Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mambo yametokea huko, ngoja waseto waje watueleze kunani! Au CCM ndio imepiga pini 'No Reforms No Election' isipate nguvu wakaanza kushawishiwa kupokea mabadiliko?!
=====
Msafara wa viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ukiongozwa na Kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu uliosafiri kuelekea nchini Angola kwa ajili ya kushiriki Mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika umezuiliwa katika uwanja wa ndege wa Luanda (Angola).
Jambo TV ikizungumza na Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa ACT, Dkt. Nasra Nassor ameeleza kuwa viongozi hao akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Lissu wanarudishwa jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini ili waweze kurudi nchini.
Nasra ameeleza kuwa msafara wa Makamu wa Rais utarejeshwa peke yake huku viongozi wengine wakirudishwa peke yao
Aidha Jambo TV imemuuliza kama walipewa sababu ya wao kuzuiliwa ameeleza kuwa mpaka sasa bado hawajaambiwa sababu ni nini ila wameambiwa watarudishwa Afrika ya Kusini.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Jambo TV imejaribu kumuuliza juu ya wao kufanya mawasiliano na ubalozi wa Tanzania nchini humo amesema kuwa wamewasiliana nao lakini ubalozi huo hauna nguvu juu ya maamuzi yaliyofanyika
Jambo TV inaendelea kufuatilia habari hii zaidi na tutaendelea kukujuza.
Msafara wa Viongozi wa ACT Wazalendo ukiongozwa na Kiongozi wa Chama Ndugu Dorothy Semu na Mwenyekiti wa Chama Ndugu Othman Masoud Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar umezuiwa kuingia nchini Angola na mamlaka za Serikali ya Angola.
Viongozi hao wanashikiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Luanda na hati zao za kusafiria zinashikiliwa. Serikali ya Angola, bila kueleza sababu yoyote imetoa amri ya viongozi hao kurejeshwa Tanzania.
Viongozi hao waliwasili Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika [The Platform for African Democrats (PAD)] yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation yaliyopangwa kufanyika kuanzia tarehe 13-16 Machi 2025.
Mbali na viongozi wa ACT Wazalendo, viongozi wengine zaidi ya 40 kutoka nchi mbalimbali Afrika ambao pia walikuwa wanahudhuria mkutano huo wamezuiliwa na Serikali ya Angola. Moja ya viongozi waandamizi waliotarajiwa kushiriki kwenye Mkutano huo ni pamoja na Marais Wastaafu Ian Khama (Botswana) na Andres Pastrana Arango (Columbia). Wengine ni Waziri wa Kilimo wa Afrika ya Kusini na Kiongozi wa Chama cha DA Ndugu John Steenhuisen na Kiongozi wa Chama cha PODEMOS cha nchini MsumbijiNdugu Venancio Mondlane.
WITO WETU
Wakati Kamati ya Uongozi Taifa ikikutana kwa dharura kutafakari juu ya mkasa huu na hatua muafaka za kuchukua, Chama kinatoa wito ufuatao katika hatua za awali;-
ACT Wazalendo inalaani kwa nguvu kitendo cha udhalilishaji kilichofanyika dhidi ya viongozi wetu na viongozi wengine kwa kuzuiliwa na kushikiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Luanda.
Tunamtaka Balozi wa Angola nchini Tanzania kutoa maelezo ni kwa sababu gani viongozi wetu akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar wamezuiliwa na kunyang'anywa hati zao za kusafiriria.
Tunaitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imuite na kumhoji Balozi wa Angola nchini juu ya kadhia hii.
Tunatoa wito kwa Serikali ya Angola kuziachia mara moja hati za kusafiria za viongozi wetu walizozishikilia na kuwaruhusu kuendelea na ratiba yao nchini Angola.
Alichoandika Tundu Lissu
Angolan immigration authorities are holding up and denying entry into Angola for me and a delegation of more than twenty senior leaders and representatives of political parties from across southern Africa who arrived in Luanda earlier today for a planned two day meeting.
The group includes a sitting First Vice President from Tanzania; a former President of Botswana; a former Prime Minister of Lesotho and a host of senior political leaders and delegates from Kenya, Sudan, Tanzania, South Africa, Namibia, Eswatini, Lesotho, Germany, USA, Uganda, DRC and Mozambique.
Angolans and Tanzanians are a brotherly people. Tanzania hosted Dr. Antonio Agostinho Neto and his MPLA fighters in the early years of their independence struggle. We supported Angola through thick and thin during the apartheid South African regime's occupation of Southern Angola in the '70s and '80s.
Like Angola, Tanzania is a SADC member state and, as such, we Tanzanians don't need visa to enter Angola.
This shabby treatment of the nationals of brotherly African nations by the Angolan immigration authorities is totally unacceptable and should be condemned in the strongest possible terms.

=========================
VIONGOZI ACT WAZALENDO WAZUIWA KUINGIA NCHINI ANGOLA