Msanii Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya

Msanii Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya

Inamaana Biashara ya Madawa ya Kulevya inaendelea kwa kasi kuliko zamani ile duh!
 
af ndo siku iyo iyo alipotumbuiza kwenyr tamasha pale taifa kumbe alivotoka pale ndo akakutwa akiuza madawa duuuh
 
af ndo siku iyo iyo alipotumbuiza kwenyr tamasha pale taifa kumbe alivotoka pale ndo akakutwa akiuza madawa duuuh
 
Lakuvunda halina ubani...ujanja mwingi mwingi mwisho wake majanga.Pole Chid Benz. Hauimbi tena...hausikiki tena kwa mazuri bali mambo yasiyo faa. Kama utapata wasaa jaribu kujikumbusha kwamba ngoma ikilia sana huwa inapasuka

Ni mimi nduguyo, Rogojin The Idiot
 
Sasa nafikiri wale mliokuwa mnawapa Lawama Tale kuachana kabisa kumsaidia huyu.mzigo mtakuwa sasa mmemuelewa Tale..

Huyu Chidd nafikiri jela ndio itamfunza zaidi kuliko kupeleka Soba...
Huyu ni kichwa cha mwenda wazimu kabisa...
kwakweli kiusalama wake wangemfunga hata miaka mitatu tu
 
Hawa serikali ndo inawalea sana, au kwakuwa wengi walizungunga na mgombea urais wa chama tawala 2015? Walipaswa kuwa gerezani hawa. Mi nashangaa serikali inahangaika kuwapeleka kwenye rehab...... Weka Segerea tu huyu!!!
Segerea atakufa na arosto, nina bro wangu alikufa early 2000's R.I.P Yusuf (MAKAMBA) alikuwa anasumbua sana baada ya kujiingiza kwenye ulaji ngada. Anapelekwa special care anaondolewa sumu anakuwa freshi kisha baada ya muda anatoroka home anaeda kunyeta, ikafikia stage akaanza udokozi wa vitu ndani mikanda ya mzee, viatu anaenda uza ili apate unga. Mara jirani akalalamika ameibiwa redio yake na anahisi Yusuf ndo kaiiba, ikawa msala...

Baada ya mzee kuchoka hio tabia ya kumuonya na mtu hasikii akamsusia polisi wakamtia ndani. Mpaka kufikia two weeks alizidiwa sana polisi wakamuachia huru arudi home. Hakumaliza week la 3 akawa kasha udanja!

So kumtia ndani bila kumtoa sumu mwilini jua anaenda kujifia huyo jamaa. Na ubaya jamaa huwa hawasikiagi hao yani wanakuwa kama wana laana!
 
pic+chidbenzi.gif

Jeshi la polisi Mkoa wa Ilala, limewakamata watu saba akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12 mwaka huu saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

Amesema jeshi la polisi limefanya msako wake na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa katika eneo ambalo linajihusisha na uuzaji wa dawa hizo.

“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema Hamduni.

Hamduni amesema jeshi hilo linafanya msako liweze kubaini mtandao mzima unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na watumiaji ili kuhakikisha wote wanachukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Itakumbukwa kuwa , Oktoba 24,2014, Chid alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jiji la Dar es Salaam akiwa na dawa za kulevya, akijaribu kuvuka nazo kwenda mkoani Mbeya kushiriki onyesho la Instagramu Party wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria .

Msanii huyo wa kizazi kipya alikiri shtaka hilo na ndipo , Februari 26 mwaka 2015, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipomhukumu kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh900,000 baada ya kupatikana na hatia ya katika makosa matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi na Heroine yenye thamani ya Sh 40,358.

Hata hivyo msanii huyo alifanikiwa kulipa faini na kukwepa kifungo hicho.

Chanzo:
Mwananchi
Kwa hapa jamaa alipofika inabidi gwajima nae atoe mchango wake
 
Hiyo ni habari iliyochapishwa kwenye ukurusa official wa gazeti la mwananchi jioni ya leo tarehe 15.08.2017

Inasemekana msanii huyu akiwa na wenzake walikamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin mnamo tarehe 12.08.2017 na jeshi la polisi mkoa wa Ilala na hadi sasa wako msimbazi central wakisubiri upelelezi ukamilike kabla ya kufikishwa mahakamani

Kilichofanya niwe interested na hii habari ni namna vyombo vya habari vilivyofanya haraka sana kutuaminisha kuwa Chid Benzi ameachana na madawa ya kulevya.

Linapokuja swala la waathirika wa madawa, baadhi ya wanajamii huwa na mtazamo hasi hasa Kwa watu ambao huwa wanatamani waathirika wapewe muda zaidi kabla ya kuanza kuutangazia umma juu ya utakatifu wao kwani wanapoanguka tena mapema hivi ni wazi kwamba kupokelewa tena na jamii sio rahisi

Media zinaweza kuwajenga watu lakini pia kuna wakati zinawabomoa kisaikolojia hawa ndugu zetu

Mtu kama Chid Benzi Kwa mtazamo wangu, ilikuwa ni mapema sana kurudishwa mbele ya kamera na kuanza kumsafisha!!

Kwa mujibu wa habari hiyo, mbali na matumizi ya madawa ya kulevya yaliyodhorotesha afya yake ya mwili na akili Kwa kiasi kikubwa sana pia alishawahi kukamatwa na madawa ya kulevya air port akielekea Mbeya kwenye show! Kesi hiyo iliisha Kwa yeye kulipa faini.

Sasa hii ni mara nyingine tena anakamatwa akiendelea na biashara hiyo tena baada ya kutoka sober house!!?

Anapoanguka mapema hivi, waliompa mbeleko wana nini cha kutueleza!?

Sent using Jamii Forums mobile app
umeongea sana KAKA...MADAWA KUACHA NI MTIHAN SANA HASA KWA MTU KAMA BENZ...AMERUDI MAZINGIRA YALEYALE .......KUNA MWAFLAN NAE MI NAMUHESABIA MIAKA TU LAZIMA ATAREJEA TENA.
 
Watoto wenu wakiguswa ndio mtamkumbuka Makonda kuwa alikuwa akifanya jambo la maana kupambana na wauzaji wa madawa kwani ni wauwaji hawa watu..
 
umeongea sana KAKA...MADAWA KUACHA NI MTIHAN SANA HASA KWA MTU KAMA BENZ...AMERUDI MAZINGIRA YALEYALE .......KUNA MWAFLAN NAE MI NAMUHESABIA MIAKA TU LAZIMA ATAREJEA TENA.
mwana wa mwenzio muombee mema sio useme unamuhesabia miaka fulani atarudia....omba Mungu amuepushe
 
Huyu jamaa sasa kwisha habari yake duuh kweli ngada mbaya sana, amtafute Ray C ampe siri ya mafanikio yake.

Determination, hayuko determined.
Rayc alikuwa na lengo akaanguka kanyanyuka tena. Ni kazi ngumu sana kuacha madawa, kama huna nia unachemka tu
 
Back
Top Bottom