Msanii Mbalamwezi kutoka kundi la 'The Mafik' afariki dunia ikidaiwa ni kutokana na majeraha ya kupigwa

Msanii Mbalamwezi kutoka kundi la 'The Mafik' afariki dunia ikidaiwa ni kutokana na majeraha ya kupigwa

Mmoja wa wasanii wanaounda Kundi la The Mafik, ajulikanaye kama Mbalamwezi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Msanii mwenzake wanaounda kundi hilo Hamadai amethibitisha.

View attachment 1182580
Caption: Msanii Marehemu Mbalamwezi

Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana ingawa inasemekeana kutokana na majeraha ambayo yanahisiwa kuwa amepigwa. Hata hivyo, uchunguzi zaidi unaendelea kuhusu kifo chake

Aidha, Mjomba wa Marehemu aliyejulikana kwa jina moja tu la Mzee Chifu amesema kifo cha Mbalamwezi kina utata. Amesema marafiki zake waliopeleka taarifa ya kifo walieleza kuwa walikuta mwili wa Mbalamwezi umetelekezwa ukiwa hauna nguo

Mwili wa Mbalamwezi umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

View attachment 1182581
Caption: Kundi la Muziki la The Mafik. Marehemu katikati
Jamaniii haunaaa nguooo tenaaa

Hope alisalimikaa na ....so saaaad
 
Dah si sawa katika wasanii ambao walipatwa na umauti ni uyu tu pekee ajaandikwa jina lake mpk kwenda kaburini sijui anaitwa mbalamwezi kwenye cheti chake awajamtendea haki
 
Dah si sawa katika wasanii ambao walipatwa na umauti ni uyu tu pekee ajaandikwa jina lake mpk kwenda kaburini sijui anaitwa mbalamwezi kwenye cheti chake awajamtendea haki
Jamaa amezikwa na kufa kiboya maskini ..

Yaani sijui alikumbwa na nini
 
Huyohuyo mkuu
Unavyosakata unanikuna mama Eh
Umenilevya na body
Sio chakakacha, wacheza kila ngoma
I wanna marry you, marry you (Uuuh)
Ukinitazama jicho la maringo (Eeeh)
Me nachapa fimbo
Ukiinama, ukiinuka fimbo
yna2 upo wapi nije nikuimbie ufurahi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kna mwanangu mmja alikuwa anawapelekea cnbs
Daily supplier wao Ngj ntamgusa nkionana lzma Atakuwa kwenye masikitiko Sahv ya kupotelewa na mwana

Ova
Najisikiaga raha sana mjani unapotajwa kwenye andiko lolote lile..
 
Kwa huyo ha
wanasema katika dunia ya sasa ya teknolojia ya digitali, information is power.

ila jf siku hizi tunapitwa sana na habari. inawezekana member wengi umri wetu umeenda, hatuwezi tena kukimbizana na kasi ya vijana wa instagram na twitter ktk kutafuta habari.

kule instagram na twitter habari za kifo cha huyu msanii zimeanza kusambaa masaa sita yaliyopita. hapa jf habari hii imeanza kuwa reported masaa mawili yaliyopita.
RIP mbalamwezi.
kwa huyo habari take lazima zitangulie insta huku kuna habari zake za kuwahi kufika mkuu!
 
Amewakosea nini?!
Wameshindwa kumshtaki kwenye vyombo vya sheria ?
Kwanini wamejichukulia sheria mkononi kwa kumuua?!

Inasikitisha shaka! [emoji24][emoji24]

Mungu amfariji mama yake na ndugu zake!
 
Back
Top Bottom