Wewe ushafanya vya haramu vingapi?
Ungekua hushiriki haramu hata huyo msanii ungekua humjui ila kwa kua ukiweka earphone unasikiliza Attitude huku watu wakikutupia Asalaam aleykum tele unajiona kama umeyapatia maisha.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Sawa, naona bado unamkingia kifua swaiba wako, na kusapoti hayo yasiyompendeza Mola wako. Mimi tiari nimefikisha ujumbe/nasaha kwako na kwake pia. Allah awaongoze!
KUSIKILIZA.
Kusikiliza: Mambo yaliyo haramishwa kuyasikiliza kwa kukusudia kuyasikiliza ni maasia na yanaharibu saumu. Na jambo lililo haramishwa kulitamka ni haramu kulisikiliza kwa kukusudia. Mifano ya haya ni kama ifuatavyo:
*Kusikiliza muziki: Kusikiliza miziki na vinanda na zumari kwa kukusudia kumekatazwa na kunaharibu saumu. Kutoka kwa Ibn Abbas R.A.A. kasema, "Kasema Mtume S.A.W,
[13]
صَوْتَانِ مَلْعُونَانِ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ: صَوْتُ مِزْمَارٍ عِنْدَ نَغْمَةٍ، وَصَوْتُ مُرِنَّةٍ عِنْدَ مُصِيبَةٍ.
Maana yake, “Sauti mbili zimelaaniwa duniani na akhera sauti za zumari
[14] wakati wa neema, na sauti ya yule anaelia huku anaomboleza wakati wa musiba”. Pia kasema Mtume S.A.W.,
[15]“
لَيَكُونَنَّ مِن أُمَّتِي أَقْوَامٌ يَسْتَحِلُّونَ الْحِرَ وَالْحَرِيرَ وَالْخَمْرَ وَالْمَعَازِفَ.
Maana yake, “Watakuwepo katika umma wangu watu wenye kuchukulia: Zinaa
[16], na (kuvaa) hariri na (kunywa) pombe na (kutumia/kusikiliza) ala za muziki (kama vile zumari, vinanda, filimbi) kuwa ni yenye kukubalika (yaani watayahalalisha kwa kubadilisha majina yake)”.
*Kusikiliza maneno yoyote ya uongo yaliyo katazwa kisheria au maneno ya kusengenya (kwa ubaya) kwa kukusudia ni maasia na yanaharibu saumu