Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Msafara wa Raisi (Presidential Motorcade) kukosea njia! Hii imekaaje kiusalama?

Sokoro waito

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
2,201
Reaction score
2,599
Heko wadau wa ulingo huu usio na mashabiki wengi.

Siku tatu zilizopita nilienda Mwanza kikazi, ndipo leo muda wa saa 4 au saa 5 asubuhi, tarehe 4 mwezi wa 9, 2018 nimeshuhudia kwa macho yangu msafara wa Raisi wa Tanzania ukikosea njia pale Mwanza kwenye Roundabout iliyoko karibu na BOT MWANZA.
1536072079241.jpeg


Pamoja na kuwa walikuwepo askari wa usalama barabarani lakini nimeshangazwa kuona gari za mbele kusimama ghafla baada ya kuwa zimeingia junction ya Musoma road badala ya kunyooka na Airport road. Baada ya kusimama ghafla gari ya mbele ilipiga honi karibia mara nne, ambapo nafikiri ilimaanisha kutaka msaada wa kuelekezwa njia baada ya kukosea njia sahihi.

Ndipo mmoja wa askari kwenye gari la pili akashuka haraka na kumuonyeshea ishara ya kugeuza ili waendelee na Airport road. Wakati hayo yakiendelea ilibidi msafara wa gari za mbele usimame huku gari za nyuma zikipunguza mwendo kwa ghafla.

Baada ya kushuhudia tukio hilo nikabaki najiuliza maswali mengi, hivi kumbe somo la mawasiliano ni shida hata kwa taasisi nyeti ambazo zinaongoza msafara wa Raisi?


Je mawasiliano ya askari wa usalama barabarani yalikuwa hacked na kupoteza umakini wa taarifa na maelekezo?

Lakini pia nikajiuliza hili tukio kiusalama lina madhara gani?

Karibuni wadau.
 
Ni hatari kwa kweli ukiachana na mawasiliano basi hata ramani wameshindwa Kuwa nayo pia hivi Mishangingi kama ile inakosa TV pale mbele inayoonyesha Ramani!!!....
Sisi baaado sana

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
 
Oooh ila hata me nilishawahi kupotea njia kule temeke ila namshukuru Mungu niliuliza nikafika

Sent using Jamii Forums mobile app
sawa mkuu ila wewe haukuwa na muongozaji, kwahiyo ni tofauti na Presidential motorcade, msafara wa Raisi unaongozwa na taasisi nyeti lakini leo umepotea njia kiajabu ajabu.
 
Back
Top Bottom