Uchaguzi 2020 Msajili wa Vyama ameionya CHADEMA kwa kuongeza ubeti wa 3 katika Wimbo wa Taifa jana katika Mkutano wa Baraza Kuu

Uchaguzi 2020 Msajili wa Vyama ameionya CHADEMA kwa kuongeza ubeti wa 3 katika Wimbo wa Taifa jana katika Mkutano wa Baraza Kuu

Ikiwa kisheria wimbo wa Taifa ni hizo beti mbili basi ukiongezeka ubeti wa tatu huo kisheria siyo wimbo wa Taifa tena ila wimbo tu wa mtaani.

Tatizo ni kama huo wimbo una patent kisheria.
Haina. Waache wasumbuke.
 
Chadema ni chama ambacho kilianzishwa kwa lengo moja tu la kuvuruga amani ya nchi.
 
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi ameionya CHADEMA kutokana na alichokiita uvunjifu wa sheria kwa kuongeza ubeti wa tatu kwenye wimbo wa Taifa.

Ameeleza kuwa kitendo hicho kilifanywa jana wakati Baraza Kuu la CHADEMA lilipokuwa likimpendekeza atakayepeperusha bendera ya Chama hicho katika nafasi ya Urais.

Msajili amesema, "Nimesikitishwa na kitendo cha kuvunja sheria kwa makusudi kilichofanywa na CHADEMA cha kuchukua wimbo wa Taifa na kuongea aya"

Amesisitiza, "Kwa hili ambalo limefanyika na CHADEMA ni kama kunajisi wimbo wa Taifa. Nataka kuwaonya wakati wanaendelea na mikutano yao, waheshimu sheria za nchi."
hawa nao wameunajisi wimbo wetu🙄😛😛😛
 
Mkishazidiwa hoja ndilo kimbilio lenu, amani, amani, amani.
Yaani jamaa kama Agents wa shetani kabisa,

Hawawezi kukaa bila kusumbuana na vyombo vya dola, kma hivi basi huko waliko wanafurahi sana.
 
Kwani kuna ubaya gani kufanyia Remix huo wimbo?
[emoji3][emoji3]
 
Mwambie mumeo lissu hatujaribiwi.
mbona umefura kama umekula hamira bibie? hebu tuimbie hapa walichoimba chadema na kuvunja sheria. au kama umejaa nyembe nenda mahakamani ukashtaki kuliko kukaa hapo kwenye key board na kuanza kujiliza kama umetelekezwa na bwana
 
Kuvaa nguo za chama na kufanya makosa hakumaanishi chama kimekosa. Lakini Chama kikiwa kwenye vikao vyake halali, huku uongozi mzima wa kichama tena kitaifa kudiriki kuvunja sheria hakiwezi kujivua 'dhambi' hii. Chadema jana walikuwa kwenye vikao halali na wamefanya kosa hilo, hivyo kama wanajielewa wawaombe radhi watanzania mara moja.

Mtanzania anayejitambua hawezi kuchezea wimbo wa Taifa.
yaani wamevunja sheria kwa kumuomba Mungu aibariki Chadema na watu wake? kosa hapo ni nini?
 
Back
Top Bottom