Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Hekima na busara muhimu sana, tuache kupenda kuminyana kwa kila jambo mengine hebu tuwe wastaarabu..

Jana kuna upande ulitumia hekima na busara mambo yakaisha salama, leo pia kuna mahala CDM mlipashwa kutumia hekima na busara na nyie kuliko kuminyana.

Kuna vitu vidogo sana vinafanya uonekana hauko smart na jamii ikakupuuza hata kwa yale ya maana, CDM jaribuni kuwa smart kidogo kuliko kutoa point za bure bure kwa adui yenu..
 
Viongozi wa kitaifa wakishaingia huruhusiwa kuingia hivyo hata Hilo dogo tu hawalijui Chadema ? Viongozi wore wa vyama vyao siasa na serikali waliingia saa moja asubuhi wao kweli wanaenda Raisi keshaingia halafu wanataka msafara waonuingie .!!! Ni Watu wa ajabu Sana hata protocol Ndogo tu hizi hawajui

Wenzao akina Seif Shariff Hamad saa. Moja asubuhi walikuwa wameshakaa jukwaani

Wanatafuta air time tu waandikwe ila walichofanya Cha kijinga hawako serious kwenye mambo serious
 
Ukichukua Sefu na Chadema, Sefu anamadhara makubwa kwa CCM kuliko Chadema.

Ni kwenye ushindi wa Sefu mwaka 2000 zaidi ya Wazanzibar 40 walifariki na wengine mpaka leo wako ukimbizini.

Ni kwenye ushindi wa Sefu serikali ya CCM ilisalimu amri Hadi kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Ni kwenye ushindi wa Sefu serikali ya CCM ilifuta matokeo ya Uchaguzi kupitia Mwenyekiti wa ZEC wakati huo Jecha....

Nyie Chadema mmewahi kufanya tukio gani la Kitaifa hadi serikali ya CCM ikasalimu amri.
Watakwambia mafuriko ya lowasa ya 2015 na yale ya jana ya Lisu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ngoja nisubiri kwenye kampeini kama kuna mtu ataingia uwanjani au sehemu yoyote wakati Rais atakua tayari yupo anaomba kura
 
Viongozi wakuu wa Chadema wamefika uwanja wa Uhuru leo saa moja asubuhi ndipo wakazuiwa kuingia wakiambiwa wasubiri kwanza utaratibu.

Ilipofika saa tatu asubuhi viongozi kadhaa walianza kumiminika na kuruhusiwa kuingia uwanjani huku viongozi wa Chadema wakiwa bado getini.

Rais alipofika akaingia ndipo viongozi wa Chadema wakaambiwa hakuna tena kuingia uwanjani.

Ndipo nasema sasa kila mtu afanye shughuli yake ili mradi hatutavunja katiba.
 
Civilisation ni somo llilowashinda MATAGA, kibaya sasa mpaka kwenye misiba.

Pia kuna mtu kwa sasa ni vigumu kukaa karibu na eneo/mahali alipo Lissu.

Kila akimuona Lissu nafsi inamsuta, kwahiyo kukaa katika mazingira ya pamoja na Lissu, kwake ni mtihani mkubwa.
 
Civilisation imewapitia mbali sana MATAGA!

Civilisation ingeoneshwa jana.
√ Wakati nchi jirani wamepeperusha bendera zao za Taifa nusu mlingoti, CHADEMA walizipeperusha kwa bwembwe kumlaki Makamu wa M/Kiti wao;
√ Badala ya mtia nia ya Urais kwenda kutoa rambirambi kwa familia ya mfiwa, aliona ni bora ahutubie waliomlaki tena kwa lugha ya kejeli dhidi ya Serikali na marehemu (akilenga jumuia ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vilivyokaribishwa kwa makusudi hayo);

Au mnaamini WaTz ni wajinga kama walivyoonesha wanachama na wafuasi wa CHADEMA jana, wakati kwa mila na desturi za kiafrika, msiba hupewa uzito mkubwa kijamii na kisiasa.

CHADEMA kitavuna kilichopanda jana.
 
Drama drama drama kama watoto, nafikiri Viongozi (wengi) wa chadema wana arrested development, ...
 
Kunakitu kinaitwa Malicious Intent kwa kikwetu. Viongozi wa CHADEMA hawakwenda pale uwanjani kwa ajili ya kuomboleza bali kwa ajili ya kudhalilisha viongozi na Nchi. Kikubwa ilikuwa ni kutafuta mileage za kisiasa. Sasa katika hali hiyo ni lazima wangefanya kitu chochote tu ili waonekane wapo. Walikuwa na nia ovu. Nani wa kuruhusu upumbavu huo katika hali kama hii ya majonzi tuliyonayo kama Taifa?
 
Viongozi wakuu wa Chadema wamefika uwanja wa Uhuru leo saa moja asubuhi ndipo wakazuiwa kuingia wakiambiwa wasubiri kwanza utaratibu.

Ilipofika saa tatu asubuhi viongozi kadhaa walianza kumiminika na kuruhusiwa kuingia uwanjani huku viongozi wa Chadema wakiwa bado getini.

Rais alipofika akaingia ndipo viongozi wa Chadema wakaambiwa hakuna tena kuingia uwanjani.

Ndipo nasema sasa kila mtu afanye shughuli yake ili mradi hatutavunja katiba.
Duuuh kama ndivyo walivyofanyiwa basi inatia shaka ueledi wa hao waliowazuia.
 
Kunakitu kinaitwa Malicious Intent kwa kikwetu. Viongozi wa CHADEMA hawakwenda pale uwanjani kwa ajiliya kuomboleza bali kwa ajili ya kudhalilisha viongozi na Nchi. Kikubwa ilikuwa ni kutafuta mileage za kisiasa. Sasa katika hali hiyo ni lazima wangefanya kitu chochote tu ili waonekane wapo. Walikuwa na nia ovu. Nani wa kuruhusu upumbavu huo katjka hali kama hii ya majonzi tuliyonayo?
Walikua wanaenda kuwadhalilishaje mkuu?
 
Kunakitu kinaitwa Malicious Intent kwa kikwetu. Viongozi wa CHADEMA hawakwenda pale uwanjani kwa ajiliya kuomboleza bali kwa ajili ya kudhalilisha viongozi na Nchi. Kikubwa ilikuwa ni kutafuta mileage za kisiasa. Sasa katika hali hiyo ni lazima wangefanya kitu chochote tu ili waonekane wapo. Walikuwa na nia ovu. Nani wa kuruhusu upumbavu huo katjka hali kama hii ya majonzi tuliyonayo?
Ni kutokana na Magufuli kuona aibu kuhusu Lissu na itamtafuna sana hiyo hali!
 
Back
Top Bottom