Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Salaam Wakuu,
Msajili Mstaafu wa Vyama va Siasa Jaji Mstaafu John Tendwa, amesema Katiba Mpya itaondoa Migogoro wakati Uchaguzi. ameyasema hayo leo 13 Feb 2021 Jijini dar Wakati wa kujadili Utatuzi wa Migogoro ya Uchaguzi Tanzania, katika Kongomano lililoandaliwa na Tanganyika law society (TLS) ambao umewahusisha Wanahabari na Asasi za kiraia.
Jaji Tendwa amesema vyombo vya habari na Asasi za kiraia wana nafasi kubwa ya kusuruhisha migogoro au kuwa chanzo cha Migogoro.
Jaji ametaja migogoro ambayo ilitokea kwenye Uchaguzi 2015 na 2020 kama ifuatavyo;
i). Kitendo cha Polisi kukamata Mtandao wa Asasi za Kiraia za Kuangalia chaguzi nchini kisa kukusanya taarifa juu ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2015 kama unavyokuwa u aendelea nchi nzima katia kituo cha kukusanya taarifa kilichokuwa katika ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ofisi ya Mbezi Beach. Ni moja ya tukio lililoleta Mgogoro baina ya Asasi za kiraia na Serikali sababu wale walikuwa hawatangazi matokeo bali walikuwa wanafuatia mchakato mzima wa Uchaguzi.
ii). Vitendo vya Watu kupigwa, kinyanyaswa, kuwekwa ndani, Kushikilia, Washiriki wa Uchaguzi ili wasifanye kazi zao kwa Uhuru. Hii ni njia mojawapo ya Serikali kuleta Migogoro. Serikali 2015 ilitumia dola kunyamazisha watu waliokuwa wanafanya kazi za Kidemokrasia. Ndo maana uchaguzi uliopita wa 2020 Wanahabari waliogopa wakihofia yaliyotokea 2015. Waliogopa watavunjiwa Vyombo, kupigwa na kupotezwa. Huu tayari umeshakuwa mgogoro wakati wa Uchaguzi.
iii). Kitendo cha CHADEMA kuikataza TBC kurusha matangazo yao, ni Mgogoro mwingine kati ya vyama vya siasa na Tasinia ya habari wakati wa Uchaguzi
iv) Uchaguzi 2015, Chadema kilikuwa chama mbadala bara na CUF Chama Mbadala Zanzibar. Lakini Tume ya Uchaguzi ilifuta Uchaguzi Zanzibar na kutaka Uchaguzi urudiwe kitendo ambacho CUF walisusa. Ukawa Mgogoro mwingine kati ya Tume ya Uchaguzi na vyama vya siasa. Wakarudia UCHAGUZI viongozi wote wakawa wa chama kimoja kinyume na katiba yao, ili kuondoa aibu wakawateua Baadhi ya viongozi wa vyama vya Upinzani kujaza nafasi zilizokuwa za CUF kinyume na Sheria. Sheria inasema chama kitakachoingia kwenye Serikali ya Umoja wa kitaifa ni kile kilichoshika nafasi ya pili, lakini walioshirikishwa kwenye hiyo Serikali hawakuwa na sifa. Ikawa Serikali liyoyumba. Sio kosa la CUF bali kosa la ZEC ndo chanzo cha Mgogoro Zanzibar. Tulijaribu kuwasuruhisha, Wakasema Rais ameshaapishwa, hata kama CUF wamesusa tutaunda Serikali.
v). Uchaguzi 2020 Zanzibar ulikuwa na Mgogoro pia. Vyama viliweka pingamizi ZEC kwa mgombea wa ACT, nia ikiwa ACT kuzuiliwa kuingia kwemye uchaguzi, hawakutaka ACT Wazalendo ipande juu. Huu ukawa mgogoro wa vyama kwa vyama.
vi). Migogoro mingine ni wakati wa kujiandikisha kupiga kura. Watu wanajiandikisha zaidi ya mara moja, wengine wanajiandikisha hawajafikisha Umri, wengine wamekufa lakini wapo kwenye daftari la kudumu. Hi ni migogoro. Inatakiwa kila baada ya muda wa miezi kadhaa daftari liboreshwe lakin hapa tanzania daftari linaboreshwa baada ya miaka mitano. Huu ni mgogoro.
vi). Migogoro mingine ni wakati wa Teuzi. Zanzibar kama hujakaa nchini miaka mitatu, huteuliwi.
vii). Mgogoro Mkubwa hivi sasa ni wa kisheria. Aliyetangazwa mshindi wa Urais anatakiwa apingwe mahakamani sababu anakuwa bado ana sifa kama wagombea wengine. Sheria ya sasa inasema mtu akishatangazwa Mshindi wa urais hatakiwi kushitakiwa popote wala kupinga matokeo yaliyompa Ushindi. Sheria inabidi ibadilishe ili kama katumia rushwa kushinda ashitakiwe, au katumia dola kuingia madarakani ashitakiwe. Kasema swala la Katiba mpya hapa ndipo utaona umuhimu wake. Nchi inahitaji Katiba mpya ili tuwe na rais mwemye vigezo vya kuwa rais
Jaji Tendwa ametaka tunatakiwa tuwe na kumbukumbu za kesi za Uchaguzi sehemu moja. Pia kataka sheria za Uchaguzi ziwe kwenye kapu moja ili watu wazijue. Kataka elimu ya Uchaguzi itolewe kwa Mahakimu, Mawakili, majaji, Wanahabari, asasi za kiraia na Polisi na Jamii kwa Ujumla.
Jaji Tendwa amekili kwamba Sheria ya sasa imempa msajili madaraka makubwa ya kutokushitakiwa kwa kosa lolote. Yule ni mtumishi wa umma, anaweza kukosea kwa makusudi au bahati mbaya. Kwa nchi ya utawala wa Sheria, hii sheria ni mbaya. Msajili ni binadamu kama wengine,ni mwajiriwa wa Serikali. "Msajili wa vyama vya siasa analindwa sana. Mimi Ofisini nlikuwa na walinzi nane, nyumbani 6 na nikitembea wawili. Nlikuwa kama mfungwa, ikabidi niwapunguze, ofisini akabaki mmoja mchana na mkoja usiku, nyumbani mmoja". Kasema Jaji Tendwa.
KUHUSU WAPIGA KURA KUPUNGUA KWENYE UCHAGUZI 2020
Msaji mstaafu wa vyama va Siasa Jaji Mstaafu John Tendwa, amesema;
i). Sababu za kiuchumi ndo zimefanya watu wapungue kwenye vituo vya kupiga kura.
ii). Kitendo cha wapinzani kususa kugoma mijadala ya bunge saa nyingine kutoingia bungeni kutetea hoja za wananchi wao kiliwakatisha tamaa wananchi.
iii). Wengi ya Wagombea walipita bila kupingwa, hii iliwafanya watu wasiende kupiga kura
iv). Wengine hawakwenda kupiga kura sababu kutokana na Kampeni zilivyoendeshwa walishajua nani atashinda
v). Watu hawakuwa na hela mfukoni, wakaona waende kupiga kura ya kazi gani.
vi). Elimu ya mpiga kura haikutolewa. Walioingia miaka 18 kuanzia mwaka 2015 hadi 2020, hawakupata nafasi ya kupata elimu ya Mpiga kura
vii). Miundo mbinu mibovu ilichangia.
Jaji Tendwa ameongeza mwaka 2015 Vyama vya upinzani vingeshinda Uchaguzi kama kungekuwa na alliance.
Mahakama imetakiwa kutenda haki kwa kufuata misingi sio Ushabiki wakati wa kesi za Uchaguzi. Tendwa kasema hadi sasa Mahakana zinafanya vizuri. Akichukulia mfano wa Jimbo la Bunda ambapo Mgombea wa CCM alishindwa akaenda mahakamani ambapo napo alishindwa.
Wakati wa Uchaguzi haki zetu za Msingi hazizingatiwi. Tunawekwa ndani.
Kasema kwa nchi za Afrika Demokrasia yake ni ya Kivita. Wakati wa Uchaguzi wa Kidemokrasia unakuta vyombo vya usalama vipo tayari tayari.