Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususan upande wa biashara....nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo Magumu kwa wengi wetu...ijapokuwa na mimi ni Miongoni mwa walio ndani ya janga hili, lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho, nitoe kusaidia kulipia kodi za Nyumba kwa miezi Mitatu mitatu kwa familia 500, walau kusaidiana Katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi hivi vya Corona...Licha ya kuwa Tiafa moja lakini siku zote mmekuwa Familia yangu kupitia Muziki wangu, hivyo naamini Shida yenu ni yangu, na Tabasamu lenu ni Langu pia.
Jumatatu nitaweka rasmi Utaratibu wote wa namna gani Familia Hizi Mia tano zinaweza kupata kodi hizo ya Nyumba....🙏🏼
Maoni yangu: hapa zinaweza kuwa nyumba zisizozidi kodi ya elf 50 kwa mwezi, ila tukikadiria ni elf 50 basi ni 150,000 kwa miezi mitatu, hivyo kwa nyumba 500 ni takribani milioni 75, Ni kiasi ambacho ni kingi ila kijana kajipinda hivyohivyo, Hongera sana