na sababu ya msingi.
 
Hawa watoto sijui nani kawaloga eti kwenda form five kwao ndio dili. Nina uncle wangu mwaka jana alipangiwa chuo cha MUST course ya umeme eti akataka kubadilisha kwenda form five kashauriwa na baba yake, mimi nikamwambia wewe jaribu kubadilsha ndio utanijua mimi ni nani. Uncle akanisikiliza akaenda MUST kufika kule nikamuombea abadilishe course asome civil kwa sababu tayari kuna watu wamesoma umeme kwenye familia akapata. Leo hii ananipigia simu anafurahia maisha ya chuo na anatarajia kulamba hela ya IPT muda sio mrefu.

Kifupi watu bado hawaelewi kuhusu hizi elimu za vyuo vya kati wao wanadhani five na six ndio dili, hawajui zama zimebadilika.

Ushauri wangu kwako usikubali mjukuu akupande kichwani, mshauri umuhimu wa kwenda chuo tena uzuri ni chuo cha afya, tumia democrasia kumshauri ikishindikana tumia nguvu tena ikiwezekana mwambie akienda form five hutomlipia ada, atakuja kukushukuru baadae.
 
Nimekuelewa! Zama zimebadilika. Nakaza buti ili tuelewane.
 
Huwa wanatoa fursa ya kubadili combination/course kila mwaka asijali kama ana ufaulu unaomruhusu

Njia nyingine ni kwenda kwa Afisa Elimu Mkoa (REO) pia huwa wanahamisha ilimradi uwe na sababu ya msingi.
Hujamuelewa mtoa mada
 
Mkuu kaa nae kwa utulivu mueleweshe..hapo kwenye Ukunga anaongeza ujuzi kuliko kule kwingine anaongeza vidato tu bila ujuzi..mfafanulie kwa mifano mujarabu.
 
Wajibu wako ni kumshauri tu ila mpe fursa ya kufanya maamuzi yake kwa sababu ana ndoto zake pia, ukimlazimisha kuwa muuguzi/mkunga atakuwa hafurahii taaluma yake baadae.
 
Nadhani kunanhaja ya kumhoji vizuri, pengine ana ndoto ya kuwa daktari na sio tu mkunga, sasa akienda a-level anaweza kuendelea na udktari kulingana na ufaulu.
Pia atakuwa anapata peer-pressure anaona wenzake wanaenda Alevel yeye anaingia chuo.
Muhimu ninkumsikiliza na kumshauri vizuri.
 
Acha mjukuu asome advance level, akimaliza asome degree mazima aje kuwa Nurse officer, au MD, sasa akasome diploma miaka 3, tena akimaliza leseni afanye mitihani ya EN
 
Amechaguliwa kwenda chuo. Anasema hapana. Anatpenda aendelee na kidato cha tano kwa mchepuko wake uleule wa masomo ya sayansi. Wapi nigeukie ili nisaidiwe?
Kuna dhamira ya ndani inamvuta kuendelea na kidato cha tano,... kama anayamudu masomo ya combination aliyopo aendelee na F5 aachane na chuo kwa sasa, ILA ahakikishe kuwa anapata division one kwenye mtihani wa F6.... Inawezekana kabisa!.
 
Back
Top Bottom