Msanii Hakeem 5: Wanataka kumteka Mama yangu naomba ulinzi wa Serikali

Msanii Hakeem 5: Wanataka kumteka Mama yangu naomba ulinzi wa Serikali

Huyo maza kafuatwa na hawara zake anasingizia kutekwa
 
Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Hakeem 5 ametoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kuna watu walienda kwa mama yake usiku majira ya saa sita wakimtaka afungue atoke nje wakidai wao wametumwa na wakubwa na wakijitambulisha kuwa ni polisi hali ilifanya wapate hofu kwanini waende usiku?

Hivyo anaamini hao ni watu wenye nia mbaya ya kumteka mama yake hivyo anaomba ulinzi kwa serikali iwasaidie ili mama yake awe salama maana ana hofu mpaka sasa Sikiliza na utoe maoni yako.

Hakim 5 ,Dully ,Mr Blue ,ALikiba ,Abby skills ni watoto wa kariakoo.

Usikute labda kuna issue za kuuza kiwanja kariakoo.
 
hakeem 5 ni underground mkongwe sio sawa kumuita msanii mkongwe
 
Wakina Davido wana uelewa mpana sana wa mambo ya civic knowledge. Sio hawa wa kwetu.

Huyu anambembeleza Rais na Waziri Mkuu binafsi wamlinde Mama yake.

Mamaako alindwe kwani we nani ???????

Kama wewe una platform, jina na sauti kwenye jamii tetea ulinzi wa jamii nzima. Elekeza nasaha zako kwa mfumo mzima wa ulinzi wa raia. Sio kubembeleza Rais amjali Mamaako. Mamaako ndo alindwe mamaako ye nani ????.
 
Back
Top Bottom