Hii inaweza kusaidia kwa kiwango fulani labda ila Sina uhakika.
Tafuta simu nyingine, nenda play store ilipo google account ya hiyo simu, utaona Kuna option ya kuadd account nyingine, ingia hapo add hiyo google account yako kama account mbadala ya kutumika kwenye hiyo simu.
Kwa kufanya hivyo hiyo simu itakuwa na access moja kwa moja kwenye gmail Yako, google photos n.k.
Ingia kwenye app ya Gmail kutakuwa na options ya kutumia account ya mwanzo iliyokuwepo kwenye simu au hiyo uliyoadd, wewe chagua uliyoadd hapo utaweza kuadd recovery phone, utaweza kuchange baadhi ya settings, pia utaweza kuadd recovery email.
Au
Hukohuko play store baada ya kuadd account Yako na kuichagua kama account inayotumika kwenye simu kwa muda huo, nenda sehemu imeandikwa manage your Google account, kisha nenda sehemu imeandikwa Personal Info huko unaweza kubadili baadhi ya taarifa kwenye account Yako.
Ukishabadili settings karudie zoezi la kulogin kwenye simu yenye changamoto. Kumbuka hili zoezi linafanyika kwenye simu nyingine tofauti na hiyo yenye changamoto.
Ukijaribu kulogin kawaida kwenye browser lazima itakuomba kuverify. Jaribu hiyo kama itakusaidia, au nenda google utapata mbinu mbalimbali