Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Je, walienda kwa dhania ya Kumuaga Rais Mstaafu Hayati Mzee Mkapa au walienda ili Kujitangaza zaidi Kisiasa na Kumuonyesha Mgeni Mwenyeji?
Sikutarajia swali la kijuha na kipopoma toka kwako.Kujitangaza walisubiri mkapa afe yaani watu wanaelekea kwenye real event wew unadhani.Its too mystereous and naive
 
Mkapa angelikuwa bado yu hai ninge Unga mkono hoja yako Lakin ameshakata kamba utamshangaa mwenyekiti atakavyo wapenda na kutaka nao maridhiano. Mwenyekiti atotaka tena makundi mwenyekiti atakopi life style ya kikwete
 
Jana msemaji wa serikali alitoa utaratibu wa viongozi kwenda Uwanja wa Taifa, wote walitakiwa kuanzia Karimjee. Sasa sijui viongozi wa CHADEMA kama habari walipata au waliamua kupuuzia
 
Msafara wa Viongozi Wakuu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, wamezuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru walikokuwa wameenda kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa.

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Mbowe aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mhe. Hashim Juma Issa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Mhe. Suzan Kiwanga na viongozi wengine waandamizi kutoka Makao Makuu ya CHADEMA, Viongozi wa Kanda 10 za chama, Viongozi CHADEMAwa Mikoa, Wilaya na Majimbo mbalimbali nchi nzima.
View attachment 1519379
Kutoka Uwanja wa Uhuru hapa, Dar es Salaam.
musitafute huruma ya vyombo vya habari jana utaratibu uliotolewa ni kwamba viongozi wa chama na serikali watapanda magari maalumu,iweje nyie muje kwa usafiri wenu alafu mnakuja muda munaotaka.
 
Nilitazamia kama chama kikomavu cha upinzani nchi ningewaona wakijumuika na watanzania wengi leo pale uwanja wa uhuru kuuga mwili wa Raisi mstaafu lakini si kiongozi mkuu wa chama hicho wala wawakilishi ambao wameweza kujitokeza.

Jambo hili linaleta picha gani katika siasa za nchi yetu. ?

Pamoja na chama pia ambaye hajaonekana ni mwanansiasa mkongwe na mwana depomasia na mwananchama mpya wa ACT wazelendo ndugu Bernard Membe ,Mwingine ni Kiongozi wa chama cha ACT ndugu Zitto Zuberi Kabwe.
 
Yani wewe bado una chuki za dr mihogo? Wtf? Move on wacha gubu! We si “me”?
Kuwa kiongozi mkubwa ni pamoja na kuwa na nidhamu , kwa hili Chadema wamekosa nidhamu..Nia yao wakazue taharuki tu kwenye msiba mbele ya Rais na wageni wake.

Acheni kiki zenu za kitoto, pangeni mipango ya maana kuelekea Uchaguzi mkuu sio sifa za Kijinga.
 
Sikutarajia swali la kijuha na kipopoma toka kwako.Kujitangaza walisubiri mkapa afe yaani watu wanaelekea kwenye real event wew unadhani.Its too mystereous and naive
Wewe na hao viongozi wako ndio Humuwezi kwenda na wakati kabisa
 
Civilisation imewapitia mbali sana MATAGA!

Usishangae wakaambiwa wameandamana bila Kibali.

Ubaguzi huu sasa unahamia mpaka kwenye misiba na ipo siku utakwenda zaidi ya hapo.

Ya jana yamewaumiza, na hizi ndio hasira zao.

Hatari ya uamuzi huu ni msiba kuchukua sura ya kisiasa na matokeo yake watu wanaweza kususa kushiriki ikiwamo kuondoka msibani kwa waliokwisha kufika.

Ila kama kuna sababu ya msingi ya kuwazuia,tuambiwe.
Wameshakamilisha sherehe za mapokezi yaLisu
 
Nawasubiri nao waje na upende wao kabla sijawahukumu. Kuna wakati kuna mengi yaliyo jificha? Kipi kimewasibu? Siamini kuwa hawajui protokali.
 
Back
Top Bottom