Msanii Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya

Msanii Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,788
Reaction score
5,217
pic+chidbenzi.gif


Jeshi la polisi Mkoa wa Ilala, limewakamata watu saba akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12 mwaka huu saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

Amesema jeshi la polisi limefanya msako wake na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa katika eneo ambalo linajihusisha na uuzaji wa dawa hizo.

“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema Hamduni.

Hamduni amesema jeshi hilo linafanya msako liweze kubaini mtandao mzima unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na watumiaji ili kuhakikisha wote wanachukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Itakumbukwa kuwa , Oktoba 24,2014, Chid alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jiji la Dar es Salaam akiwa na dawa za kulevya, akijaribu kuvuka nazo kwenda mkoani Mbeya kushiriki onyesho la Instagramu Party wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria .

Msanii huyo wa kizazi kipya alikiri shtaka hilo na ndipo , Februari 26 mwaka 2015, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipomhukumu kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh900,000 baada ya kupatikana na hatia ya katika makosa matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi na Heroine yenye thamani ya Sh 40,358.

Hata hivyo msanii huyo alifanikiwa kulipa faini na kukwepa kifungo hicho.

Chanzo:
Mwananchi
 
Sijui hata nisemeje yan...daah.!!
Huyu kijana ndoto zake ndo zinakufa pamoja nae hivi....mmmh
 
Ipi bora, vita ya DAB japo ilikua na mapungufu yake au hii ya kimyakimya tuliyoambiwa inaendeshwa ki ustaadi na ufanisi chini ya mteule kamishna?

Hili janga linaangamiza sana nguvu kazi ya taifa.
 
Halafu unamwonea huruma nyau kama chid

Sent from my TV
 
Hiyo ni habari iliyochapishwa kwenye ukurusa official wa gazeti la mwananchi jioni ya leo tarehe 15.08.2017

Inasemekana msanii huyu akiwa na wenzake walikamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin mnamo tarehe 12.08.2017 na jeshi la polisi mkoa wa Ilala na hadi sasa wako msimbazi central wakisubiri upelelezi ukamilike kabla ya kufikishwa mahakamani

Kilichofanya niwe interested na hii habari ni namna vyombo vya habari vilivyofanya haraka sana kutuaminisha kuwa Chid Benzi ameachana na madawa ya kulevya.

Linapokuja swala la waathirika wa madawa, baadhi ya wanajamii huwa na mtazamo hasi hasa Kwa watu ambao huwa wanatamani waathirika wapewe muda zaidi kabla ya kuanza kuutangazia umma juu ya utakatifu wao kwani wanapoanguka tena mapema hivi ni wazi kwamba kupokelewa tena na jamii sio rahisi

Media zinaweza kuwajenga watu lakini pia kuna wakati zinawabomoa kisaikolojia hawa ndugu zetu

Mtu kama Chid Benzi Kwa mtazamo wangu, ilikuwa ni mapema sana kurudishwa mbele ya kamera na kuanza kumsafisha!!

Kwa mujibu wa habari hiyo, mbali na matumizi ya madawa ya kulevya yaliyodhorotesha afya yake ya mwili na akili Kwa kiasi kikubwa sana pia alishawahi kukamatwa na madawa ya kulevya air port akielekea Mbeya kwenye show! Kesi hiyo iliisha Kwa yeye kulipa faini.

Sasa hii ni mara nyingine tena anakamatwa akiendelea na biashara hiyo tena baada ya kutoka sober house!!?

Anapoanguka mapema hivi, waliompa mbeleko wana nini cha kutueleza!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa nafikiri wale mliokuwa mnawapa Lawama Tale kuachana kabisa kumsaidia huyu.mzigo mtakuwa sasa mmemuelewa Tale..

Huyu Chidd nafikiri jela ndio itamfunza zaidi kuliko kupeleka Soba...
Huyu ni kichwa cha mwenda wazimu kabisa...
 
Back
Top Bottom