Mimi sio fundi Ila wakati najenga fundi wangu alinielewesha kidogo.
Iko hivi:-
Tukianza na generation za hizo sckimming material ilianza
Gypsum Powder
White Cement
Wall putty
Mafundi wengi hawako sana familia na wall putty hivyo kama ujuavyo mtu hupendelea kile akijuacho.
Faida kubwa ya wall putty ina antifungal ndani yake kudhibiti fungus za ukutani lakini pia unaweka hiyo BINDER kuifanya rangi yako isibanduke hasa maeneo yenye unyevu.
Hivyo basi ushauri ambao alinipa nitumie white cement ndani sababu kutakuwa na unyevu kidogo au usiwepo kabisa na kwa sababu white cement inacover square mita nyingi kulinganisha na wall putty.
Nje alinishauri nitumie wall putty ili kuhimili unyevu wa nje na fungus za ukutani. Kwa hiyo kwa generation wall putty ni toleo za kisasa zaidi tukiamini zitakuwa zimecover changamoto za matoleo ya nyuma.
Uamuzi ni wako kulingana na eneo lako na hali ya mfuko wako. Hongera kwa hatua ya finishing nikikumbuka ilivyonipelekesha sina hamu nayo.