Msaada wenu Wakuu, baba yangu hataki kunilipa deni langu

Nakushauri achana kumdai Mzazi.Huyo ni Baba yako hujui kama anakupima? Wazee wengi huwapima watoto wao kwa njia nyingi.Kuna kitu anakipima kwako usifikiri hajui kwamba unamdai.Jiongeze na kama una kazi/biashara yako jitahidi uwe unampa hela bila kujali kwamba unamdai.Faida yake utaiona.Huyo ni Mzazi.Mwenye masikio na asikie.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwitie wahuni, wampige, azimie wampore hela wakupe za kwako wabaki na za kwao full stop ,pumbavu mkubwa simbilisi nyambuzi ngengenga ndukulikudusucho mkubwa weee
 
anza kwanza kumlipa kodi ya tumiaka 7 uliyokaa kwake uone kama hujapewa vijisenti vyako
 
Usimpe stress kabisa huyo mzee kisa eti ulimkopesha hyo fedha,tena ilitakiwa akitaka kukupa uikatae kabisa kama ukoma,usimpe mawazo kabisa nasisitiza kwani akifikiria aliyokufanyia utausononesha sana moyo wake na hutapata radhi zake
 

Una matatizo makubwa sana na ukiendelea na huo mtazamo hautafanikiwa, Mwambie Baba yako akuombee Baraka na Ondoka hapo home hata kwa Miguu katafute maisha!

Shenzhen kabisa wewe! Hiyo miaka 7 uliyokaa hapo piga hesabu ya kodi na chakula maana ulishamaliza Shule ulitakiwa uwapishe uende! Ni shilling ngapi?

Huu ujinga wako wa kumdai Mzee ndio ambao unakufanya ukae hapo mpaka Leo bila kazi au mafanikio!
 
Ukiwa hauna pesa unaweza kuona hiyo 900,000 ni kubwa sana so unaweza kuidai kwa nguvu. Ila sasa ukipewa ukaenda kuanza maisha utajikuta hauna kitu. So samehe hiyo pesa. Maana kiutaratibu ulipofikisha miaka 18 tayari ulishakuwa mtu mzima ulitakiwa uishi kwako. Vp mshua akikupigia mahesabu,utatoboa kweli ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo serious kabisa? Daaah nakuonea huruma kwa akili uliyo nayo
 
Huyu jamaa nashindwa kumuelewa kabisa waungwana, sasa na yeye akiamua kukudai gharama zote alizotumia kukukuza mpaka ukafikia umri huo wa kuja kupiga porojo hapa utamudu kumlipa??
 
Sasa si hana hela angekua nayo si angekulipa unataka akatoe wapi baba yako

Yaani wtu tunawasitiri watu tusiowajua sembuse baba mzazi we jamaa umenishngaza sana

Hebu jipige pige kifua na ujiambie mimi ni mchawi
[emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Nadhani ingekuwa busara kwanza wewe ulipe deni ambalo anakudai na kama unaweza kufanya hivyo, ninadhani baada ya malipo hayo naye atakulipa.
 
Ninachokiona we jamaa huna maelewano na baba yako na ndio kinapelekea yote hayo!
Na itakuwa baba yako keshakuchoka umri mkubwa namna hiyo bado uko kwa baba yako na unamdai pesa kidogo kiasi hicho!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wewe hadi kufikia umri huo unaweza kumlipa baba yako hata ⅓ tu ya alivyojitoa dhidi yako? Kwa wazee huwa tunawekeza. Akilipa sawa na asipolipa pia sawa. Na huwa hatudai.

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…