Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Nina bahati mbaya ya kukutana na wasanii wakiwa washaporomoka. Niliwahi kukutana cheed benzino twitter pub ikiwa inavuma, niliwahi kukutana na wema sepenga hapo hapo jirani na twitter kwa frank fundi wa kitimoto. Niliwahi kukutana msanii sio maarufu sana kule ubungo pale tanesco ndani ndani kuna bar ya mwenyekiti, nilimwona anakunywa chibuku mimi ndio nikampiga tafu kilimanjaro 2 kubwa.
Chidi nimekutana nae juzi kimara mwisho Hana mwili kabisa yaani Mimi nae yeye Mimi baunsa [emoji2]

Amekaa kijiweni kimara mwisho
 
kipindi naifahamu Facebook, rafiki yangu mkubwa alikuwa Marehemu Steve Kanumba....

hili hakuna ambae ange amini ila simu niliyo kuwa natumia enzi hizo ilikuwa ya button na haikuwa na uwezo wa ku screenshot kama ilivyo leo.

masaa machache kabla Kanumba hajafa tulichat nikawa nampa hongera ya ubunifu wake kwenye kazi yake ya Anko J.J ambayo ilikuwa hot sana enzi zile.

Muda kama wa saa 6 hivi kuelekea saa 7 usiku nikaona walaka mrefu ulio andikwa na Thesi {mdogo wake Kanumba ambae pia ni Marehemu R.I.P} andiko hilo la Thesi lilielezea tukio zima Lili lotokea hadi Kanumba akafikwa na Umauti.

lakini ni kama Thesi aliandika haraka haraka kisha akaifuta ile post kule Facebook. kwani baada tu ya kulisoma lile bandiko lilifutika siku liona tena hadi leo😭​
 
siku moja nipo stendi ya mabasi yaendayo mikoani UBUNGO...nilikutana uso kwa uso na JOYCE KIRIA...kipindi hicho alikuwa hot kweli kweli hakuwa mnene kama hivi sasa. sikuweza kuzungumza nae chochote🤣🤣🤣🤣

nilipo muona Nikajisemea nahitaji kufanya kazi na huyu mtu. sikuwa na namba yake na wala sikujua zilipo ofisi zake.

mtandao wa Instagram ulinisaidia JOYCE KIRIA akawa Rafiki yangu mkubwa na boss wangu pia {hadi leo japo sifanyi nae kazi ila ni mwanangu sana}

kupitia Joyce Kiria. nimewahi kukutana na kuzungumza na Paul Makonda, kipindi akiwa mkuu wa mkoa na alivyo itishaga mkutano wa wafanya kazi wa Bar pale mlimani city mimi na team yangu ndio tulio muunganisha na watu hao hadi ukumbi ukajaa🤣🤣🤣

kupitia Joyce Kiria niliwahi kuzungumza kwa kirefu na Shilole nilimpenda sana japo ni mtu ambae bila pombe awezi kuwa vile mnavyo muona...{sorry for this} kipindi hicho mgahawa wake wa shishi food ulikuwa pale near airtel head office. Shilole alini hadithia jinsi shishi food ilivyo anza.


niliwahi kuonana na Rinna pamoja na Maua Sama...nilicho kigundua mastar wa bongo wakionana kwenye sehemu za starehe huwa wengi awapeani hi. wanakwepana😭😭😭😭

asilimia kubwa ya mastar wa bongo ni zero brain kuna mmoja kabla hajawa maarufu kwenye story za hapa na pale likaniambia eti akitaka kusafiri anatumia passport ya ndugu yake🤣🤣🤣 huyu dada nilimuona fala sana ngoja nilihifadhi jina lake.

mtaa niliokuwa naishi enzi za utoto tulikuwa jirani na H.MBIZO mzee wa nilonge nisi longe...{R.I.P} huyu mwamba alikuwa poua sana ila enzi hizo anatoa hicho kibao mimi nilikuwa mdoga sana nipo darasa la 3🤣🤣🤣

kupitia H.mbizo nilimuona Q chief.
 
Lost Boyz Mr cheeks ilikuwa club bill billcanas
Brenda fussie ilikuwa sea clif hotel
Yvonne chakachaka nlikutana naye agies record
Hao wakina sugu tushakutana mara kibao tu
Wengine nmewasahau

Ova
Hii ya mr chicks nafkiri ni ile LB walikuja bongo miaka ile...
Mmoja akavuliwa pete kimasta...!

Ila mrangi we ni masta..hv unamjua Mkali? Au masawe Alikuaga Azam kijiwe zamani?
 
Duly sykes, lady j dee, harmonize, lulu. Hao nakutana nao sana na kuwasiliana. Wengine wengi mno nakutana nao mikocheni kwa Papaa Mudilo. Leo naenda nyumbani lounge madam komando kaniita kwa kazi fulani ya kiufundi.
Mkuu ww ni fundi?
 
Back
Top Bottom