Msamaha kubutuliwa, Ndugai aungwe mkono

Kwa kauli zile za Mama, hata huo msamaha wa JN inaonekana amefanya kwa shinikizo baada ya kutonywa kwa yajayo. Lazima kuna mtu kavujisha siri ili amuokoe Mzee wa Galilaya. Wakaona kuomba radhi hadharani inaweza kunusuru.
Mimi sikuona sababu ya Mshenga wa Yesu (Ndugai) kuomba radhi maana alichokiongea ni kweli tupu.
 
wafuasi wa chadema wakiongozwa na mzee Mbatia wamepoteza mwelekeo kabisaa...yaani wanachezeshwa ngoma bila kujua wimbo
Unajiona mjanjaaaa! Kwa taarifa yako hakuna kuchezeshwa wala nini. Tunachoshuhudia ni mtifuano halisi.
 
Tatizo brazaj unasahau mapema sana.
CCM lao moja huo NI mpango wao.wanafanya wanagombana ili wawatoe mchezoni
NANI ANAMKUMBUKA MBOWE MAHABUSU?
Free mbowe imeishia wapi?
 
Kwani yeye haogopi!?
 
Kwa kuipata katiba mpya ya wananchi.
Shida ya wanasiasa wetu wakichukia mtu wanchukia na kile anachokisema ata kama kitakuwa kizuri au chenye faida kwake.
Kama ntu mnaa , unaa ukikomaa unageuka usaliti.
 
Hataki kabisa! Ndio maana amekua mkali
 
Ameomba msamaha haya mambo yaishe tusonge mbele
Tutasonga vipi mbele wakati mtu kakopa trillion 10 ndani ya miezi 9 kwa ajili ya madawati tena bila idhini ya bunge, na hajatubu wala Kuomba msamaha?! How do we move on?! Tukija kupigwa mnada je?!
 
Tatizo brazaj unasahau mapema sana.
CCM lao moja huo NI mpango wao.wanafanya wanagombana ili wawatoe mchezoni
NANI ANAMKUMBUKA MBOWE MAHABUSU?
Free mbowe imeishia wapi?

Tunajua mnaumia mno na hoja yoyote yenye mwelekeo wa maridhiano.

Mbowe, Lissu, Ling'wenya, Adamoo, Ben, Mawazo, Lijenje au wa kwenye viroba wanasahauliwa na nani?

Ushauri wa bure kwenu Makamanda na wanamageuzi watukuka

Jipya lipi tumeanza kuliandika leo?

Ungali ukitusikia nusu nusu?
 
“Sasa 2025 mtaamua mkitoa waliopo nayo sawa waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa, endapo hiyo namna ya ku-run nchi (kuongoza nchi) hivi sasa deni letu ‘seventy trilioni’ (Sh70 trilioni). hivi nyinyi si wasomi ‘is that healthy’ (hiyo ni afya). Kuna siku nchi itapigwa mnada hii,” alihoji Ndugai kwenye mkutano huo wa kimila wa kabila la Wagogo
 
Binafsi siwezi muunga mkono
 
Kuondoka Kwa waliolivuruga taifa, sii kwa maneno yake ya hivi karibuni, ila kwa mipango na mikakati ya makusudi, ama kwa kujua au kutokujua au kwa uwezo wa kutekeleza jukumu lake la msingi Kwa nafasi aliyoitumikia/anayoitumikia ni fursa na nafasi Kwa mtu mwenye weledi kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya taifa na manufaa ya watanzania, tukiiona ni fursa ya kisiasa, sidhani kama ni sahihi, ila yafaa tulione hili kama fursa kwa maslahi mapana kwa taifa, na mwanzo wakurekebisha dosari zinazolikwamisha taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…