Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Kuingia wa mwisho mtu kama lissu ni kuvuruga attention ya watu waliotulia maana uwanja ungelipuka, ni kama msiba wa ruge diamond alienda wa mwisho wakamrudisha maana alianza kuchukua attention ya watu, angefika on time kusingekuwa hata na bugdha
Sio Lissu tu, hata nikiingia mimi sasa hivi rais amesimama na nikatakiwa kwenda kukaa jukwaa kuu lazima nivuruge attention za watu.
 
Kwahiyo hakuna MTU yeyote aliyeingia baada ya Rais kuingia hapo uwanjani?

Itoshe kusema tu mwenyekiti wa ccm na watu wake ni waoga tu.
#2020
#RIPMzeeMkapa
Chadema ni taasisi inayopambana kuchukua Dola.

Sasa kama hawafahamu taratibu za kidola, ni nani atawapatia Dola?

Tatizo lipo tena kubwa ndani ya Chadema, kimsingi wajirekebishe ikiwezekana watuombe radhi watanzania kwa utovu wa nidhamu waliouonesha leo.

Mtu mwingine anaweza kusema walikwenda ili kuvuruga shughuli kuu ya leo na sio kwa bahati mbaya bali walifanya kusudi ili mradi tu attention kubwa iwe kwa mgeni mwenyeji.
 
Nafikiri kwenye hili tuache ushabiki Viongozi wa Chadema wamechelewa kufika uwanjani na walipaswa kukaa presidential Area wangekaaje na je uwanjani wangeingia vp wakati Rais kaishaingia?

Wakubwa sehemu yeyote ambayo kama kuna event mtu wa mwisho kuingia ni Rais ukichelewa kaa mbali tu!
Hivi tangu lini CCM mnaithamini CHADEMA kiasi hicho cha kuwaweka jukwaa la heshima?

Hivi ni CHADEMA hii hii ambayo Lissu alishambuliwa kwa risasi? Mbowe, Lema, Msigwa, Mdee, Bulaya na Sugu wamelazwa ndani gerezani?

Ni lini ushetani umewatoka mkawa malaika?
 
Hakuna cha kushangaza-uwepo wa Lissu ungeweza kuibua hamasa na shauku tofauti na kile kinacho endelea pale. Umpende Lissu usimpende, watu wangekua na shauku ya kumuona huyo mtu ambae risasi 16 haziku mmaliza-huu nu muujiza. Watu wa protokali wangelimaliza hili na CDM jana, sasa wamelikoroga.
Kwahiyo amezuiwa sababu hii,au utaratibu alitakiwa kuwahi kabla![emoji16][emoji16][emoji16].

Nyinyi watu mna tabu sana.
 
Protocol ni muhimu. Siku zote Mh. Rais akishaingia kwenye event yoyote ya kitaifa geti hufungwa na hairuhusiwi mtu yoyote ama panya kupita.

Chadema mjifunze kuwa na nidhamu, kwa hili mlilolionesha leo mmejipunguzia wapiga kura wa kutosha.
 
Kuingia wa mwisho mtu kama lissu ni kuvuruga attention ya watu waliotulia maana uwanja ungelipuka ,ni kama msiba wa ruge diamond alienda wa mwisho wakamrudisha maana alianza kuchukua attention ya watu ,angefika on time kusingekuwa hata na bugdha
Bila shaka mambo mengi yangesimama kwa muda kupisha attention ya Lissu kitu ambacho kingeleta aibu kubwa Sana.
 
Hivi tangu lini CCM mnaithamini CHADEMA kiasi hicho cha kuwaweka jukwaa la heshima?

Hivi ni CHADEMA hii hii ambayo Lissu alishambuliwa kwa risasi? Mbowe, Lema, Msigwa, Mdee, Bulaya na Sugu wamelazwa ndani gerezani?

Ni lini ushetani umewatoka mkawa malaika?
Labda kama ulimaanisha meza kuu,jukwaa kuu ni huku wanapokaa public figure wote,au kivulini.

Ndio hukaa huko siku zote.
 
Wanajua sana, wanacheza games kama mademu, kesho utasikia nyumba ya Tundu Lisu imevamiwa na kuilaumu Serikali, hao ni watoto wanatafuta attention kwa kila hali.
 
Wamekosea kuchelewa ila hata kama wangewahi kwa figisu za CCM wanaweza kuambiwa mmewahi hamwingii
Hivi tangu lini CCM mnaithamini CHADEMA kiasi hicho cha kuwaweka jukwaa la heshima?

Hivi ni CHADEMA hii hii ambayo Lissu alishambuliwa kwa risasi? Mbowe, Lema, Msigwa, Mdee, Bulaya na Sugu wamelazwa ndani gerezani?

Ni lini ushetani umewatoka mkawa malaika?
 
[emoji16][emoji16][emoji16]yaani hapa ndio huwa siwaelewi watz wenzangu kuwatetea hawa jamaa.

Hawa ni wahuni tu kama manzese,tofauti yao wao ni maarufu na wanavaa suti safi.

Toka jana msemaji wa serikali ametangaza,kwa utaratibu wa viongozi wa uma,wanasiasa na wageni wa alikwa kwenda taifa kuaga mpendwa wetu,wataacha magari karimjee hall na kupanda gari maalum zilizoandaliwa kwenda huko.na muda ni kuanzia saa moja na nusu asubuhi.

Watu wanaingia uwanjani saa tatu na msafara wao binafsi,kama si kutafuta kick za kipuuzi ni nini??
Mmesha wazuia kumuaga Rais wenu wa CCM sasa maneno mengi ya nini tena? Mmetaifisha Mali nyingi za taifa hili na kuzifanya za ccm, sasa mnabinafsisha hata msiba wa taifa kuwa wa CCM?
Hakika ukizoea kuwa mwizi utaiba hata maiti, CCM kweli ni wezi wabobezi
 
Kundi Kubwa la Wahuni limejikuta katika wakati mgumu mara baada ya Kuzuiliwa kuingia katika Uwanjwa wa Uhuru Kumuaga Rais Mkapa.

Nilishatoa Uzi kuwa Tanzania si sehemu ya Kufanya Vitendo vya Kihuni ikiwemo kusubiri Rais Magufuli aingie halafu na wewe ndo Uingie Kutafuta Attention na Kuharibu msiba wa Taifa.

Navipongeza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Kudhibiti wahuni.
 
Tena wangekuwa wanatamka neno hilo kwa mzuka na hamasa kubwa. Nina hakika isingekuwa msiba tena, bali ingekuwa tambo za kisiasa za cdm na ccm. Kama kweli viongozi wa Cdm walitaka kwenda msibani, walipaswa kuchukua utaratibu toka jana, kisha wajipange kuendana na utaratibu uliopo. Japo kwangu busara kubwa ilikuwa ni kutokwenda, hasa hasa Lisu.
Unajuaje kama hawakuchukua utaratibu? Unajuaje labda walichukua Ila ndio wamegeukwa?
 
Back
Top Bottom