Msanii Country Boy Rasmi Ameachana Na Recording Label Ya Kondegang

Msanii Country Boy Rasmi Ameachana Na Recording Label Ya Kondegang

Kichwa Ze Don

Senior Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
198
Reaction score
321
Leo Tarehe 08/01/2021 Kupitia Ukarasa Rasmi Wa Instagram Wa Kondegang Umethibisha Mkataba Wa Country Wizzy Na Kondegang Umefika Tamati ...,

Kuanzia Sasa Country Wizzy Atakuwa Msanii Anayetegemea ..., Za Chini Ya Kapeti Killy Na Cheed Nao Wanataka Kujitoa Ila Boss Wao Harmonize Anataka Gharama Zakuvunja Mkataba.

1641672337276.jpg
 
Hapa angekuwa Sadala hii thread ingekuwa inakimbilia page ya 10,watu wangeanza kutunga yao "........mara jamaa ana roho mbaya......kila siku anataka kuwa yy.........hawapi madogo nafasi........Sallam huyo ana roho mbaya.........".

Kumanage label inahitaji kujitoa na hata kujinyima mwenyewe, ndicho alichofanikiwa Sadala, yupo tayari kuahirisha au kusitisha projects zake ili ampromoti msanii wake. Sasa Harmonize miaka miwili kaachia nyimbo nyingi nje ya album zake mbili na zote zina hitaji promo, bado wasanii wake nao anatakiwa awapigie promo mwisho wa siku wasanii wanaona kama wanatengwa.

Ila nawaonea huruma Cheed na Killy, bora tu wangebaki Kings au wangekuwa wao wenyewe, ila wakitoka watakuwa na hali mbaya. Sijui Country kama amaetoka vizuri au vibaya. Kama vibaya tusubirie tu nae atoe siri za kambi ambazo zinaweza kuwa kweli au uwongo wenye nchumvi na pilipili juu.
 
Wasanii wengi upstairs hamnazo kabisa. Hivi msanii mwenye fikra zake anaweza kuthubutu kwenda kusainiwa na Harmonize? Simdhatau ila yuko rush katika utendaji wake wa kazi na isingekuwa kuwasimamisha wasanii 5 kwa muda mfupi huu ambao yeye mwenyewe anafight asianguke.
 
Leo Tarehe 08/01/2021 Kupitia Ukarasa Rasmi Wa Instagram Wa Kondegang Umethibisha Mkataba Wa Country Wizzy Na Kondegang Umefika Tamati ...,
Kuanzia Sasa Country Wizzy Atakuwa Msanii Anayetegemea ..., Za Chini Ya Kapeti Killy Na Cheed Nao Wanataka Kujitoa Ila Boss Wao Harmonize Anataka Gharama Zakuvunja MkatabaView attachment 2074076
Country boy kwa upande wangu niliona toka ajiunge na konde gang alishuka. Kuna kipindi nilianza kuona kama mziki wake ulikuwa una take off, zile ngoma za vijana kama kibegi, wanaona haya na ngoma zake nyingine za trap zilifanya poa sana.
Ila ghafla mambo yakawa ovyo.
 
Huu mtindo Harmonize kakurupuka sana kingine country wizzy kama mavoko yaani wako level sawa na Harmonize

Kama walivyokuwa mavoko na sadala so maslahi yataleta tatizo

Harmonize bado hana mirija mingi ya kupiga pesa nae anategemea kutoa ngoma maisha yaende na show sa ni mbaya sana mfano anatoa hits nyingin daily kulinda soko lake
 
Back
Top Bottom