Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Nakumbuka kwangu enzi nipo Arusha miaka ya 2016 , Nlikuwa na kawaida ya kwenda club D maeneo ya Moshono.

Siku ya siku wakaja kina Mr Blue na Rommy Jons ambae alipewa u DJ.

Cha ajabu hatukuwa wengi sana, hatukufika hata 30,

Basi ikawa Mr Blue ananipa mic sana tu niwe nafuatiliza nyimbo zake maana nilikuwa nimezikariri nyingi.

Ilikuwa poa sana ile siku kwangu, Jamaa yupo peace hana makuu


!
!
Nash Mc, Sugu, Jiz Mabovu, Skwiza, na Mke wangu
 
Nishawahi mchezea rafu ya makusudi Stamina pale Mazimbu ground ili nione itakuwaje.
 
Kuna msanii mmoja enzi hizo akiwa mchekeshaji na sasa ni mtangazaji mkubwa sana sita taja jiana lake

Tulikua nae mitaani anaishi kwao na mama yake, alikua anatupiga sana mizinga ya ninunulie konyagi ndogo na nauli za kwenda kufanya shooting na kutuomba nyumba kama location
Binafsi amefanyia shooting kwenye geto langu

Sasa hivi akija mtaani na ndinga yake kuja kumsabahi mama yake anatupita full vioo vya tinted hata salamu tu hakuna

Siku moja tukamtolea uvivu kwa mama yake ni jirani na grosary tukapaki gari tuka mblock ikabidi aje grosary kuomba gari itoke ili atoe yake
Wananzengo wakaanza kumpa makavu live kwamba hatutaki hela zake ila salamu tu kama enzi hizo
Basi kuanzia siku hiyo akawa lazima ashuke aje tupige stori sana na kama yupo njema anatembeza konyagi huyo
Mpoki ndiyo kawaida yake ana zarau sana
 
Afande Sele, nilionana nae maeneo karibia na Sinde, wayback 2006. Yuko simple sana, anapiga stori kama siyo star vile enzi hizo.
Huyu jamaa kuna siku nilimkuta mtaani amelewa chakari, anaongea maandazi tu! Jicho nyanya!
 
Mpoki ndiyo kawaida yake ana zarau sana
Screenshot (84).png
 
Mboso ..tangu hajawa star Hadi sasa tukikutana maeneo ya kwao akija kutembea na Mimi nikiwa maeneo hayo salamu za hapa na pale..yupo poa Sana

Godzila (r.i.p)..enzi hizo naishi mbezibeach tulikuwa tunakutana mida ya jioni pale belinda kwa story za hapa na pale na marafiki zangu

Dullyskyes..kwa mara ya Kwanza tulikutana yahya boutique kino..mazoea yakaanzia hapo jamaa yupo straight hapindishi ukizingua

Nitarudi
mboso kwao?? au ulimanisha kwake
 
Dully sykes zamani sana alikuwa mshikaji nadhani ilikuwa around 2002 au 2003 wakati huo anatembea na "ATU" ,cha kusikitisha ATU alifariki kwa "NGOMA".

Father Nelly alikuwa msela wangu sana enzi hizo wakati nakaa "NGALIMI".
uliona vipimo au ulijuaje ni ngoma mkuu,au ndio macho yanatosha
 
Back
Top Bottom