Msajili Hazina: Watumishi wa Umma wako busy kuomba uhamisho kwenda TRA, EWURA, TANESCO na TPA kufuata maslah makubwa

Msajili Hazina: Watumishi wa Umma wako busy kuomba uhamisho kwenda TRA, EWURA, TANESCO na TPA kufuata maslah makubwa

Thubutu! Kuna taasisi ukiweka mishahara midogo (ya kawaida) utakuwa umepalilia rushwa na wizi utakaopelekea uchumi ku collapse. Mfano afisa wa TRA anayeenda kumkadiria mfanyabishara kodi ya mamilioni au bilioni umlipe milioni moja au mshahara sawa na mwalimu au afisa maendeleo au bwana kilimo!
Hao TRA ndio wanaongoza kwa Rushwa sasa kama hujui. Swala la uaminifu kazini halihusiani kabisa na maslahi. Ni lifestyle tu ya watumishi ndio inayochochea rushwa. Huwezi ona boss wako anapiga hela na anaishi maisha ya anasa na wewe usitamani ndio maana hadi maofisa wanakuwa wahuni wahuni.
 
Usiwe na shaka, siku za usoni shule nazo itabidi zijitegemee kama taasisi nyingine yoyote ya Kiserikali.

Wameanza na mashirika ya umma na ya kiserikali, na taasisi zake zote.

Wanakuja kuondoa ujinga wa kupeleka pesa taasisi zote za kidini.

Wakimaliza hapo mashule lazima yajitegemee.
Shule unazozijua wewe Mzee mwezangu zilikuwa za katoliki,Pugu,Minaki,Tosamaganga,Tabora boys ,Girls ,Kibaha sekondary na

Vyuo vya ualimu vyote Tanzania waliviomba toka kwa kanisa na hawajavirudisha ,Chuo cha chang'ombe sasa DUCE ,Msasani na Mpuguso Mbeya,Matogoro Songea Ruvuma

Serikali ilipoamua kuzipora waliweka makubaliano baadhi ya taasisi hawakuzipora na waliahidi watazirudisha baadae

Mpaka sasa shule zote hawajazirudisha kwa kanisa mpaka vyuo vya ualimu

Serikali walipora mpaka hospital baadae zikawa zinafanya vibaya ndio ikaja makubaliano ya kuziendesha

Hospital kubwa kama Ndanda lindi,Peramiho Songea zote serikali iliingilia zikataka kufa ndio wanashirikiana kuziendesha

Serikali wakitaka si wazirudishe ,Kila siku kanisa linataka shule zake na hospital zake

Kanisa linaidai serikali Pugu sekondari kila siku ,Serikali hawataki kuirudisha kwa walioijenga shule wakatoliki

Pugu pale ni eneo la hija la wakatoliki Dar es Salaam na ile shule ni yao

Jumapili kibao michango inatolewa kukarabati eneo la Pugu na ni DSM yote michango inachangwa

Serikali wawarudishie wakatoliki shule zao na hospital zao kwanini bado wanazitumia wakati wana shule zao za kata?

Cha kushangaza wamezikarabati zote na wanaziita shule za vipaji maalum
 
Hebu saidia ni namna gani scale zifanane across.
Maana baada ya mkapa kutofautisha serikali na taasisi za kiserikali na kuzipa uhuru wa kujilipa kulingana na wanachokizalisha kila taasisi ilijiwekea scale yake. Scale nyingine zina maslahi makubwa sana.
Ili ku cut across kwa scale lazma ufanye harmonization across, hii maanake ni kuwa kila mtumishi wa umma apate maslahi yale yaliyo juu kabisa ktk scale ambayo ndo best ktk taasisi kwa kuwa huwezi kushusha mshahara wa mtu.
Hii maanake ni kuwa bajeti yote ya serikali ita service mshahara pekee na pengine isitoshe
duh ko wewe unakula vinavyotoka wapi? acheni kusemea mali za wenzenu eti kisa waisilamu tafuta na wewe zako ndo ututambishie hiyo hoja yako ni ya kitoto kabisa.
 
Thubutu! Kuna taasisi ukiweka mishahara midogo (ya kawaida) utakuwa umepalilia rushwa na wizi utakaopelekea uchumi ku collapse. Mfano afisa wa TRA anayeenda kumkadiria mfanyabishara kodi ya mamilioni au bilioni umlipe milioni moja au mshahara sawa na mwalimu au afisa maendeleo au bwana kilimo!
Mbona hao hao maafisa TRA unaodai wanalipwa hela nyingi, baadhi yao wanakula rushwa? Mishahara huwa haitoshi.
 
Fanyeni harmonization ya mishahara.

Suluhisho pekee
 
hata ajira ya afya nayo ni ujamaa kupata kazi labda uwe mchagga
 
Waongeze wenye mishahara midogo ilingane
Sasa mkuu hao wafanyakazi wa Tamisemi ni wengi mno, wakiongeza mishahara hadi ifikie 1.8mil ilingane na ya taasisi si taifa litafilisika.
 
Sasa mkuu hao wafanyakazi wa Tamisemi ni wengi mno, wakiongeza mishahara hadi ifikie 1.8mil ilingane na ya taasisi si taifa litafilisika.
Basi kwanini mishahara yote ya umma isilingane tu. Kama ndio suluhisho.
 
Halafu wakifika kwenye hizo taasisi hawawezi kazi.

Wamezoea kuingia na kutoka na sherehe sherehe huko walikotoka kuoiga mzigo hawawezi.

Yaani unaambiwa hadi aibu kwamba wamefikajefikaje?

Ni afadhali kila taasisi iajiri yenyewe kuliko kupelekewa watumishi mizigo.
Kwahiyo watu walio taasisi Wana akili kinoma yaani🙉🙉
 
Usiwe na shaka, siku za usoni shule nazo itabidi zijitegemee kama taasisi nyingine yoyote ya Kiserikali.

Wameanza na mashirika ya umma na ya kiserikali, na taasisi zake zote.

Wanakuja kuondoa ujinga wa kupeleka pesa taasisi zote za kidini.

Wakimaliza hapo mashule lazima yajitegemee.
Nchi haina mwelekeo.

Haya matumaini kalale nayo
 
Wewe unao mwelekeo?
👇👇

1697189897400.png
 
Back
Top Bottom