Msajili asaidiwe asiinajisi Ofisi ya Umma. CCM + TLP, CHADEMA + ACT hawajavunja Sheria

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Labda huyu msajili atuambie Chama cha TLP kinachomnadi Mgombea wa CCM ndugu Magufuli sio chama cha Siasa.

Kwa tafsiri ndogo ya kifungu cha 11A cha sheria ya vyama vya siasa Sura 258 iliyonukuliwa na msajiri hapo, ni kwamba sheria inahusu KUUNGANA KWA VYAMA yaani kwa kizungu wanaita merging/mergermation au Coalition

Sio hii inayotumika na Chadema na ACT wala inayotumika na CCM na TLP ambayo sio muungano bali ni gentlemen agreement au Cooperation. Au kwa siasa za Marekani huitwa endorsement.

Chadema na ACT walijua tangu mwanzo kwamba ccm na msajiri wametegesha zengwe hili ili kusiwepo na muungano kama ule wa UKAWA ndiomaana utaratibu huu wa KUUNGA MKONO mgombea mmoja wapo wa wagombea ulichelewa.

Kwa lugha rahisi ya kitaalamu, hakuna muungano wowote uliopo kati ya Chadema na ACT wala hakuna muungano wowote uliopo kati ya CCM na TLP. Kilichoko kitaalamu huwa kinaitwa kuunga "mkono mgombea flani" ama huitwa endorsement kwa siasa za kimagharibi hasa za USA na UK, Cooperation ama kijeshi hasa kijasusi huitwa gentleman's Agreement. Tena kwenye ujasusi hutumika pale mnapogongana kwenye anga la espionage.

Msajiri wa vyama vya siasa ijapokuwa ni jaji na muhudumu wa sheria, katika hili anahitaji msaada zaidi kuitafsiri sheria hii na kutafsiri matukio ya kisiasa kuliko kukariri na kuendesha ofisi kilumumbalumumba tu.


Na Yericko Nyerere

Pia soma > Uchaguzi 2020 - Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa: Vyama vya Siasa vinavyotaka kushirikiana Uchaguzi Mkuu vimeshachelewa kwa mujibu wa Sheria

 
TLP walisema mapema kabla ya muda kuisha wa kuungana, meaning sheria ya NEC imetoa muda wa vyama kuungana, ukipita hakuna ruhusa kuungana, ACT & CHADEMA chunguzeni hiyo sheria mpya, kwa makini, la sivyo mtaingia ktk mgogoro mkubwa na NEC..

Ilitakiwa ACT na CHADEMA waungane mapema na wapeleke mgombea mmoja wa Rais pale NEC, nadhani wamechelewa, ingetakiwa miezi 3 kabla ya uchaguzi

Uchaguzi 2020 - Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa: Vyama vya Siasa vinavyotaka kushirikiana Uchaguzi Mkuu vimeshachelewa kwa mujibu wa Sheria
 
Umenena vizuri sana!

Wanatakiwa wakumbushwe sheria inasemaje kuhusu kuungana kwa vyama wakati wa uchaguzi. Sio,kwamba hawajui ni ukaidi tu wa sheria ili NEC ionekana inakipendelea chama Cha Mapinduzi.

Ukweli ni kwamba kuungana kuwa na mgombea mmoja wamechelewa na wanatakiwa watafakari upya kile wanachokitaka kukifanya.
 
Kama hauelewi anachokisema Zitto wewe ni mjinga (mtu asiyeelewa jambo fulani lakini akieleweshwa huelewa). Zitto anaongelea ushirikiano wa vyama, siyo kuunganishwa vyama. Wagombea wote wataendelea kuwepo kwenye karatasi ya kupiga kura.

Hakuna sheria inayokataza vyama kushirikiana. Acheni ku-panic. Mmjenga mabarabara, mmennunua mandege makubwa makubwa, ushirikiano wa ACT na CHADEMA ambao hata baiskeli hawajanunua, unawanyimaje usingizi?
Alafu unasikia, once you quote my post, any, kuwa na nidhamu, otherwise utakuwa nyamafu sasa hivi, hooligan..!!

Uchaguzi 2020 - Zitto Kabwe: Oktoba 3 tutatangaza mgombea wa Urais atakayewakilisha upinzani
 
Umelifafanua vema. Delete ccm oct 28
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…