Msaada: Wenye ujuzi na uzoefu kuhusu kazi ya uvuvi

Msaada: Wenye ujuzi na uzoefu kuhusu kazi ya uvuvi

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Namaanisha ile kwenda baharini na kuomba kibarua cha kazi ya kuanza kuvua samaki hlf ni mgeni na sina uzoefu wa kuogelea.

Nimeongea na wavuvi wenyeji Wenye mtumbwi wa kawaida tu, wamekubali nijiunge nao, je ni kazi yenye maslahi?

Malipo yake kwa siku ni tshs ngapi? Majukumu yangu yatakuwa yapi kwa hizi siku za mwanzo? Changamoto zake ni zipi?
 
Chief. Huna haja ya Kuwaza hayo yote nenda kafanye kazi.
Na kuhusu ujira utapata kutegemeana na kilichopatikana.
Na inaonyesha we si kijana mgumu ndiyo maana unapata mawazo na hisia mbaya dhidi ya kazi unayotaka kuifanya.
 
Jifunze kwanza kuogelea ndio ufanye uvuvi
Zingatia :kazi ya uvuvi ni high risk ila ni nzuri
 
Namaanisha ile kwenda baharini na kuomba kibarua cha kazi ya kuanza kuvua samaki hlf ni mgeni na sina uzoefu wa kuogelea.

Nimeongea na wavuvi wenyeji Wenye mtumbwi wa kawaida tu, wamekubali nijiunge nao, je ni kazi yenye maslahi?

Malipo yake kwa siku ni tshs ngapi? Majukumu yangu yatakuwa yapi kwa hizi siku za mwanzo? Changamoto zake ni zipi?
Jiweke kiroho vizuri, kwenye maisha ya baharini au ziwani Kuna vitu vya kiroho vizito...
 
Niombee tu, siku nikiwa Afisa Uvuvi, nitakutafutia gap huko kwenye chain.

Ila jua, mvua, baridi, majambazi, mawimbi ya maji, kupiga kasia kwa mitumbwi isiyo na injini vyote vyako.

Kikubwa uwe na nguvu.
 
Nawaonea Ngoa (wivu wa kimaendeleo) sana wavuvi japo ni ngumu kwangu kuifanya hii Kazi
 
Kuna anaejua kwa nini majibu ya msaidizi wa uvuvi yamechelewa kutoka maana ishapita miezi 5
 
Namaanisha ile kwenda baharini na kuomba kibarua cha kazi ya kuanza kuvua samaki hlf ni mgeni na sina uzoefu wa kuogelea.

Nimeongea na wavuvi wenyeji Wenye mtumbwi wa kawaida tu, wamekubali nijiunge nao, je ni kazi yenye maslahi?

Malipo yake kwa siku ni tshs ngapi? Majukumu yangu yatakuwa yapi kwa hizi siku za mwanzo? Changamoto zake ni zipi?
Kwa kweli kazi ya uvuvi inahitaji moyo, kujitoa kweli kweli kwani ni too risk,, kutokana na kazi zake kufanyika majini, japo hakuna kazi isiyo na risk,, kingine Kuna visa vingi vya ajabu hutokea huko majini,, hii husababishwa na UGOMVI miongoni mwa wavuvi wa kundi moja na jingine ama miongoni mwenu wenyewe,,, hivyo ni kujipanga haswa,,, by the way kazi risky zote huwa zina faida,, wavuvi pia wanapata faida kubwa,, japo ndo hivyo wengine wanashindwa kutumia hiyo faida ipasavyo.
Na mwisho angalia ROHO yako inasema nini usiende kisa umesikia au Kuona kuwa wavuvi wanapiga pesa.

"Do what you love mostly and something that you're good at"
 
Kuna anaejua kwa nini majibu ya msaidizi wa uvuvi yamechelewa kutoka maana ishapita miezi 5
Yeye anaulizia wavuvi wa baharini wao hawana smartphone ila angeuliza wale wa kayenze na ukerewe majibu mbona yalikuwepo.
 
Back
Top Bottom