FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
- Thread starter
- #21
Kuna sra kwenye Qur'an inaitwa surat Jinn, ni nzuri sana, isome tafsiri yake kidogo:Haya yote ni baada ya kufurahishwa na Koran Sura ya Majini na mashetani aya za Shetain.. Hongera zake kuchagua hell...
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Qur'an 72:
1. Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu! 1
2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi. 2
3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana. 3
4. Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu. 4
5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu. 5
6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi. 6
7. Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume. 7
8. Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo. 8
9. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia! 9
10. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu. 10
Soma zaidi: Al jinn