Msanii Linah afunguka ashawahi kutoa mimba mara mbili

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
301,221
Reaction score
1,172,274
Kabla ya kupata mtoto wa kike linah afunguka kuwa ashawahi kuchoropoa mimba mbili. Na hayo ndo yalikuwa majibu yake alipokuwa akiulizwa na Mtangazaji Soudy Brown >>>

“Yah nisiwe muongo nilishawahi kutoa mimba kipindi cha nyuma, nilikuwa naogopa kwasababu Baba yangu alikataa mtu kubeba mimba nje ya ndoa” “Mimba nimezitoa, siyo mara nyingi ila naweza kusema kama mara mbilii”:-Linah


Linah akiwa na binti yake
 
anaongea as if ni kitu cha kawaida tu kama kuchinja kuku na kumla, hao wangekuja kuwa binadamu kama wewe lina...hivi mnapeleka message gani kwa mabinti wadogo wanaokuwa?
kama mnazungumzia uuaji kirahisi rahisi hivyo.
hebu piga magoti na ujutie hilo tendo!!
 
Hata kama ni confession si kila kitu ni cha kuongea hadharani... Akumbuke kuna kesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mmmh huwa sielewi mtu unazaa unabaki na kitambi, nu uoga wa kufunga tumbo au? Mastar wetu hawaangalii cha kujibu, kwani lazima ukiri ushatoa looh
 
Kama kweli kaongea hvyo basi linah hana huruma

HALAFU INAKUWAJE MTU ANADECLARE KUWA AMETOA MIMBA MBILI HALAFU VYOMBO VYA DOLA HAVICHUKUI HATUA? AU KUTOA MIMBA SYO KOSA?

UPANDE WA PILI.. HV LINAH HAJUI KUWA ANAHAMASISHA UTOAJI MIMBA KWA WALE WANAOMTIZAMA KAMA KIOO CHAO?
 
Nimewaza hao viumbe aliowaua walimkosea nini...
Yani kisa tu Baba hataki ubebe mimba nje ya ndoa unaua...?
Ona sasa imebumbulika, atajuta!!
 
Kuna watu kwenye huu uzi washatoa/wameshahusika katika kutoa kama 3+ lakini watakuja hapa kuponda na kujidai ni dada/kaka wa malaika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…