Msanii Joslin anauza chipsi Sinza Kumekucha

Mimi mwenyewe msanii, nina umri mkubwa kiasi ila bado sijatoka ila sijakata tamaa cuz am doing music for passion only, hope nikitoka nitahit zaidi ya mond bin laden.
Kweli
 
Weka picha ya ushahidi basi
 
Kwa lugha ya mtaani ukiitwa msanii manake ni muongo muongo flani hivi, na karibu sote tu waongo, hivyo sote tu wasanii.
 
Mbona shilole ni mama ntilie

Masanja naye


Ni kawaida, piga kaz ili mtad ikuingize kipato na iwe halali

Maisha ya kuigiza utapigwa dole
 
Bora jamaa anakomaa kiume kuliko PNC ,aliyekuwa analialia.Haya ndio maisha hayana formula,ila ndio utajua hapa bongo hamna washabiki bali oya oya ndio wapo kibao na wale washikadau walio mtumia wamemsusa sasa hivi anapambambana peke yake ndio maisha yalivyo.
 
jambo zuri kuliko wale wanaokimbilia kubugia unga
 
Safi sana, gonga kazi hata kama ni kuuza mkaa, mwenyewe kuna kinglion nimeipaki tu, nikifulia naanza kuendesha bodaboda.
Bodaboda ina hela, sema maaskari ndiyo hawawapendi hawa bodaboda

kama kipindi cha mvua unakula vichwa sana
 
Hongera zake hajaingia kwenye ngada kama Darasa..
 
Hongera sana kwa kujituma kujitafutia riziki yako halali.
 
Ana wateja wengi sana, mpk pa kukaa muda mwingine unakosa, good target amefanya, hongeta sana joslin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…