Msanii Hakeem 5: Wanataka kumteka Mama yangu naomba ulinzi wa Serikali

Msanii Hakeem 5: Wanataka kumteka Mama yangu naomba ulinzi wa Serikali

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Hakeem 5 ametoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kuna watu walienda kwa mama yake usiku majira ya saa sita wakimtaka afungue atoke nje wakidai wao wametumwa na wakubwa na wakijitambulisha kuwa ni polisi hali ilifanya wapate hofu kwanini waende usiku?

Hivyo anaamini hao ni watu wenye nia mbaya ya kumteka mama yake hivyo anaomba ulinzi kwa serikali iwasaidie ili mama yake awe salama maana ana hofu mpaka sasa Sikiliza na utoe maoni yako.

 
Kwa kujua au bila kujua watekaji wanaombwa msaada tena?
Kazi ni kipimo cha utu
 
Mbona hatujawahi kusikia watekaji wameuawa au kupigwa na wananchi, ina maana watekaji hujitekea watu kirahisi bila kupata upinzani? Ndio kusema watekaji wana nguvu kubwa?
Kuna matukio mawili niliyashuhudia yamenipa maswali sanaa, "Polisi walikuwa wanataka kumkamata mtu(wawili wakiwa na uniform,mmoja akiwa kavaa kiraia) sasa wakati wanamkwida yule mtuhumiwa akawa anapiga kelele kumwambia mtu aliyekuwa nae, " chukua simu rekodi video" yule jamaa wa pembeni akatoa smartphone yake na kuanza kurekodi. Cha kushangaza wale askari wakamtishia na yule ila hakuacha kurekodi. Mwisho wa siku waliamua kuacha kumkamata yule kijana na kuondoka na V8 yao nyeusi.
Tukio hili huwa linanipa maswali sanaa,kama kweli walikuwa na haki ya kumkamata yule mtu kwanini waogope kamera??
 
We nawe tuondolee ujinga hapa. Kwani wakija mchana hawawezi kumkuta? Kwanini wakamteke?
Huyo mama anajishugulisha na nini?
We unaweza niona mjinga,
Ila hakuna kitu kinachokosa sababu ????
Muda sana,nlishawahi kusema humu kuwa "huu upepo trend wa kutekana kuna watu nao watapita nao"

Ova
 
Siku hizi kila mtu achunge mzigo wake, polisi wako kwa ajili ya maslahi mapana ya viongozi wa chama 'twawala'.

Utekaji kwa asilimia kubwa inafanywa na hao hao.
Akina Mdude, Polepole n.k wamepotea huku hao tunaowaita polisi wakikaa kimya lakini juzi kati mchina kauawa na masai...chap wahalifu wakatiwa mboroni ili kulinda wachina wasikimbie.
Wengine mkifa poa tu...kifo ni kifo.
 
Back
Top Bottom