Msanii Belle 9 amewakosea nini Watanzania? Kwanini anapuuzwa? Ni wapi anakosea?

Msanii Belle 9 amewakosea nini Watanzania? Kwanini anapuuzwa? Ni wapi anakosea?

Binafsi naona scandal ndo zinawapaisha watu. Bila scandal si rahisi kuwa kwenye media hivyo ni rahisi kusahauliwa na mashabiki
 
Nahisi tatzo nyota belle9 ni msanii mzur sana lakin ata tuzo huwa hapat
 
Jibu lipo wazi mbona!! Belle 9 aache kufanya muziki kizamani. Atafute Management Nzuri inayoeleweka. Sio hao wakina Mona gangstar.
 
Yaan mi mwenyew roho yangu huwa inaniuma sana juu ya belle9, huwa sielew why so much regardless to him, najtahd kila mwaka kumpigia kura na kuangalia kaz zote anazotoa, najifarji kwa stail hyo.mfano mzuri ni ule wimbo aliomshirikisha joh makin "vitamin music" wimbo mzur sana bt ndo vle zzzzzzzzz
 
Hebu wekeni picha yake tumuone, wengine ndio tunamsikia leo
 
Binafsi huyu dogo nimemkubali from the very first song! Hayo uliyotaja ni chanzo hususani hapo kwenye RED lakini in addition, ambalo nalo pia linachangiwa hapo kwenye RED, hivi sasa ukitaka uendelee kusikika basi na wewe mwenyewe hutakiwi kujipoteza bila sababu za msingi! Radio station huwa zinapokea nyimbo nyingi sana kwa siku hususani zile radio pendwa! Sasa msanii hata kama utatoa pini kali namna gani, ukipotea itafika wakati pini lako nalo litapotezewa coz' kila siku new hits zinaingia sokoni! Hivi sasa si kama zamani... mashabiki wana access na kusikiliza wimbo husika kupitia various sources; kwa sasa zaidi kupitia kwenye simu na kidogo kwenye radio na kwenye mitandao! Nyimbo ikiwa hit, kama usafiri wako ni daladala kila siku, basi kuna uwezekano kwenye kila route wimbo husika utasikika! Kutokana na hilo, it's obvious baada ya muda wimbo utapotezewa tu coz' mtu utakuwa umesikia mara kadhaa... angalu mara kumi kwa wiki!

So, ikiwa msanii utakuwa unakaa sana bila kutia nyimbo mpya, then prepare yourself to be left behind! Hata wewe Mkuu wangu Ruttashobolwa ingawaje unamkubali Diamond, nikikuuliza Nitampata Wapi umeisikiliza lini mara ya mwisho si ajabu huwezi kukumbuka! Now assume Chibu anakaa miezi sita bila kuachia track... si ajabu ndani ya hiyo miezi sita huyo Diamond utakuwa umesikiliza mara chache tu na zingine ni zile za kugongana na nyimbo husika just by chance!

So, pamoja na mchango wa mashabiki, msanii mwenyewe anatakiwa kuji-boost! Huyu Kiba ambae kila leo siku hizi Kiba, Kiba! tayari alishapotea coz' mwenyewe ali-opt kujipoteza!

Umeongea ukweli mtupu mkuu..
Kuna wasanii wachache tu ambao huu mziki ni kama wao hata wakae kimya kwa mda gani wakija na ngoma kali tu wanatoka tena..
Mfno😀ully sykes,Mr:Blue..

Na hata kiba kwa jinsi alivokaaga kimya mda mrefu mi nilijua hatorudi tena lakin alinishangaza jinsi Mwana Ilivo hit utadhani ndo anatoka upya..
 
Last edited by a moderator:
Ungeweka na miziki yake unayoipenda kwenye post ya kwanza ingeanza kumpa promo kimsaada.
 
Mimi hajanikosea chochote na namkubali sana tu.Nyimbo zake alizowahi kuzitoa hakuna niliowahi kutokuupenda hata mmoja! Hata mimi hua nashangaa kwanini hatoki? Laiti ningekua na uwezo ningempa hata tuzo moja tu ya kumfariji.

Ahsante mkuu umesema kilicho moyoni mwangu,,!!!
 
Umeongea ukweli mtupu mkuu..
Kuna wasanii wachache tu ambao huu mziki ni kama wao hata wakae kimya kwa mda gani wakija na ngoma kali tu wanatoka tena..
Mfno😀ully sykes,Mr:Blue..

Na hata kiba kwa jinsi alivokaaga kimya mda mrefu mi nilijua hatorudi tena lakin alinishangaza jinsi Mwana Ilivo hit utadhani ndo anatoka upya..
Kilichomsaidia Kiba ni kwavile tayari alishakuwa na base ya mashabiki... ukishakuwa na base ya mashabiki, hata ukikaa kimya kwa muda gani, bado mashabiki wako watakuwa wanakusubiria kwa hamu na ukirudi vizuri watakupokea tu! Belly 9 alikuwa bado hajajenga fans base itakayokaa kumsubiria kwa hamu... kujenga fans base ni zaidi ya kutoa nyimbo mzuri! Kujenga fans base si kazi ndogo kama watu wanavyodhani hususani kama unakuja na kutoka! Fans base mara nyingi zinakuwa na makundi makubwa mawili... kama vile Yanga na Simba, Barcelona na Real Madrid, Inter na AC Millan, Man U na "Liverpool", East Coast na West Coast (USA), East Coast na TMK, n.k!

Muziki wa Tanzania kwa sasa tayari kuna Diamond na Kiba... hili haliepukiki! Yeyote anayetakiwa kuingia katikakati ni lazima afanye kazi ya ziada huku akiombea mmoja wapo kati ya Kiba na Diamond aporomoke; sawa na ilivyoporomoka Liverpool na nafasi yake kuchukuliwa na Arsenal huku mashabikiwa Liverpool nao wakiwa bado wamekaa mkao wa kula kuisubiria Liverpool yao! Kwavile kuingia kati ya timu kubwa mbili kunategemea sana timu moja kuporomoka, kinyume chake unatakiwa kuwa serious na kazi ili kama hata kama utashindwa kujipenyeza kati kati basi angalau uwe ni mtoa changamoto! Kule UK kuna wakati Newcastle ilifanya hivi na wakaanza kupata mashabiki... wakashindwa ku-maintain na hivyo wakapotea kama alivyokuwa amepotea Belle 9! Wakaja Chelsea wakatia changamoto kwenye EPL na bado kila leo inaendelea kujenga fans base lakini sio rahisi kuchukua nafasi ya Man U or Arsenal unless mmoja wao anapotea! Wameingia Man City na wao wameanza kutengeneza fans base... wakishindwa ku-maintain kama alivyofanya Belle 9, nao watapotea tu coz' bado hawajajenga strong fans base kama ile ya Man U na Arsenal kama ambavyo Belle 9 alikuwa hajajenga strong fans base kama ile ya Diamond na Ali Kiba... fans ambazo nao walizipata baada ya kupromoka kwa kambo mbili maarufu; ile ya East Coast na TMK... hawa nao walipotea kwavile hawakuwa na jipya tena! Kutokana na hilo, utaona kwamba hakuna uchawi wowote zaidi ya kazi za msanii mwenyewe na consistency yake! Huwezi kutoa wimbo mmoja leo au hata mbili kisha unaka kimyaa mwaka mzima halafu ukatarajia ukirudi utapokolewa kwa mashahada na maua wakati hata ulipopotea ulikuwa bado hujatengeneza fans base!
 
Sidhani kama swala ni kuwapigia magoti labda kuwa karibu na wadau wamuziki lakini nini kina mshinda?

Mkuu unapotaja "WADAU WA MYUZIKI" ktk bongo flavor, huna namna but you have to surrender all you have to BONGO FLAVOR OWNERS.

Hao msanii hana namna ya kuwakwepa ili awe juu, ndio maana mdau hapo juu kasema "AKAWAPIGIE MAGOTI"

Labda tuweke kumbukumbu sawa, siku hizi walaji hatuli tutakavyo, tunalishwa wanavotaka hao niliowaita BONGO FLAVOR OWNERS

Unaweza ukanisaidia kitu hiki, siku hizi SAID FELLA ananunua album nzima ya msanii, na huku tunajua hana Tv wala radio, unategemea nini hapo?

Ni kwamba kazi ya kununua albam ni ya shabiki, sasa siku hizi fella ananunua kwa niaba yetu, hii inamaanisha tutaiskiliza au niseme tutasikilizishwa aina hiyo ya myuziki by hook by crook.

Fella, Babu Tale, Ruge, to mention the few, wamehodhi media, wakaenda mbele kidogo, wakahodhi makampuni makubwa, bado wakahodhi na wasanii, yaani WAKWETU vs SIWAKWETU.

Nini kifanyike, kwa umoja wangewashinda hawa lkn kwa ubinafsi wao, wasanii wataendelea kupata ROI low or nothing at all!
 
Hebu nisaidie kitu kimoja
kuna kampuni ngapi zinazofanya biashara ya muziki wa simu
'callertunes' na ringtones'
na hizo kampuni ni zipi na za nani?
 
Unaweza ukanisaidia kitu hiki, siku hizi SAID FELLA ananunua album nzima ya msanii, na huku tunajua hana Tv wala radio, unategemea nini hapo?
Said Fella ni mfanyabiashara, sawa na Mamu au Wananchi! Kuna kitu watu hatujakijua... kuna hits kibao za kitambo ambazo hadi leo watu wanazi-feel na hawajui watazitoa wapi! Hata wewe leo hii ukifanya collection ya hits kali za zamani ukawapa jamaa chao, basi una uwezekano mkubwa sana wa kufanya biashara... ama kwa ku-risk kupitia uuzaji wa CDs au hata kupitia web medias kama Mikito! Unanunua album, unaiingiza sokoni... simple tu!
 
Hebu nisaidie kitu kimoja
kuna kampuni ngapi zinazofanya biashara ya muziki wa simu
'callertunes' na ringtones'
na hizo kampuni ni zipi na za nani?

Ni nyingi tu the boss, wasanii wetu hawaaminiki mbele ya kampuni hizi, wao km wao mpaka washikwe mkono na WADAU!
 
Said Fella ni mfanyabiashara, sawa na Mamu au Wananchi! Kuna kitu watu hatujakijua... kuna hits kibao za kitambo ambazo hadi leo watu wanazi-feel na hawajui watazitoa wapi! Hata wewe leo hii ukifanya collection ya hits kali za zamani ukawapa jamaa chao, basi una uwezekano mkubwa sana wa kufanya biashara... ama kwa ku-risk kupitia uuzaji wa CDs au hata kupitia web medias kama Mikito! Unanunua album, unaiingiza sokoni... simple tu!

Huko kote upo sahihi mkuu! Concern yng kubwa hapa ni kwamba, kwa upande wa Radio stations na Tv, zinapigwa ngoma ambazo Fella na wenzake wamezipeleka, iwe single ama album.

Na ikibidi hata kwa gharama ya "ngoma za msanii x zisipigwe"
 
Kwa hiyo unajaribu kusema wanamuziki wote wanao fanya vyema kwa sasa wana kwenda kwa Waganga? Unamshauri aende kwa waganga?

Ndio, huoni diamond alimuibia Jums nature mganga wake now anashine wakati Nature amepotea kwenye rada.?
 
Back
Top Bottom