Msanii Lina Sanga aporomoshewa matusi kwa kuanika picha za nusu utupu za ujauzito wake

Msanii Lina Sanga aporomoshewa matusi kwa kuanika picha za nusu utupu za ujauzito wake

View attachment 504899 Linah apokea kichambo kwa picha hizi

Msanii wa muziki Bongo Linah Sanga, wiki hii ameamua kutoa picha za muonekano wa tumbo lake lilivyo kwa sasa.

Katika moja ya picha, baadhi ya watu na wadau wa msanii huyo wamemtupia maneno huku wengine wakimtaka avae dera kama nia ni kuonesha tumbo lake.

Wengine wameishia kusema "wanga" ni wengi,unaweza kupigwa jicho tu la husda ukaishia kuzaa mjusi.Hali hii imefanya watu waamini ni kinyume cha maadili na kuiga utamaduni wa magharibi kuonyeshatumbo lenye ujauzito
Lijinga sana hili libidada, kuanzia Leo navunja CD zote zenye Nyimbo zake, flash hata memory card nafuta kabisa! Sipendagi ujinga Mimi,!
 
Mbna kina Beyonce wakipiga mnaishia kugonga like... Wabongo acheni unafiki

Hicho ni kipindi kitamu sana kwa kijana ukifika utajua
Hapana, huu ni upuuzi. Anamuonesha nani??
Kama ni furaha ya mimba basi piga picha weka chumbani kwako, ziangalie zikutoshe.
Mi mwenyewe my wife anakaribia kujifungia lakini tumbo lake analijua nesi tu na mimi.
Ya nini hasa??
 
Mnaomtukana hamjui raha ya mtt wa kwanza
Kwani kaishamzaa kwa usalama kwanza? Si angoje azaliwe, anaweza akawa na hilo limimba na asizae au mtoto au mama akafa, we unadhani ujauzito ni jambo la mzahamzaha hivi!
 
Shwaini kabisa... Wanawake wa siku hizi kumbe ni hovyo hivi.. Halafu wanalia hwmawaolewi...
 
Kuna kitu mimi sikielewi katika maisha ya kila siku ya binadamu. Kwanini sisi walimwengu ni wepesi sana kuhukumu maisha ya wenzetu???? Yaani ukisoma bandiko la huyu mwenzetu it is like.....yeye is super human. Na kila mtu inabidi aishi na kuyaona maisha yeye anavyoyaona. What makes you think that you can impose your values on others? Umeshamuhukumu ni Limbukeni, Malaya, hajiheshimu. Sidhani kama uko sahihi. Jitafakari.

Tuache kuhukumu maisha ya wengine. Linah ana amaisha yake. Let her do what makes her happy.

Mimi simjui na wala si shabiki wake huyu dada. Lakini naamini ana haki ya kufanya anayoyafanya na mwili wake.
Mkuu naheshimu mawazo yako.
Lakini, kupiga picha sio kosa. Kila mtu anapiga picha kwa ajili ya kumbukumbu zake.
Shida ni je kwa nini uexpose kwa watu??
Watu wakiona tumbo lako na toothpick zako inawasaidiaje/inakusaidiaje??
Hata mimi nina mke, hata wewe una mke/mme inakusaidia nini kuonesha mwili wako kwa watu wasiohusika??
 
Sawa.kwa kuwa lina ni wa kwanza kufanya hivyo.simtetei.ila kwanini asemwe yeye peke ake.au kwa kuwa Beyonce ni black America hajui kiswahili.
Kuna siku CNN walipost tumbo la Beyonce na kuandika "thats what the America have been waiting for" ningependa uuone jinsi wamarekani walivyo react. Huu ni upuuzi
 
Simuhurumii yeye ila ninamhurumia mzazi wake haswa anapokuwa akiinjilisha...
Ni moyo mkubwa sana lakini ni akheri mtu asikie yaliyo ya sirini lakini si kujianika hivyo...

Mungu anajua kuwa hatupaswi kuhukumu wengineo ila tuache maisha yawe hakimu wake lakini siamini chozi la mzazi wake kama litaenda bure...
Itabidi mzazi astaafu kuhubiri. Maana kama mtoto kamzidi kidogoo kete
 
w

wanajifanya kuiga mila za magharibi ndio tatizo, wameona amberose kapiga picha hivyo na wao haaaooo, badala ya mtu kufanya yako ukaheshimika wao ndio unataka kutuletea yaaale ati ooh Israel na Uingereza hawana katiba, kwani ni lazima tuwafate wao badala ya kufanya yetu?
Katiba inaingiaje hapa wewe?
 
Kuna siku CNN walipost tumbo la Beyonce na kuandika "thats what the America have been waiting for" ningependa uuone jinsi wamarekani walivyo react. Huu ni upuuzi
Kuna watu wanaishi maisha fake mkuu...ingekuwa ndo mm nimempa hiyo mimba unatamani uichukue hadi ikue, but Noway ! Ujinga ujinga ujinga
 
Huyu Dada mshamba Na aliyemwoa pia mshamba,jinga kabisa
 
Katiba inaingiaje hapa wewe?
si ndio mnapenda kuiga mambo ya wenzenu, mie nimetolea mfano tu kuwa kuiga iga hakuna maana, flani kafanya hivi na wewe lazima ufanye vile vile, haina maana, fanya yako uheshimike
 
Huyu dada nilimuona fala siku ile anadai ametoa "mimba kama mbili hivi". Means hana uhakika so huenda ni zaidi ya hizo. Issue si kutoa mimba ila ujinga ni kukiri umetoa mimba kwenye media. Sio kila kitu ulichofanya kila mtu ajue, uchafu mwingine unabaki nao wewe mwenyewe ukimuomba Mungu akusamehe.
Hapo sasa. Halafu unakuta kuna mtu kabisa na akili zake huko mitaani anatamba kabisa kwamba eti huyu ndio dem wake!
 
Back
Top Bottom