Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Jux, vanessa, janjaro, a.m recordz tandale, maproducer wakubwa wote, kuna mmoja anaimba nyimbo za dini alishika I phone yangu then anawaambia wenzake kwamba ni yake baadae aliing'ang'ania mpaka nikamuuzie kwa hasara, wanafake sana maisha, kuna dj mmoja wa clouds tulikutanaye bar flan akaja meza yetu shobo nyingi haa mm nabadili magari kla baada ya miezi mitatu mara cjui nn baadae ananipiga mzinga wa ten.
vipi ulimpa?
 
Godzilla nimesoma nae na hata namba yake nilifuta alivyofariki...

Izzo business home boy story nyingi tu

TID nimecheza nae pool table sana tu zamani kidogo miaka ya 2009

Mr blue alikuja street kwetu enzi zile za nyimbo ya blue blue anachana,tunamnunulia bangi[emoji1787][emoji1787].Alikuwa na kigari kdg hivi cheusi sijui vits ile.

Wema ameshawahi kunipa pochi nimshikie wakati anaigiza movies

Marehemu Kanumba amenilipa 7000 kwa kushiriki movies yake ya white maria..

J.B tumegombea mikate shoprite pale kwa sana

Lulu sijui aliniona mimi ndo crush wake tumeshawahi kukutanisha macho pale mlimani city mpk nikajisemea ina maana Lulu ndo kanipenda au mbona ananiangalia km kaona pesa vile[emoji30][emoji30][emoji30]

Hawa sikuongea Racka,Bashe,Mwana Fa,Stamina mapenzi yamemtesa zamami sana alikuwa anakuja kutongoza mtaani kwenu demu anamkataa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
mtaa gani??[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Nilipanda Bajaji!! Na mwinjuma muumin tokea Gongo la mboto!!! Tunakwenda Mnaz Mmoja!!!

Kuna huyu Jamaa Dulayo '' huku Ukonga!!! Mitaa ya Banana Goms!! Anagongea K Vant Tuu!! Ana kitu:

Masanja Mkandamizaji!! Nimekutana Nae sana Ofisin kwetu hapa!!! Japo masihala yake yako vile vile!!!

Baghdad Aliwah kutubeba kweny Uber!!!! Ile siku Tumeita Uber mitaa ya Tazara.....Inakuja simama !! Dereva nikamtambua Baghdad!!!! Daa bas story ziliendelea......mpka chench yangu 7500/ Nilikuachia Mtoto wa Mexixana Baghdad!!!!!!

N.B
U-star zigo la mavi, !!!!!
Kwa kina dullayo bado wanafuga mabata yao? Majumba sita
 
Kuna msanii mmoja enzi hizo akiwa mchekeshaji na sasa ni mtangazaji mkubwa sana sita taja jiana lake

Tulikua nae mitaani anaishi kwao na mama yake, alikua anatupiga sana mizinga ya ninunulie konyagi ndogo na nauli za kwenda kufanya shooting na kutuomba nyumba kama location
Binafsi amefanyia shooting kwenye geto langu

Sasa hivi akija mtaani na ndinga yake kuja kumsabahi mama yake anatupita full vioo vya tinted hata salamu tu hakuna

Siku moja tukamtolea uvivu kwa mama yake ni jirani na grosary tukapaki gari tuka mblock ikabidi aje grosary kuomba gari itoke ili atoe yake
Wananzengo wakaanza kumpa makavu live kwamba hatutaki hela zake ila salamu tu kama enzi hizo
Basi kuanzia siku hiyo akawa lazima ashuke aje tupige stori sana na kama yupo njema anatembeza konyagi huyo
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] alikuwa anavimba
 
QJay nilikutana mara mbili Bukoba, mara ya kwanza mtaani tukaongea mawili matatu, mara ya pili nikakutana nae Club. Songa nilikutana nae Dar, kuna mshkaji wangu ni rafiki yake alikuja nae maeneo ya maskani
anasemaje Songa?
 
2018 nimekutana ba Belle 9 naelekea mwanza nimepanda kisbo tulikaa sit moja yeye alipandia moro akashuka dodoma.muongeaji kawaida tu ila alikua anajishtukia shtukia sasa sijui why...ila usanii ni kazi ngumu sanaa
 
Back
Top Bottom