IGP Mangu na Msajili Judge Mutungi, kwani hii dhana ya ulinzi shirikishi imeondoka baada ya IGP mwema kustaafu au haihusiani na vyama vya siasa? Kama elimu imekuwa ikitolewa kwa kiasi kikubwa raia washiriki katika ulinzi na usalama wa wao wenyewe na mali zao kwa sababu jeshi la polisi halina uwezo wa kuwa na idadi ya askari wa kuifanya kazi hiyo kwa ukamilifu, nini kinachokuja kwa tamko lao hili kuwa USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO NI KAZI YA POLISI na raia (kupitia vyama vya siasa) wasihusike katika ulinzi?
Je! Wanatuambiaje au wanatoa ufafanuzi gani juu ya ULINZI NA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO kwa kuangalia haya yafuatayo:- 1). POLISI wenyewe, 2). WANAMGAMBO, 3). ASKARI WA JIJI, 4). PRIVATE SECURITY COMPANIES (Hapa ni utitiri wa makampuni na Polisi ndiyo watoa vibali). 5). GREEN GUARDS, 6). RED BRIGADE, 7). BLUE GUARDS, 8). "ZAMBARAU" GUARDS, 9). SUNGU SUNGU, 10). POLISI JAMII, 11). NEIGHBOUR HOOD WATCH, 12). KOROKORONI, etc. etc.
Inawezekana kutofautisha maana ya USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO na kazi inayofanywa na vikundi, majeshi au watajwa wengine hapo juu?
Kutakuwa na kuchanganyikiwa sana kwa watu wengi endapo msajili na IGP wataanza kujaribu kusema nani anahusika na ulinzi au usalama hapo.
WATAFAKARI KABLA YA KUCHUKUA HATUA kwa kufuata maelekezo ya kupotosha ya walioshika hatamu kwa sasa.