Msajili wa Vyama vya Siasa: Nitavifuta CHADEMA na CUF

Msajili wa Vyama vya Siasa: Nitavifuta CHADEMA na CUF

Kuongelea kufuta CHADEMA NA CUF kwasasa amechelewa.

hawa wamekomaa na kutambulika ndani na nje ya nchi.

Nikama kauli ya kichaa au ndoto ya mwendawazimu. Anajidhalilisha maana wanaotishiwa nyau ni watoto tena wadogo sio cdm & cuf hawa wamekomaa.
 
Aanze na ccm wafute chipukizi na wengine watafuata hiyo ni njia ya kuzuiya uhuru wa vyama kulinda wizi wa kura na kwanni hili limetangazwa muda mfupi tu kuelekea uchaguzi?tunamashaka sana na msajili na mangu wana ajenda ya siri ambayo ipo wazi kwamba wana njama za kuibeba ccm.

Huu ni ushahidi kwamba kujipendekeza ni maradhi hatari sana. Vyama hivyo vilisajiliwaje, CCM je, leo ndo ameliona hili.
Nafasi hii ya ujaji Tanzania inachezewa sana na ndiyo sababu mkulu wa nchi anaweza kuteua majaji hata 10 kwa mpigo kila mwaka. Maneno haya kama yamesemwa na jaji, tumekwisha. Maana huyu anatishia amani kwa kiasi kikubwa, wakubwa wake wamkanye leo.
 
vp ataifuta na kwenye mioyo ya Watanganyika au atafuta kwenye makaratasi kwa kutumia correction fluid?! asipoangalia atafutika yeye.
 
Aanze na CCM kwanza yeny green guard wanaotumia bunduki ndo avifute.
 
Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama kurekebisha katiba zao kwenye kipengele kinachoruhusu kuanzishwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama.

Vyama vyenye vikosi cha ulinzi na usalama ni Chadema chenye Red Brigade, CCM (Green Guard), CUF (Blue Guard) na sasa ACT-Wazalendo (ACT Amani).

Mutungi alisema uanzishwaji wa vikundi hivyo unakwenda kinyume na Katiba ya nchi inayolipa jeshi la polisi mamlaka ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

Akizungumza baada ya mkutano wake na vyama hivyo jana, Jaji Mutungi alisema katiba za vyama vingi vilivyosajiliwa kabla hajaingia ofisini vilikuwa na kifungu kinachoruhusu kuanzishwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama wa mali za chama au viongozi wao wawapo katika mikutano.

“Haturuhusu kifungu hicho kuwapo kwenye katiba za vyama vinavyosajiliwa sasa (hakugusia ACT - Wazalendo). Hatuvifundishi vyama vya siasa namna ya kuandaa katiba zao lakini tunasimamia kifungu hiki kwa vile kinapingana na sheria.”

Jaji Mutungi alisisitiza kuwa vyama vya siasa nchini havina uelewa wa sheria ya vyama vya siasa ambayo ndiyo inayovisimamia, ndiyo maana vinashindwa kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria hiyo




Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Jamani hili gazeti nalo limekua la udaku tena?
Alichosema ni halali vyama kua vikundi vya ulinzi kulinda mali zao ila visiwe na mwelekeo wa kuunda jeshi!Mwishoni alimalizia kwa kusema hivi vyama vikae na kupitia katiba zao!Sikusikia popote akisema viondolewe kabisa.
Chanzo changu: VOA Jana saa 1:30 jioni.
 
hizi ni hatua za kupongeza kwa vyombo hivyo kuchukua hatua.

na sisi wananchi ni jukumu letu kuliunga mkono hilo kwa maana ni kwa faida yetu wenyewe.

tujiulize ni nchi gani imewahi kupata maendeleo kwa makundi kuwa na vikundi vya kijeshi au ni nchi gani zimewahi kuvurugana kwa makundi katika jamii kuwa na makundi ya kijeshi.

tuhamasishe vyama vya siasa kuunda vitengo vya kupanga mipango ya maendeleo na kumkataa yeyote anayeonyesha mwelekeo wa kuunda kitu cha kutufanya wakimbizi, kupoteza kila tulicho nacho kama tutabahatika kubaki tukiwa hai.

hili tusilifanye mtaji wa kisiasa bali huu uwe ujumbe wetu sote kwa makundi yoyote.
 
unaweza kufuta vyama vyote lakini huwezi kuifuta kiu ya mabadiliko kutoka kwa mioyo ya watanzania,
 
"KAMA katiba zao zinaruhusu wazifanyie marekebisho"...

Ina maana huyu msajili hajawahi kuzisoma hizo katiba. Sasa huwa anaenda ofisini kila siku asubuhi hadi jioni kufanya nini!

Huwa yuko facebook na hapa JF anaperuuuzi
 
Aanze na ccm wafute chipukizi na wengine watafuata hiyo ni njia ya kuzuiya uhuru wa vyama kulinda wizi wa kura na kwanni hili limetangazwa muda mfupi tu kuelekea uchaguzi?tunamashaka sana na msajili na mangu wana ajenda ya siri ambayo ipo wazi kwamba wana njama za kuibeba ccm.

siku hizi haiitwi chipukiza bali Green Guard
 
Kuifuta chadema ni sawa na kufuta watanzania katika uso wa dunia!
 
Mkuu huu ni uongo usiokua na maana!Hizo habari si za kweli ni kujaribu kupotosha kauli sahihi aliyoitamka msajili.Fuatili kwa makini na uisome habari hiyo uone jinsi ambavyo vyombo vyetu vya habari vinatumika, Waandishi wamekua makanjanja kuhangaikia matumbo yao tu.Jana siku ya Alhamisi nilisikiliza mwenyewe kwa masikio yangu kauli aliyoitoa msajili kupitia redio ya VOA alichokisema,Alichokisema ni kwamba ni halali kikatiba kua na vikundi vya ulinzi katika vyama lakini visiwe na mwelekeo wa kuunda jeshi,akamalizia na kusema kua vyama vyenyewe vikae na kupitia katiba za vyama vyao na visivuke mipaka ya kikatiba.Sikusikia popote akisema kua atavifuta vyama tusipende kukuza mambo kumsingizia msajili.

acha usanii wako
 
Huyu anafikiri kuifuta chadema ni rahisi kaa kupoga katerero! Ajaribu aone
 
Msajili aliyemtangulia naona kafutika na sasa hata hasikiki tena! sijui bado yupo nchi hii!

na yeye aliwahi kusema hivi hivi kwamba ataifuta Chadema! naona alifutika yeye!
 
hqdefault.jpg

Green Guard Zanzibar ni Imara zaidi ya Chuma.​
images

Hao vijana nialali. Ila nyie mnaovaa zambarau na bluulazima muwekwe ndani
 
waanze na green guard kuifuta kwanza. :tape2::tape2::tape2::tape2:
 
Back
Top Bottom