Msajili wa Vyama vya Siasa: Nitavifuta CHADEMA na CUF

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,905
Reaction score
4,054
Msajili wa Vyama vya Siasa, amedai wote watakao kiuka kuvunja vikundi binafsi vya ulinzi vya vyama hivo atavifuta.

Amedai kama Katiba zao zinatambua jambo hilo walifanyie mabadiliko haraka.

Tamko hill limetolewa kwa ushirikiano wa IGP Mangu kwa niaba ya Jeshi la polisi na ofisi ya msajili.


My Take.

Niwazi kwa ubishi wa CHADEMA bila shaka kitafutwa katika medani za siasa.

=========================================



Chanzo: Mwananchi
 
Kitengo kingine cha Maintarahamwe AKA MACCM kikitumika vizuri kuelekea kwenye kura ya maoni na uchaguzi Mkuu. Kati ya CHADEMA na Mainterahamwe sijui ni yupi alianza kuwa na vikundi binafsi vya ulinzi.
 
"KAMA katiba zao zinaruhusu wazifanyie marekebisho"...

Ina maana huyu msajili hajawahi kuzisoma hizo katiba. Sasa huwa anaenda ofisini kila siku asubuhi hadi jioni kufanya nini!
 
Aanze na ccm wafute chipukizi na wengine watafuata hiyo ni njia ya kuzuiya uhuru wa vyama kulinda wizi wa kura na kwanni hili limetangazwa muda mfupi tu kuelekea uchaguzi?tunamashaka sana na msajili na mangu wana ajenda ya siri ambayo ipo wazi kwamba wana njama za kuibeba ccm.
 
Kishapewa muongozo toka Lumumba Mkuu Tuko abwabwaje hadi kutoa povu kuhusu issue hii.

"KAMA katiba zao zinaruhusu wazifanyie marekebisho"...

Ina maana huyu msajili hajawahi kuzisoma hizo katiba. Sasa huwa anaenda ofisini kila siku asubuhi hadi jioni kufanya nini!
 
Last edited by a moderator:
GREEN GUARD ya MACCM vp??!! Wale si ndio wanafanya magwaride huku wakiwa na bunduki kabisa??!!

Green Guard wanatumiwa kwenye sherehe zao mbele ya raisi na mawaziri na jeshi la polisi likishangilia na tena wakiwemo watoto wadogo wanaopewa bunduki,CCM mnaita Chipukizi-chipukiziwa ujambazi au ufisadi,mbona mmekaa kimya??!!
 

Cdm kama ingekuwa ni mwanamume basi unge hatarisha ndoa yake
 

Mutungiphobia loading...........futa uone moto wake!
 

Mkuu huyo mutungi na mangu hawana ubavu wa kulazimisha cuf na cdm kufuta hivyo vikundi bila kuvifuta kwanza green guard hapo ndio patachimbika
 
"KAMA katiba zao zinaruhusu wazifanyie marekebisho"...

Ina maana huyu msajili hajawahi kuzisoma hizo katiba. Sasa huwa anaenda ofisini kila siku asubuhi hadi jioni kufanya nini!

Hayo ndio maajabu ya msajiri. Katiba zote anazipitisha yeye sasa anauliza nini? This means anajua kwamba katiba zao zina accomodate kitu hicho ndio maana anasema wafanye marekebisho.
Hivi yeye kama msajiri si anajua process za kurekebisha katiba? Anataka warekebishe kisirisiri? Je atawapa gharama za kuitisha vikao vya kurekebisha katiba?

Kama katiba zao zina accomodate kitu ambacho kina kwenda kimyume na katiba ya nchi na yeye ndiye alizipitisha nani wa kuwajibika zaidi yake?
 
Msajiki Mutungi na Mkuu WA Polisi Mangu, vipi chama kikiunda kikosi cha mbwa katika kujilinda? Nauliza hivi kutokana na kukaa kwenu kimya kuhusu kuanzishwa kwa kikosi cha ulinzi cha mafisi na CCM. Je hamuoni hatari kwa watu kushambuliwa na manyang'au kwenye mikutano ya kampeni.

CCM ilianzisha kikosi cha kigaidi cha Green Guard mkakaa kimya, wakaanzisha kikosi cha mafisadi na wezi mkakaa kimya, wakaanzisha kikosi cha mafisi mkakaa kimya...je tuwaeleweje? Kwa nini polisi wameshindwa kuithibiti CCM?
 
Ha!Ha!Ha!Ha!, naona ccm wameamua kuibuka na njia mpya ya kutoa maagizo kwa mtungi,afute cdm na cuf aone moto utakavo waka.
 

Mkuu huu ni uongo usiokua na maana!Hizo habari si za kweli ni kujaribu kupotosha kauli sahihi aliyoitamka msajili.Fuatili kwa makini na uisome habari hiyo uone jinsi ambavyo vyombo vyetu vya habari vinatumika, Waandishi wamekua makanjanja kuhangaikia matumbo yao tu.Jana siku ya Alhamisi nilisikiliza mwenyewe kwa masikio yangu kauli aliyoitoa msajili kupitia redio ya VOA alichokisema,Alichokisema ni kwamba ni halali kikatiba kua na vikundi vya ulinzi katika vyama lakini visiwe na mwelekeo wa kuunda jeshi,akamalizia na kusema kua vyama vyenyewe vikae na kupitia katiba za vyama vyao na visivuke mipaka ya kikatiba.Sikusikia popote akisema kua atavifuta vyama tusipende kukuza mambo kumsingizia msajili.
 
haiingii akilini kuwa hawajawahi kusoma katiba za hivi vyama vya siasa na sheria ya vyama vya siasa kiujumla,vipi kuhusu vijana chipukizi wa chama tawala or green guard,je nao watahusika au itakua double standards?
 
walinzi wao wenyewe na malipo ni yao wenyewe kinachowauma nini? Polisi ingebidi ivishukuru vyama kwa kuwa wabunifu na kuweka ulinzi kwy mikutano kusaidiana na polisi kudhibiti usalama wa watu na mali zao kwani kazi hiyo kutokana na uchache wa polisi hawana uwezo wa kudhibiti kila mikutano na tumeshasikia mara nyingine mikutano ikiairishwa kisa hakuna polisi kwahiyo vyama viendelee kutumia walinzi wao kujilinda ni dhana nzuri. kama mimi mtu mmoja na familia tuna walinzi wa kulinda nyumbani kwangu itakuwa mkutano mzima ambao unajaza mamia ya watu .

otherwise mkingangnia tutajua munataka wasiwe na walinzi ili ccm itume wahuni kufanya vurugu bila kudhibitiwa mmechelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…