Msaada wenu Wakuu, baba yangu hataki kunilipa deni langu

kikoozi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2015
Posts
2,094
Reaction score
3,108
Habarini za uzima wakuu

Mimi ni kijana nina miaka 31, mwaka huu mwezi wa pili mungu akipenda natimiza 32 (kwa kweli litakuwa jambo la kumshukuru Mungu kwa uhai huo)

Niende kwenye maada moja kwa moja

Kipindi nipo chuo 2013 nilikuwa napata bumu langu vizuri tu, baba yangu aliniomba nimsaidie sh laki 5 kipindi nipo mwaka wa pili nikampa kwa miadi kuwa atanirejeshea pesa yangu.

Mwaka wa tatu semister ya pili mzee akaniomba laki 4 tena uku akiwa bado hajanilipa laki 5 yangu, sikuwa na iyana nikampa

Jumla nikawa namdai SH LAKI 9 (900,000)

Baada ya kumaliza chuo na kurudi home ni mwaka wa 7 sasa baba hataki kunilipa deni langu

Umri wa kuondoka nyumbani umeshakaribia, nimemuomba mzee anipatie iyo pesa yangu nikapange chumba nifungue na biashara ila kila siku anasema hayupo vizuri

Wakuu naombeni ushauri wenu nifanyeje nipate haki yangu

Maana nikimuambia mambo ya siasa anasema kama naipenda CCM niondoke nyumbani kwakwe, wakati huohuo hataki kunipa ela yangu

Kila siku is naumia moyoni

Naombeni msaada wenu

Sent using komputa mpakato
 
Pole sana mkuu, naamini huyo ni baba yako mzazi. Kama hana hela utafahamu na kama anajifanyisha unafahamu. Samehe anza upya 2020. Tafuta hela nyingine nenda kapange. Haina haja ya kuwa na vinyongo/bifu na wazazi wetu, maana bado atabaki kuwa baba yako tu. Fanya kazi kwa bidii uhame na pia usisahau kuwasaidia wazazi wako. Mungu akubariki sana.
 
Natokaje mkuu wakati baba kakaa na ela zangu

Sent using komputa mpakato
Acha ujinga Mkuu... Hizo hela sio zako, huwezi kumdai mzee pesa tena laki 9? And believe me anakuona mjinga sana wewe kuendelea kumdai hiyo hela... Umesoma umefika level ya chuo bado unashindwa kuchanganua suala kama hilo? MZAZI HADAIWI
 
Hapana mkuu yeye mwenyewe alisema atanilipa ila kwa sasa naona dalili zote za kutokulipa naumia sana, naona kama ananizurumu nawaza kwenda mahakamani

Sent using komputa mpakato
Sasa si hana hela angekua nayo si angekulipa unataka akatoe wapi baba yako

Yaani wtu tunawasitiri watu tusiowajua sembuse baba mzazi we jamaa umenishngaza sana

Hebu jipige pige kifua na ujiambie mimi ni mchawi Mungu baba nisaidie
 
Sijafahamu siana unacho kidai au lalamiko lakoni nini. Ila kwamaeezoyako naona mambo mawili.

1: Deni la laki tisa - 900,000/=

2: Mambo ya siasa - Kuipenda ccm.

Ingekuwa vizuri kuwa wazi tatizo lenu liko wapi, kwenye siasa au kulipana pesa.

NB:
Kwa ushauri wangu, jambo la kumda Babako pesa si sahihi, kwani akikudai gharama za kukulea, kukutibu, kukusomesha na hadi leo una umri wa miaka 32 bado tu unakula na kulala kwake, ukimdai utaonekana una adabu wala shukurani kwa wazazi wako.

Wewe kama unataka kutoka kwa wazazi na ukajitegemee, basi chukua hiyo hatua bila kuhusisha mambo ya siasa.

Miaka yote hiyo 32 unakula na kulala kwa wazazi bado unang'ang,ania ulipwe 900,000/= ukaanze maisha, miaka 7 yote baada ya kumaliza chuo ulikuwa unafanya nini hujaanza kujitegemea? Kweli wewe ni mzigo mzito sana kwa wazazi.

Mwisho: wewe ni KE au ME?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…