Sasa si uende huko CCM wakupe nyumba, hiyo nyumba wewe haikuhusu. Nyumba ni yaya baba yako anayo haki ya kukutimua kwa huo umbavu wako.Marehemu babu yangu kabla ya kufariki alisema kabisa na wazi kuwa nisinyanyasike kwenye ule mji.
[emoji23][emoji23][emoji23]miaka 28 mpaka leo uko kwa baba ako, baba ako nae sijui ana miaka mingapi ila na yeye anakaa kwa baba ake. ngoja waje.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]dume kulilia nyumba ya "urisi"!..hhhaaa "anakela xana"
[emoji23][emoji23][emoji23]umefikiria ka mm,alitazamia watu wamjaze upepo hapa akaweke ding ndan kisa cha nyumba ya babu yake
naona baba yako amepata mpangaji ambae hanyi hivyo choo hakita jaaHapana mkuu hapo nyumbani kuna chumba ambacho mzee amekifunga na kufuli na kunitolea vitu nje, ananitukana eti bora apangishe hapate kodi kuliko mimi kukaa na kujaza choo
Babu amempa chumba na kumwambia asinyanyasike nae akapata kiburi,ni bora umwambie baba yako akupe nyumba yako ya urithi kisha wewe nawe umpangisheDuu yaani baba yako anaishi kwao na wewe unaishi kwa babu yako.
We dada hujui kuna mapinduzi ya uandishi siku hizi?
Kwa hiyo ulitaka mdingi akenue meno kwa kufanywa msukule wa CCM?halafu uliwahi ona wapi ccm ikamjali mtu waliemtumia?Maisha haya magumu. Unaanzaje kuchagua kazi? Hata kama unaichukua CCM siyo suala la kugombezana na mtoto kisa kujiingiza kwenye CCM. Watu siku hizi wanatafuta pesa na siyo chama. Popote pale kwenye pesa watu wataenda kufanya kazi. Huyo dingi hajatumia busara kabisa
Mkuu bora usepeHabarini ndugu zangu wana JamiiForums, matumaini yangu mu wazima wa afya tele.
Nisiwachoshe niende kwenye mada moja kwa moja
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, nimemaliza chuo kikuu mwaka jana. Tangu nimemaliza chuo, nimehangaika sana kupata kazi bila mafanikio. Mwaka huu mwezi uliopita nilibahatika kupata kazi ya kuandikisha wapiga kura kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
Baba yangu alikataa kabisa nisijihusishe kwenye mambo yoyote yanayohusiana na siasa kwa hiyo hakupendezwa. Baada ya hilo zoezi la uandikishaji kuisha, juzi Ijumaa kuna mjumbe wa chama cha mapinduzi (CCM) aliniambia kuwa nimtafutie wanachama 20 tu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, na kuahidi atanipa pesa ya maji.
Pale home jumla tupo watu 7 pamoja na ndugu wengine, nilitaka kwanza kuanza na familia yangu, nilimfuata baba yangu na kumueleza kuwa na yeye awe mmoja wapo katika watu 20 nilioombwa na mjumbe
Ndugu zangu, baba alinitukana matusi mazito, siwezi kuyaandika hapa, mpaka kufikia kuniambia nitakuwa nimelaaniwa na dunia. Kaenda mbali zaidi ananimbia kama ntashilikiana na watu wa CCM na kumhusisha yeye, ataniondoa kwenye nyumba tunayoishi, ukizingatia hiyo nyumba ni ya babu yangu ambaye yeye ni baba yake.
Marehemu babu yangu kabla ya kufariki alisema kabisa na wazi kuwa nisinyanyasike kwenye ule mji. Wakuu, mpaka ninapoandika hapa, baba atoa vitu vyangu nje, anasema nikahamie kwa huyo mjumbe.
Naombeni ushauri wenu wakuu, nataka kuipigania haki yangu, maana babu alisema kile chumba nilichokuwa nakaa ni mali yangu halali.
Nipo katika wakati mkuu, nisaidieni niende polisi au nifanye nini wakuu?
Asanteni.
ungemwambia tu aende kwenye nyumba ya baba yake ili kuepusha shariKesi ya nyani umeileta kwa mkulima!
Acha nijiandae kusoma komenti watakutia hasira huku hadi ujikute unajuta kuandika uzi wako.