Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Mbona mimi nilienda tu jana bila itifaki?
Hahah

Viongozi wa nchi walikuwepo? Kama waliwahi kufika kabla mkuu wa nchi ajafika itakuwa wameonewa ila kama wamefika baada ya rais ni sawa tu kuzuiwa.

Kumbuka hao ni watu mashuhuri lazima wakae kule viongozi mashuhuru wanapokaa,wakikaa kwa wananchi wa kawaida kungeleta manunguniko kama wametengwa ila kama tunalichukulia kisiasa sawa.
 
Jana polisi wameawachia mkajinafasi maksema mmeogopwa.
 
Je, walienda kwa dhania ya Kumuaga Rais Mstaafu Hayati Mzee Mkapa au walienda ili Kujitangaza zaidi Kisiasa na Kumuonyesha Mgeni Mwenyeji?
Unaakili sana mzee hao walikuwa na yao sasa imeshindikana kwaa wapuuzi wenzao wataona wameonewa hongera nafikiri kila mtu akiona hapa ataelewa.
 
Wapuuzi Hawa wataendaje na msafara wakati Rais ameshaingia tena anahutubia naona sifa zinawalevya Sasa.
 
Kuna Watu ninawashangaa mno Mkuu kwani wanamjua kabisa Mwamba alivyo na Kisununu na Kisasi na Wao wanaendelea Kumtibua tu kama hivi.
Huyo mwamba wako lazima ajue hii nchi inaendeshwa kwa sheria na taratibu, haiendeshwi kwa kanuni ya kuuangalia uso wa mwamba wako ukoje, hilo mlijue vizuri.
 
Hawa jamaa wanafanya mzaha na msiba wa taifa . Kiki ya jana imebuma wameona waende wakatafute kiki nyingine msibani. Aibu sana kwa CHADEMA.
Jana polisi imecheza nao kwa akili sana!
 
Je, walienda kwa dhania ya Kumuaga Rais Mstaafu Hayati Mzee Mkapa au walienda ili Kujitangaza zaidi Kisiasa na Kumuonyesha Mgeni Mwenyeji?
Ndio maana mgeni mwenyeji alipania sana leo.

Chadema walisahau kuwa wenyeji waendeo misibani uwa hawatoi taarifa, inaonekana interigencia yao haikujiandaa vema.
Hata hivyo haikuwa busara kwenda saa nne wakati tayari wakuu wa nchi walikwisha fika,maana nyepesi ni kuwa hizo ni dharau.
 
Wameonyesha dharau kubwa Sana, na ni utomvu mkubwa wa nidhamu.
 
Unataka sababu gani wakati ushawaita wabaguzi
 
Wasalaam!

Wanajamvi wasalaam!

Ni wazi chama kinacho jinadi kinataka kwenda Ikulu na viongozi wake wanatarajiwa kuonesha uwezo na uelewa wa kile wanachokisema au kukitaka hasa kuhusu nchi, taratibu na protocol za nchi na taratibu kwa kila jambo linalohusisha viongozi wa nchi hasa sherehe za kitaifa na shughuli za kitaifa!

Ni kweli CHADEMA na viongozi wake hawajui kuwa kwenye shughuli za kitaifa kuwa kiutaratibu mtu wa mwisho kuingia kwenye shughuli za kitaifa hasa anapokuwepo Rais ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Hivi kweli CHADEMA hawajui huu utaratibu? Kweli viongozi hawa wa CHADEMA hawajui huu utaratibu?

Nini kimewafanya viongozi wa CHADEMA kutaka kuja baada ya Rais kuanza kutoa hotuba?

CHADEMA wana shida gani? Walitaka kushangiliwa?

Hii ni aibu kwa CHADEMA

Wasalaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…