Au amnyan'ganye kabisa Zari, hahahaa hapo hata Masogange itaanza kupigwa kwa upya kabisa na kwenye top ten itakuwepo, chezea skendo ww.
Akili za mende aliekunywa sumu!
Hiyo avatar yako imenikumbusha mbali sana.
Binafsi huyu dogo nimemkubali from the very first song! Hayo uliyotaja ni chanzo hususani hapo kwenye RED lakini in addition, ambalo nalo pia linachangiwa hapo kwenye RED, hivi sasa ukitaka uendelee kusikika basi na wewe mwenyewe hutakiwi kujipoteza bila sababu za msingi! Radio station huwa zinapokea nyimbo nyingi sana kwa siku hususani zile radio pendwa! Sasa msanii hata kama utatoa pini kali namna gani, ukipotea itafika wakati pini lako nalo litapotezewa coz' kila siku new hits zinaingia sokoni! Hivi sasa si kama zamani... mashabiki wana access na kusikiliza wimbo husika kupitia various sources; kwa sasa zaidi kupitia kwenye simu na kidogo kwenye radio na kwenye mitandao! Nyimbo ikiwa hit, kama usafiri wako ni daladala kila siku, basi kuna uwezekano kwenye kila route wimbo husika utasikika! Kutokana na hilo, it's obvious baada ya muda wimbo utapotezewa tu coz' mtu utakuwa umesikia mara kadhaa... angalu mara kumi kwa wiki!
So, ikiwa msanii utakuwa unakaa sana bila kutia nyimbo mpya, then prepare yourself to be left behind! Hata wewe Mkuu wangu Ruttashobolwa ingawaje unamkubali Diamond, nikikuuliza Nitampata Wapi umeisikiliza lini mara ya mwisho si ajabu huwezi kukumbuka! Now assume Chibu anakaa miezi sita bila kuachia track... si ajabu ndani ya hiyo miezi sita huyo Diamond utakuwa umesikiliza mara chache tu na zingine ni zile za kugongana na nyimbo husika just by chance!
So, pamoja na mchango wa mashabiki, msanii mwenyewe anatakiwa kuji-boost! Huyu Kiba ambae kila leo siku hizi Kiba, Kiba! tayari alishapotea coz' mwenyewe ali-opt kujipoteza!
Mimi hajanikosea chochote na namkubali sana tu.Nyimbo zake alizowahi kuzitoa hakuna niliowahi kutokuupenda hata mmoja! Hata mimi hua nashangaa kwanini hatoki? Laiti ningekua na uwezo ningempa hata tuzo moja tu ya kumfariji.
Kilichomsaidia Kiba ni kwavile tayari alishakuwa na base ya mashabiki... ukishakuwa na base ya mashabiki, hata ukikaa kimya kwa muda gani, bado mashabiki wako watakuwa wanakusubiria kwa hamu na ukirudi vizuri watakupokea tu! Belly 9 alikuwa bado hajajenga fans base itakayokaa kumsubiria kwa hamu... kujenga fans base ni zaidi ya kutoa nyimbo mzuri! Kujenga fans base si kazi ndogo kama watu wanavyodhani hususani kama unakuja na kutoka! Fans base mara nyingi zinakuwa na makundi makubwa mawili... kama vile Yanga na Simba, Barcelona na Real Madrid, Inter na AC Millan, Man U na "Liverpool", East Coast na West Coast (USA), East Coast na TMK, n.k!Umeongea ukweli mtupu mkuu..
Kuna wasanii wachache tu ambao huu mziki ni kama wao hata wakae kimya kwa mda gani wakija na ngoma kali tu wanatoka tena..
Mfno😀ully sykes,Mr:Blue..
Na hata kiba kwa jinsi alivokaaga kimya mda mrefu mi nilijua hatorudi tena lakin alinishangaza jinsi Mwana Ilivo hit utadhani ndo anatoka upya..
Belle 9 kama matonya tu wanaimba vizuri ila ndo hivo...hadi nimehisi kuwaonea huruma
Sidhani kama swala ni kuwapigia magoti labda kuwa karibu na wadau wamuziki lakini nini kina mshinda?
Mkuu unapotaja "WADAU WA MYUZIKI" ktk bongo flavor, huna namna but you have to surrender all you have to BONGO FLAVOR OWNERS.
Hao msanii hana namna ya kuwakwepa ili awe juu, ndio maana mdau hapo juu kasema "AKAWAPIGIE MAGOTI"
Labda tuweke kumbukumbu sawa, siku hizi walaji hatuli tutakavyo, tunalishwa wanavotaka hao niliowaita BONGO FLAVOR OWNERS
Unaweza ukanisaidia kitu hiki, siku hizi SAID FELLA ananunua album nzima ya msanii, na huku tunajua hana Tv wala radio, unategemea nini hapo?
Ni kwamba kazi ya kununua albam ni ya shabiki, sasa siku hizi fella ananunua kwa niaba yetu, hii inamaanisha tutaiskiliza au niseme tutasikilizishwa aina hiyo ya myuziki by hook by crook.
Fella, Babu Tale, Ruge, to mention the few, wamehodhi media, wakaenda mbele kidogo, wakahodhi makampuni makubwa, bado wakahodhi na wasanii, yaani WAKWETU vs SIWAKWETU.
Nini kifanyike, kwa umoja wangewashinda hawa lkn kwa ubinafsi wao, wasanii wataendelea kupata ROI low or nothing at all!
Said Fella ni mfanyabiashara, sawa na Mamu au Wananchi! Kuna kitu watu hatujakijua... kuna hits kibao za kitambo ambazo hadi leo watu wanazi-feel na hawajui watazitoa wapi! Hata wewe leo hii ukifanya collection ya hits kali za zamani ukawapa jamaa chao, basi una uwezekano mkubwa sana wa kufanya biashara... ama kwa ku-risk kupitia uuzaji wa CDs au hata kupitia web medias kama Mikito! Unanunua album, unaiingiza sokoni... simple tu!Unaweza ukanisaidia kitu hiki, siku hizi SAID FELLA ananunua album nzima ya msanii, na huku tunajua hana Tv wala radio, unategemea nini hapo?
Hebu nisaidie kitu kimoja
kuna kampuni ngapi zinazofanya biashara ya muziki wa simu
'callertunes' na ringtones'
na hizo kampuni ni zipi na za nani?
Said Fella ni mfanyabiashara, sawa na Mamu au Wananchi! Kuna kitu watu hatujakijua... kuna hits kibao za kitambo ambazo hadi leo watu wanazi-feel na hawajui watazitoa wapi! Hata wewe leo hii ukifanya collection ya hits kali za zamani ukawapa jamaa chao, basi una uwezekano mkubwa sana wa kufanya biashara... ama kwa ku-risk kupitia uuzaji wa CDs au hata kupitia web medias kama Mikito! Unanunua album, unaiingiza sokoni... simple tu!
Hii kweli kabisa aiseekamfanya masogange kuwa maarufu zaidi kuliko yeye kwa kumtumia kama video queen.
Kwa hiyo unajaribu kusema wanamuziki wote wanao fanya vyema kwa sasa wana kwenda kwa Waganga? Unamshauri aende kwa waganga?