Msanii Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya

Msanii Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya

Unaweza kuwa na tatizo dogo lakini vile unalitatua lisikupe matokeo chanya au matokeo ya kuonekanika.Roho ii radhi lakini mwili u dhaifu. Kuna vitu vingine wakuna nafsi ndo inayougua sasa ukimpeleka magereza sana sana utamzika huyu mtu. Kuitibu nafsi lazima ujue alianzaje kuna stori ndefu. Kati ya haya mawili hakuna mwenye nia ya dhati ya kumsaidia huyu kijana au wote wanaojaribu kumsaidia hawajui jinsi ya kumsaidia.
Naafiki na unachosema. Wanasaikolojia wanaweza kutupa ushauri juu ya namna bora ya kushughulika na waathirika wa, si madawa tu, bali hata wa hali ngumu ya maisha!
 
Kamanda aliyechukua nafasi ya makonda ajiuzuru tu hajui analifanya au anapokea mrungula dawa walizokamata itakuwa ndio hizo wanazowauzia kina chidi
 
pic+chidbenzi.gif


Jeshi la polisi Mkoa wa Ilala, limewakamata watu saba akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12 mwaka huu saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

Amesema jeshi la polisi limefanya msako wake na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa katika eneo ambalo linajihusisha na uuzaji wa dawa hizo.
Sikio la kufa halisikii dawa!
“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema Hamduni.

Hamduni amesema jeshi hilo linafanya msako liweze kubaini mtandao mzima unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na watumiaji ili kuhakikisha wote wanachukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Itakumbukwa kuwa , Oktoba 24,2014, Chid alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jiji la Dar es Salaam akiwa na dawa za kulevya, akijaribu kuvuka nazo kwenda mkoani Mbeya kushiriki onyesho la Instagramu Party wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria .

Msanii huyo wa kizazi kipya alikiri shtaka hilo na ndipo , Februari 26 mwaka 2015, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipomhukumu kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh900,000 baada ya kupatikana na hatia ya katika makosa matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi na Heroine yenye thamani ya Sh 40,358.

Hata hivyo msanii huyo alifanikiwa kulipa faini na kukwepa kifungo hicho.

Chanzo:
Mwananchi
 
Adhabu kali inabidi zichukuliwe dhidi yake, maana wanabebwa sana hawabebeki
 
Pole yake.sielewi kwa nini kuacha hii kitu ni ngumu.wengi hurudia kutumia.

kuna dakatri alinambia, mwanaume ukiwa una ejaculate ukiwa unafanya mapenzi, ile raha unayopata yake ni dopamine 300 units, mtu akitumia Heroin akivuta ile raha anayoskia ni dopamine 1500 units (mara 5 ya wakati wa ku ejaculate), so u can imagine io level ya happiness anayokua nayo mtumiaji akiwa high. ndo maana ni ngumu kuacha ile kitu.

nmenukuu
 
Hakimu utakayesikiliza hiyo kesi mpeleke jela moja kwa moja bila kutoa option ya faini labda akitoka huko atakuwa raia mwema
 
Back
Top Bottom