Emanuel Makofia
JF-Expert Member
- Jan 5, 2010
- 3,832
- 635
Hajarudia bali anaendela hajawahi achaKarudia tena?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hajarudia bali anaendela hajawahi achaKarudia tena?
Naafiki na unachosema. Wanasaikolojia wanaweza kutupa ushauri juu ya namna bora ya kushughulika na waathirika wa, si madawa tu, bali hata wa hali ngumu ya maisha!Unaweza kuwa na tatizo dogo lakini vile unalitatua lisikupe matokeo chanya au matokeo ya kuonekanika.Roho ii radhi lakini mwili u dhaifu. Kuna vitu vingine wakuna nafsi ndo inayougua sasa ukimpeleka magereza sana sana utamzika huyu mtu. Kuitibu nafsi lazima ujue alianzaje kuna stori ndefu. Kati ya haya mawili hakuna mwenye nia ya dhati ya kumsaidia huyu kijana au wote wanaojaribu kumsaidia hawajui jinsi ya kumsaidia.
Ni sawa na wewe uambiwe uachane na JF 😀😀Pole yake.sielewi kwa nini kuacha hii kitu ni ngumu.wengi hurudia kutumia.
Wanajiendekeza 2 na ujinga wa kuiga mambo ndio faida yake hiyoIpi bora, vita ya DAB japo ilikua na mapungufu yake au hii ya kimyakimya tuliyoambiwa inaendeshwa ki ustaadi na ufanisi chini ya mteule kamishna?
Hili janga linaangamiza sana nguvu kazi ya taifa.
Duwh humuelewi barnaba mkuu aseeBinafsi sijuagi BARNABA sijui SHILOLE wanaimbaga nini
Me tooBinafsi sijuagi BARNABA sijui SHILOLE wanaimbaga nini
![]()
Jeshi la polisi Mkoa wa Ilala, limewakamata watu saba akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12 mwaka huu saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.
Amesema jeshi la polisi limefanya msako wake na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa katika eneo ambalo linajihusisha na uuzaji wa dawa hizo.
Sikio la kufa halisikii dawa!
“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema Hamduni.
Hamduni amesema jeshi hilo linafanya msako liweze kubaini mtandao mzima unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na watumiaji ili kuhakikisha wote wanachukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Itakumbukwa kuwa , Oktoba 24,2014, Chid alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jiji la Dar es Salaam akiwa na dawa za kulevya, akijaribu kuvuka nazo kwenda mkoani Mbeya kushiriki onyesho la Instagramu Party wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria .
Msanii huyo wa kizazi kipya alikiri shtaka hilo na ndipo , Februari 26 mwaka 2015, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipomhukumu kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh900,000 baada ya kupatikana na hatia ya katika makosa matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi na Heroine yenye thamani ya Sh 40,358.
Hata hivyo msanii huyo alifanikiwa kulipa faini na kukwepa kifungo hicho.
Chanzo: Mwananchi
Teja habebekiAdhabu kali inabidi zichukuliwe dhidi yake, maana wanabebwa sana hawabebeki
Pole yake.sielewi kwa nini kuacha hii kitu ni ngumu.wengi hurudia kutumia.
Simuelewi hakika. Naona anapiga mayowe tuDuwh humuelewi barnaba mkuu asee
kuna dereva wa daladala za Mwananyamala Stesheni anaita Cyborg yeye alienda Kigamboni na ameacha kabisa...kuacha yale madude si kazi ndogo
yaani ni ngumu kama kuacha puri.