Msaada wenu Wakuu, baba yangu hataki kunilipa deni langu

Thaminisha hiyo fedha kwa miaka uloishi

900,000/32 = 28, 125 TZS kwa mwaka
28,125/12 = 2,344 TZS kwa mwezi
2,344/30 = 78 TZS kwa siku

___linganisha na matunzo yako alogharamikia
Chakula & Mavazi
Uliugua akakupeleka hospital
Ada ya shule alolipa
Ulinzi alokupa hadi sasa umekuwa
Ulivunja/ama kuharibu vitu vyake ama vya wengine/shuleni akalipa

"...Mwanangu waheshimu wazazi wako upate miaka mingi na heri duniani..."
 
  • Kijana kwanza utambue wazi kwamba baba yako alitumia muda mwingi na rasilimali nyingi sana kumpata mama yako,ikiwemokukoswa koswa mishale na wajombazako ambao ni kakawa mama zako.
  • Mbili baba yako ali hustle sana kujiweka sawa kimaisha baada ya kuanza kuishi na mama kabla wewe hujafikiriwa.
  • Ulimtesa sana baba kipindi cha ujauzito wa mama kwa kuwa hakuwa na kazi ya kueleweka na bado alikuwa na madukumu mengine yaliyomtegemea yeye.
  • Ukiwa mdogo umeharibu vitu vingi sana nyumbani ambavyo utahitajika ukurasa mzima wa A3 kuelezea uharibifu huo.
  • Gharama aliyotumia kukulisha,kukuvisha,kukutibu na kukununulia mahitaji ni kubwa mno hasa ukizingatia palikuwa na transition mbaya ya uongozi na anguko la uchumi toka kwa mzee Mwinyi hadi kwa mzee Ben.
  • Umekaa kwa mzee bure kwa miaka yote hiyo hujui bei ya umeme,hujui bei ya mkaa,hujui bill ya maji na bado ameweza kujikunja kukusomesha.
  • Kwa muktadha huo unapaswa wewe ndiye ulipe gharama zooooote alizotumia na kurudisha mali zake zote kisha mkae chini muandikiane mkataba kama ataona inafaa basi uendelee kuwa mwanae ama utafute baba mwingine.
 
Mkuu nilikua pia nampa mzazi boom kipindi nipo chuo kuanzia mwaka wa pili mpaka namaliza wanne ikawa jumla ya 3.6 million

Nikapiga hesabu 3.6 m ni mtaji tosha

Nilivoenda kudai nikapigwa kiswahili kimoja tu roho iliuma maana nlikua namipango nayo niliondoka na home mwwzi huo huo sikuidai tena
Mpaka leo miaka miwili imepita

Mzazi adaiwi hata kama alikukopaa
 
Acha hizo Kama baba yake alitaka ampe hela angemuomba tu Sio kusingizia mkopo.
Halafu mtoto Yuko chuo unamkopa Sio sahihi

Amlipe pesa zake huo Ni uhuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…