Msanii mpya wa wasafi, Diamond alikurupuka!

brownboy

Senior Member
Joined
Jun 10, 2023
Posts
103
Reaction score
278
Hana vigezo vya kumfanya aonekane wa tofauti na wenzie. Anaimba kawaida Tena bora hata ya lavalava.

Tulitegemea tutaletewa msanii anayeimba kileoleo style za kina Rema, Ruger etc.

Mnatuletea msanii anaimba kama mzee yusuf ama mwandei.

Nope hapa mmebugi wazee
 
Subiri uone. Kuna watu wana uwezo wa kukuuzia mti wakakwambia ni almasi na ukaamini.
Ila dogo anajua mimi sisikilizi singeli ila singeli yake ya kuachana shilingi ngapi niliielewa nikaiweka kwenye playlist. Hasa aliyetengeneza ile beat ameweka sampling flan verse ya kwanza na kwenye intro sampling za vocal ziliipendezesha beat sana
 
Yaan watu hawana jicho la tatu kabisaa...siku ya kwanza tuu namsikia huyu dogo..ubongo wangu uli sense kitu kwake...na sikumpuuza nikajisemea tu moyoni kana uwezo...kumbe sikuona mimi tu...yupo vizur sana..muda ni mwalim mzuri
 
Yaan watu hawana jicho la tatu kabisaa...siku ya kwanza tuu namsikia huyu dogo..ubongo wangu uli sense kitu kwake...na sikumpuuza nikajisemea tu moyoni kana uwezo...kumbe sikuona mimi tu...yupo vizur sana..muda ni mwalim mzuri
Yuo vizuri lakini style yake ya uimbaji na exposure hakuna kitu tunahitaji wasanii broadminded ili kucompete na soko la mziki wa sasa huyo hawezi kucompete na wapopo..huyo hana utofauti na wasanii wengine wa wcb wote waimba taarabu tu
 
Diamond na timu yake wanafanya biashara ya muziki na burudani, wakati sisi tunaona bidhaa haifai watauza na watu watakula.

Wasanii kama Harmonize, Rayvan, Zuchu sio bora ukilinganisha na wengine wenye ujuzi wa sauti na kuimba, ila WCB wameweza kuwakuza na kuwafanya brand kubwa.
 


Wasifu wako? Maana ku challenge mfanya biashara kama diamond kwenye tasnia iliyompa billions inaitaji uwe na cv ya kueleweka.
 
Hajakuletea wewe amejiletea yeye kwa faida na hasara yake, wewe wasikilize wale wanaoimba usasa tu mkuu usiteseke dunia ni pana
 
Mafanikio kwenye.mziki ni zaid.ya.sauti. na mazoezi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…