Ubarikiwe sana ndugu.nikikuta kuna mwanaume na mwanamke wanauza bidhaa za aina moja, naendaga kununua kwa mwanaume mwenzangu.
Binafsi mimi hata vile vitoto vya mitaani ambavyo vinaranda randa stendi vikiomba omba hela kwa wapita njia mara nyingi kama nina coins huwa nazigawa kwa vitoto vya kiume na sio vya kike.... maana ninaamini kabisa wale wa kike muda wowote wanapata msaada na kuwaacha hawa wa kiume wakiendelea kuranda randa hapo stend... na of course ni ukweli uliowazi watoto wengi wa mitaani ni wa kiume.
Ukija kwenye biashara ndio usiseme sikumbuki ni lini mara ya mwisho nimenunua bidhaa kwenye duka ambalo najua fika linamilikiwa na mwanamke au muuzaji wake ni mwanamke.....!!
Mimi nikienda kununua bidhaa sehemu yoyote ile yenye wauzaji wengi wake kwa waume, siwezi nikaacha kununua kwa wanaume wenzangu eti nijipeleke kwa wanawake, maana naamini mwanaume mwenzangu asipouza kuna uwezekano mkubwa sana yeye na familia yake wakalala na njaa siku hiyo, tofauti kabisa na mwanamke ambaye unakuta mbali na hiyo biashara ana danga lake linalomuweka mjini au kama ni mke wa mtu basi ndani ya nyumba matumizi yote anayegharamika ni mume na hivyo basi hata asipouza siku hiyo hakuna kitakachomuharibikia.
Let's get back our lost brotherhood strongly.